Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Tuna kazi kubwa ya kupata maendeleo, ipo haja ya serikali kujifunza, ni kuazisha somo la ustarabu, ili new generation iwe yenye heshima
 
Kuna watu mtaiponda serikali kwa hili lakini mimi naiunga mkono 100%. Watanzania imejaa wajinga wengi sana, viwanja vikiwa hamna wa kwanza kulaumu serikali, sasa vimetengenezwa mnaanza tabia za nyani mnavunja viti makusudi, alafu waafrika wakiitwa nyani wanakua wa kwanza kulalamika, hehehe! hizi tabia ni za myama gani sasa?
Mi naiponda serkal kwa kutengeneza viti visivyo imara. Ova
 
Nafikiri kuzuia uwanja usitumike ni kuwaadhibu wachezaji ambao hawahusiki na kung'oa viti wala kuvunja mageti. Timu hizo zicheze bila watazamaji ambao ndiyo wanalate uharibifu.
Cha ajabu baadhi ya viongozi wanatoa sababu za kuutetea uharibifu uliofanywa. Inasikitisha sana. Adhabu iliyotolewa ni ya sh 1,0000/ badala ya sh 100/. Wachezaji hawana kosa. Wasiadhibiwe Kwa kosa la Mashabiki wasiowastaraabu kwenye Mpira wa miguu.
 
sababu ya tatu n viti vyenyewe kuwa dhaifu kwa kufungwa na nyaya, na kwa sababu viti havivunjiki hapi thamani halisi ni ya waya na fundi..............ila mm ni miongoni mwa waliolaani tukio hilo lote
 
Kwani ni jukumu la serikali kuwatafutia Simba na Yanga mahali pa kuchezea.Klabu hizi zimekuwepo miaka mingi na zimelala kwa sababu serikali inafanya majukumu yao badala ya wao kujitegemea.Watacheza hata viwanja vya tandika huko ambako hakuna viti.Wanaudhi sana. Pesa yote hiyo ingeweza kufanya mambo ya maana kabisa.
Ndo uchumi wa dunia ya 3 kaka..... hata serikali kuna mengi tu hawajatenda... tunashare kilichopo....
 
Mi naiponda serkal kwa kutengeneza viti visivyo imara. Ova

Viti visivyo imara, unataka waweke viti ambavyo hata ukivuta havitoki, alafu bei ije kiti kimoja milioni, hiyo gharama nani atalipa? Watanzania wanatakiwa wawe wastaarabu, hivyo viti ni imara sana tu kwa matumizi ya kawaida, kuving'oa na kurushiana makusudi sio tatizo la serikali, ni tatizo la nyani.
 
unnamed%2B%252834%2529.jpg
 
Napongeza kwa hili, wajenge viwanja vyao halafu waharibu, sio hicho cha umma
 
Waamuzi nao wanachangia kwa kiasi kikubwa huu ujinga kutokea. Nao wapewe adhabu kali. Na hasa kufungiwa maisha.
Pamoja na refarii kuwa na poor performance haitoi kibali kwa washabiki kufanya fujo na kuharibu mali.
Kufungwa na hata mwamuzi kukosea ni sehemu ya mchezo
ila wale mashabiki wa simba ni watu wa ajabu sana ustaarabu zero, walipe tu
 
Wakati mwinyi yupo rais wa tanzania aliwahi kuhudhuria mechi ya simba na yanga

Ile mechi haikumalizika mwenyekiti wa yanga wakat huo bw tarimba aliamuru timu yake itoke nje kabla ya mpira kwisha

Mwinyi alichukulia ni hali ya mpira tu

Magu angefanyaje...
Unaandika upuuzi wewe
 
Hiyo 300ml. ni hela ya mboga kwa Mo,kesho Jumatatu ataandika cheki tena moja kwa moja kwa Vuvuzela habari iishie hapo.
 
Back
Top Bottom