Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Tuna kazi kubwa ya kupata maendeleo, ipo haja ya serikali kujifunza, ni kuazisha somo la ustarabu, ili new generation iwe yenye heshima
 
Wanaipe mimi hiyo tender ya kufanya marekebisho mil 50 nyingi!
 
Mi naiponda serkal kwa kutengeneza viti visivyo imara. Ova
 
Nafikiri kuzuia uwanja usitumike ni kuwaadhibu wachezaji ambao hawahusiki na kung'oa viti wala kuvunja mageti. Timu hizo zicheze bila watazamaji ambao ndiyo wanalate uharibifu.
Cha ajabu baadhi ya viongozi wanatoa sababu za kuutetea uharibifu uliofanywa. Inasikitisha sana. Adhabu iliyotolewa ni ya sh 1,0000/ badala ya sh 100/. Wachezaji hawana kosa. Wasiadhibiwe Kwa kosa la Mashabiki wasiowastaraabu kwenye Mpira wa miguu.
 
sababu ya tatu n viti vyenyewe kuwa dhaifu kwa kufungwa na nyaya, na kwa sababu viti havivunjiki hapi thamani halisi ni ya waya na fundi..............ila mm ni miongoni mwa waliolaani tukio hilo lote
 
Ndo uchumi wa dunia ya 3 kaka..... hata serikali kuna mengi tu hawajatenda... tunashare kilichopo....
 
Mi naiponda serkal kwa kutengeneza viti visivyo imara. Ova

Viti visivyo imara, unataka waweke viti ambavyo hata ukivuta havitoki, alafu bei ije kiti kimoja milioni, hiyo gharama nani atalipa? Watanzania wanatakiwa wawe wastaarabu, hivyo viti ni imara sana tu kwa matumizi ya kawaida, kuving'oa na kurushiana makusudi sio tatizo la serikali, ni tatizo la nyani.
 
Napongeza kwa hili, wajenge viwanja vyao halafu waharibu, sio hicho cha umma
 
Waamuzi nao wanachangia kwa kiasi kikubwa huu ujinga kutokea. Nao wapewe adhabu kali. Na hasa kufungiwa maisha.
Pamoja na refarii kuwa na poor performance haitoi kibali kwa washabiki kufanya fujo na kuharibu mali.
Kufungwa na hata mwamuzi kukosea ni sehemu ya mchezo
ila wale mashabiki wa simba ni watu wa ajabu sana ustaarabu zero, walipe tu
 
Unaandika upuuzi wewe
 
Hiyo 300ml. ni hela ya mboga kwa Mo,kesho Jumatatu ataandika cheki tena moja kwa moja kwa Vuvuzela habari iishie hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…