Rais Magufuli anatengeneza upinzani "Pure" utamsumbua sana

Rais Magufuli anatengeneza upinzani "Pure" utamsumbua sana

Uko sawa kabisa kwenye maelezo yako ila nadhani swala lipo palepale, kwa uzoefu wako unadhani nani au akina nani wanafaa kuiongoza CDM badala ya Mbowe.

Miaka 28 chama hakina mtu mwingine wa kuweza kuwa mwenyekiti? Mkuu mambo mengine hata ni aibu kuongea hadharani. Sasa kama chama hakiwezi kupata mwenyekiti mwingine zaidi ya mtu mmoja, tunataka kuchukua dola ili iweje kwa mfano? Au ndio tutawachukua wanaccm wafanye kazi hiyo? Kama ni hivyo ni kwanini tunapambana na ccm?

Kuna watu walikuwa wanamwambia Nyerere akitoka madarakani nchi itayumba, matokeo yake akakaa madarakani zaidi ya miaka 20 hadi wananchi wakawa wanavaa viraka, na kupiga mswaki na chumvi. Alipotoka madarakani, ndio watu wakaanza kuvaa tena nguo zisizo na viraka.
 
Tangu nimeanza kukufahamu leo umezungumza point tupu naona hata nafasi yako katika hicho kitengo cha propaganda umeiweka rehani!

Huwa naongea pointi siku zote, sema hizi za leo hazikuumizi kama hizo nyingine za siku zote.
 
Yes Hadi wanachama watakapoona yatosha, Mandela, Nyerere baada ya takwa la mapambano kutimia waliwaachia wengine so ni subira tu

Kwenye suala la uongozi sio sahihi kuwaweka kapu moja Nyerere na Mandela. Labda kama lengo lako ni kuchangia na sio kuchangia kwa mantiki.
 
Naona kwa sasa mnakubaliana kimyakimya na Dr Slaa.

Muda haujawahi kuniangusha halafu huyo jamaa yenu huwa mnatumia nguvu kubwa kutuaminisha kwamba yupo smart ila ukweli ni kwamba he's just like other "country pumpkins"

Mkuu akina nani wanaokubaliana na Slaa kimya kimya?
 
Lowassa aliletwa Chadema na TISS wakimtumia Apson na Gwajima. bila Mbowe kujua ila badae alikuja kugundua na hakutaka ajue chochote alifanya hivyo pia kwa Sumaye, Masha& Co. Mbowe baada ya kugundua alifanya makosa akaanza kuwafanyia ujasusi na kugundua wote walio kuja kutokea ccm na wimbi la Lowassa hakuna mwenye mapenzi na chama.

Sasa lile wimbi la Lowassa limegundua hawana nafasi mbele ya chadema asili wameondoka wamebaki wale wachumia tumbo ambao walipata ubunge kwa upepo wa fisadi Lowassa. wanatafuta nguzo za chama wakiangamize lakini wapi mbowe kasimama wamekwama.

Sasa Magufuli anatengeneza upinzani pure asili wa wafia chama ambao wapo tayari kwa lolote kuelekea uchaguzi mkuu, Anatengeneza mgogoro ndani ya ccm wa uteuzi wa wabunge mwaka 2020 kama ilivyokuwa kwa chadema mwaka 2015 yaani kiufupi yale waliyoyaita makapi na mafisadi watatumia muda mwingi kuyasafisha wakati chadema watakuwa na wagombea pure 2020.

Sasa wale mnaosubiri chadema ife subiri kura ya hasira ya wanachama wa ccm kwenye makapi.
Haya mfia saccos ya Chadema!
 
