28yrs kweli chama hakina mtu mwingine wa kuweza kushika nafasi ya uenyekiti! Na wasomi wote hao ndani ya chama. It's a shame. Kwahiyo nijue kuanzia sasa iwapo Mbowe atafariki au kustaafu siasa cdm itakuwa haina mwenyekiti tena. Utani mwingine bana.
Hahaaa kuna jambo nikwambie. tatizo unalinganisha CCM na CDM ndio maana unaona 28 yrs ni mingi sana.
CCM ni chama kikongwe zaidi, kina rasilimali na taasisi wanazoweza kuzitumia kuidhoofisha CDM, tumeona bunge na mahakama zinavyoendeahwa. Sasa kwny mazingira haya CDM lazima wawe makini sn kwa yule watakayempa chama, mbinu za CCM ni nyingi, wanaweza honga mgombea huko nje mumpe chama halafu CDM ndio ibaki historia, na siku CCM wakiipata CDM kwny amgle yao, wataipoteza mazima, siku zote wanataka vyama vyote vya upinzani viwe dhaifu.
Kama siasa za hii nchi zingekuwa za kistaarabu nakuhakikishia Mbowe leo tungekuwa tumeshamsahau, tatizo wengi wa wanasiasa wa nchi hii ni njaa, wana bei, tunaona kila siku uthibitisho wa hili, ni hili sio tatizo la CDM kama chama, ni tatizo la watu binafsi, wapo sehemu kwa maslahi yao, ni wabinafsi japo wana tudanganya vinginevyo.
Sasa niambie, leo CDM waamue kumtoa Mbowe halafu chukulia mfano wampe mtu kama Mwambe kwasababu ndie aliekuwa mgombea pinzani wa Mbowe, mtu aliyeshindwa kuvumilia kukosa ushindi wa uenyekiti, angeweza kuvumilia hila na mbinu chafu za CCM?!
Wengi wa wanaompinga Mbowe ni CCM ukiachilia wachache wenye msimamo kama wako ndani ya chama, sasa huoni kumuondoa Mbowe madarakani hasa kwa wakati huu na awamu hii ni kukaribisha majanga kwa chama? unadhani Magu anataka kiongozi wa upinzani mwenye msimamo km Mbowe? na km asingekuwa Mbowe m/kiti wa CDM leo hii nina hakika hizi vurugu za watu kukimbilia NCCR na CCM mpk CUF leo hii zisingekuwepo, coz km wameshaona wanawamudu kwanini wahangaike na nyie?
Mbowe kawasababisha CCM watenge pesa maalum kwa ajili ya kununua watu toka CDM, wakifika kule wanapewa mpk uwaziri!
Sometimes I blv if you cant defeat them kwa hila zao, basi atlist wakere, ndicho kinachotokea sasa, wacha wapoteze pesa kununua watu ambao naamini watasababisha mgogoro huko kwao mbele ya safari.
Halafu kuna msimamo wako mwingine huwa siuelewi, "no tume huru no uchaguzi" is it practicable on your part? and if the answer is yes, unadhani likitokea litamnufaisha nani? ukumbuke CDM wasiposhiriki watashiriki kina NCCR na wenzie, sijui why unaamini kwenye kumsusia fisi bucha!.