Mkuu Slaa na Lipumba ushujaa wao uko wapi? Mtu aliyekimbia mtu kisa hampendi au ana mawaa ana ushujaa gani?Huenda mimi ndio sielewi maana ya ushujaa. Mimi niko cdm siku zote na sijawahi kukubaliana na ujio wa Lowassa ndani ya cdm, na huwa sifichi huo msimamo wangu. Hivi wazee wetu wangekimbia nchi hii kisa wakaloni walikuja kuwatala ingekuwaje? Ndio wangekuwa mashujaa kwa kukimbia?
upo sahihi mkuu lkn uchaguzi upo karibu mno unazani nani anafaa kugombea hususa huko chedema kwa mtazamo wako
 
Kwa hiyo kwako wabunge wale ndio wanaifanya Chadema iwepo. Ushamba wenu ndio uliwafanya mtumie hela za umma kuanza mradi wa kununua wabunge ili Chadema kife! Akili ya kitoto sana, CDM ni watu, CDM iko kwenye mioyo ya watu. Ukitaka kujua hilo, maelfu ya watu wametia nia kugombe ubunge na nafasi za udiwani kupitia Chadema kwa kuomba sio kuombwa, kama vyama vyenu mlivyopandikiza vinavyofanya. na ninakuhakikishia uchaguzi wa 2020 bila mbeleko mnazotegemea za Tume na polisi, asubuhi tu game inamalizika! na wabunge kibao watashinda Chadema! Siasa za hovyo hovyo mnazofanya zinakokota watu "wanaoelewa polepole tu"!
Sawa naona cdm Ina wabunge kibao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwenye ujio wa Lowassa Mbowe alizingua. Ile haikuhitaji intelijensia ya juu kujua kuwa Lowassa alikuwa sio mtu sahihi kwa cdm kwa nafasi hata ya udiwani, achia mbali ya urais.

Mkuu kila siku huwa nasema humu ndani kiongozi mzuri wa kuchaguliwa mwisho ni miaka 10, ukiwa na bahati ya ajabu mwisho ni miaka 15, nje ya hapo ni mauzauza. Hivi majuzi wakati wa uchaguzi mkuu wa cdm nilikuwa wazi kabisa kuwa Mbowe hastahili kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm tena, sio kwakuwa sio kiongozi mzuri, ila aisingweza kuwa na jipya tena. Sababu kubwa ni kuwa kakaa madarakani zaidi ya miaka 15, na kosa la kipuuzi kabisa la kumchukua Lowassa.

Mbowe na cdm wamejiweka kwenye mazingira ya kushambuliwa kisiasa, na kufanyiwa hujuma za wazi kwa sababu ya Mbowe kung'ang'ania madaraka. Hao wabunge wachache wanaohama na kukichafua chama wanapata nguvu hiyo kwanza kwa kuhongwa, na kisha wanatumia hiyo weakness ya Mbowe kukaa madarakani kuhama na kuichafua cdm. Sikufichi hao, wanaohama na tuhuma wanazotoa hata kama zote sio kweli, lakini zaidi ya asilimia 50 zina ukweli. Sisi tuko humu mitandaoni tunaitetea cdm kama taasisi, maana tunajua umuhimu wa upinzani, lakini hatuna uwezo wa kutetea viongozi ving'ang'anizi wa madaraka. Mbowe ana kipi cha maana ambacho kashindwa kukileta ndani ya cdm kwa hiyo miaka 15,ila ataweza sasa? Tusipokuwa wawazi kwa hawa viongozi wa wanaong'ang'ania madaraka kisa tunaipenda taasisi husika, itakuwa ngumu kuwakemea hawa madictator uchwara. Ukweli ni kuwa Mbowe hakustahili tena kuwa mwenyekiti wa cdm, vinginevyo tutajua yuko madarakani kulinda hayo anayochafuliwa nayo. Ni vyema Mbowe kama anaipenda cdm, akae pembeni maana miaka 15 inatosha kwa kiongozi muungwana.
Antipas Mbowe 4 Life
 
Kwa maana ya walikuwa ni wanaharakati

Kwa unaharakati wanafanana. Lakini baada ya uhuru Mandela alikaa miaka minne madarakani akatoka, hakuanza mbwembwe kuwa ndio aliyeleta uhuru. Nyerere alikaa miaka 24 baada ya uhuru, tena baada ya nchi kuwa fukara ndio akatoka. Hii ni tofauti kubwa ya wawili hawa.
 
Kwa hiyo kwako wabunge wale ndio wanaifanya Chadema iwepo. Ushamba wenu ndio uliwafanya mtumie hela za umma kuanza mradi wa kununua wabunge ili Chadema kife! Akili ya kitoto sana, CDM ni watu, CDM iko kwenye mioyo ya watu. Ukitaka kujua hilo, maelfu ya watu wametia nia kugombe ubunge na nafasi za udiwani kupitia Chadema kwa kuomba sio kuombwa, kama vyama vyenu mlivyopandikiza vinavyofanya. na ninakuhakikishia uchaguzi wa 2020 bila mbeleko mnazotegemea za Tume na polisi, asubuhi tu game inamalizika! na wabunge kibao watashinda Chadema! Siasa za hovyo hovyo mnazofanya zinakokota watu "wanaoelewa polepole tu"!
Kwa hiyo wabunge na wanachama wenu Ni "Malaya" wananunulika? Mbona mnajiaibisha wenyewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo kwako wabunge wale ndio wanaifanya Chadema iwepo. Ushamba wenu ndio uliwafanya mtumie hela za umma kuanza mradi wa kununua wabunge ili Chadema kife! Akili ya kitoto sana, CDM ni watu, CDM iko kwenye mioyo ya watu. Ukitaka kujua hilo, maelfu ya watu wametia nia kugombe ubunge na nafasi za udiwani kupitia Chadema kwa kuomba sio kuombwa, kama vyama vyenu mlivyopandikiza vinavyofanya. na ninakuhakikishia uchaguzi wa 2020 bila mbeleko mnazotegemea za Tume na polisi, asubuhi tu game inamalizika! na wabunge kibao watashinda Chadema! Siasa za hovyo hovyo mnazofanya zinakokota watu "wanaoelewa polepole tu"!

Kwa mchango huu hapa tuko pamoja sana. Utetezi wa kweli kwa cdm kama taasisi naukubali maana ndio ukweli wenyewe. Lakini utetezi wa watu ndani ya cdm kwangu hauna nafasi maana najua ndio shida kwenye taasisi unapoanzia.
 
Kwa unaharakati wanafanana. Lakini baada ya uhuru Mandela alikaa miaka minne madarakani akatoka, hakuanza mbwembwe kuwa ndio aliyeleta uhuru. Nyerere alikaa miaka 24 baada ya uhuru, tena baada ya nchi kuwa fukara ndio akatoka. Hii ni tofauti kubwa ya wawili hawa.
Wote walitoka baada ya uanarakati na si kabla
 
upo sahihi mkuu lkn uchaguzi upo karibu mno unazani nani anafaa kugombea hususa huko chedema kwa mtazamo wako

Kwangu Lissu ndio sahihi ndani ya cdm, japo naye amejikita zaidi kwenye eneo la sheria hivyo huenda tukapata mabadiliko ya mifumo ya kiutawala zaidi. Tatizo la kuegemea eneo moja naliona hata sasa kwa Magufuli, maana yeye nguvu zake zote kaelekeza kwenye ujenzi wa miradi tu, demokrasia, ajira, kilimo nk havina nafasi kwenye utawala wake.
 
Upinzani 'pure' utakao iteteresha CCM unaweza kupatikana baada ya miaka 100 ijayo. CCM ni zaidi ya chama ni mfumo rasmi wa uendeshaji wa siasa za kistaarabu hapa nchini. Inapendwa na wana CCM wenywe na inapendwa sana na hao wanaojiita wapinzania. Hii ndiyo sababu kila siku hawaishi kurudi huku.
 
Ccm sio chama cha siasa bali ni kikundi cha dola kilichojivika koti la chama cha siasa. Na hakina siasa zozote za kistaarabu bali kinajenga siasa za hofu na shuruti ili kubaki madarakani.
 
Back
Top Bottom