Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Wewe JF Great thinker kabisa. Ahsante sana
 
Atakae kupinga aje na hoja kama hivi, sio blah blah. Binafsi nimepata darasa na uelewa kuhusiana na mradi huu.
 
Hivi alisemaje kuhusu tatizo la umeme na baada ya kifo chake si yakejirudia? Alikuwa mkweli ila mafisadi mnayaamini nyie wapuuzi, bisha
 

Bado wanapambana kutusaidia😂😂😂 zitto msanii sana
 
Mi naomba kwanza muweke mikata ya bwawa la Nyerere na SGR hapa kama mmewahi kuiona.Maana ni upuuzi kung'ang'ania kuona mkataba wa bandari tu ili hali mikataba mingine pia haijawahi oneshwa.
 
Unakaa kanyagwa wewe.
 
Bandari inaelezwa itajengwa na mataifa mawili yaani China na Mwarabu.Huku China ikidili na utalamu na mwarabu akitoa pesa.
Sasa kwa nini watu mnalazimisha tuamini mradi huu wamepewa wa China pekee?.
 
Mkuu Chige!Kuanzia sasa ntahakikisha nafuatilia kila bandiko lako.Wewe unamadini yenye thamani sana katika ubongo wangu.
 
@Sampuli06
 
Sampul06
 
Hili la ''mazungumzo'' (soma udalali) kuendelea wala huhitaji kuwa graduate kuelewa. Infact kila kitu kilishamalizika na mradi ulishapitishwa tangu siku ile Magufuli alipofariki. Mbona Samia alisema kabisa kuwa ni lazima hiyo bandari itajengwa? Ni suala la muda tu lakini mambo yataanza. Tunachofanya sisi ni kuweka tu kumbukumbu ili vizazi vijavyo visione kuwa ni watanzania wote walikuwa wapumbavu kiasi cha kukubali kuunga mkono mkataba wa kijinga namna hii. Tunajua Zitto ana role kubwa sana kwenye serikali ya sasa na amekuwa kama ni technical director na msemaji wa serikali asiye rasmi.
 
Hili la ''mazungumzo'' (soma udalali) kuendelea wala huhitaji kuwa graduate kuelewa. Infact kila kitu kilishamalizika na mradi ulishapitishwa tangu siku ile Magufuli alipofariki.
Sasa hayo mazungumzo yalikuwa yanaendeshwa na nani kama sio serikali ya huyo unayesema maamuzi yalipitishwa baada ya kufa?
Mbona Samia alisema kabisa kuwa ni lazima hiyo bandari itajengwa? Ni suala la muda tu lakini mambo yataanza.
Na kumbe Magufuli alisemaje kwenye hiyo video niliyokuwekea?
Tunachofanya sisi ni kuweka tu kumbukumbu ili vizazi vijavyo visione kuwa ni watanzania wote walikuwa wapumbavu kiasi cha kukubali kuunga mkono mkataba wa kijinga namna hii.
The problem, hujawahi kutoa hoja yoyote kuhusu ubaya wa huu mradi!! Kila siku, the same old story... mara kuna upigaji, mara vile!! Mara Kikwete, mara Zitto... jadili faida na hasara za mradi!

Hakuna asiyefahamu kwamba nchi hii kuna upigaji!! Hoja hapa ni faida na hasara za mradi, na namna gani mradi unaweza kufanywa kwa maslahi ya nchi.

Hicho ndicho unachotakiwa kujadili! Na ndicho mara zote nimekuwa nikijadili!!!

Au unataka kusema upigaji utakuwa kwenye Bandari ya Bagamoyo tu, na kwingine kote hakuna upigaji?! Au ndo yale yale ya kutuaminisha mwizi mkubwa nchi hii ni Acaccia na makinikia yake, wakati kampuni zote za madini ni wale wale tu??!
Tunajua Zitto ana role kubwa sana kwenye serikali ya sasa na amekuwa kama ni technical director na msemaji wa serikali asiye rasmi.
Hiyo obsession yako na akina Zitto, nakuachia mwenyewe!!
 
Nishasema sana hapa, na nitarudia...

Hizo habari za miaka 99 tusikusanye chochote ni UONGO unaonezwa na Wapingaji wa mradi kwa sababu zao binafsi!! Hakuna kitu kama hicho sehemu yoyote duniani!!

Huo ni uongo kama ule uliokuwa unaenezwa kwamba China imepora Bandari ya Sri Lanka ili kulipia deni lao!!!

Ukweli ni kwamba, Mchina; kama alivyo mwekezaji yeyote yule; LAZIMA ataomba msamaha wa kodi!!

Lakini lazima mfahamu kuna aina mbalimbali za kodi, na nyingine zinasameheka kwa mujibu wa sheria zetu wenyewe!!!

Kwa kawaida, ukiondoa ile grace period ambayo sio jambo geni, Mchina huwa anaomba aondolewa INCOME TAX!

What's income tax!

Kwa mfano wewe ukipitisha mzigo pale Bandari ya Dar es salaam, na ukachelewa kuuchukua, Mamlaka ya Bandari (sio TRA) watakuchaji tozo ya kukuhifadhia mzigo wako!

Hiyo Tozo ndio moja ya Income za Mamlaka ya Bandari!! Na kwa sheria zetu, TPA watalazimika kulipa Income Tax kwa TRA kutokana na mapato wanayoingiza kupitia tozo mbalimbali!!

Sasa basi, tukichukua mfano huo huo tukaupeleka Bandari ya Bagamoyo...

Kama umepitisha shehena pale, assuming ni bandari ya kawaida, basi utalipa Import Tax, Stamp Duty, na VAT...

Hizo kodi always ni MALI YA SERIKALI!

NI mali ya serikali kwa sababu anayelipa sie "Mmiliki/Mwendeshaji wa Bandari" bali Mtumiaji wa Bandari!!!

Lakini kama nilivyotoa mfano wa Bandari ya Dar es salaam, wewe utalazimika kutumia huduma za Mchina hapo bandarini.

Kwa mfano, utalazimika kumlipa gharama za kupakia na kupakua mzigo! Utalazimika kumlipa gharama za kuhifadhi mizigo kwa muda utakaowekwa!!

Hizo pesa unazolipa ni za Mchina na sio TRA!! Lakini kwavile unapokuwa umemlipa Mchina inamaanisha anakuwa ameingiza INCOME, hapo ndipo TRA atapiga hodi kuitaka Income Tax!!

Hii Income Tax hailipwi na Mtumiaji wa Bandari bali ni Mwendeshaji/Mmiliki wa Bandari!!

Sasa kwavile Mwendeshaji ni Mchina, kwa kawaida, Mchina huwa anaomba kufutiwa hiyo Income Tax! Kama ulimlipa TZS 100M ili kukuhifadhia mizigo yako, Mchina ataomba hiyo 100M isikatwe kodi (Income Tax)!

Lakini kwamba eti anataka miaka 99 tusikusanye chochote, ni HABARI ZA UONGO!!

Na hata kwenye hiyo 99, watu wanachanganya madesa....

Kumbuka sheria zetu za umiliki wa ardhi ni miaka 33 (renewable), miaka 66 (renewable), na miaka 99!!

Kilichopo ni kwamba, Mchina anataka AMILIKISHWE ARDHI kwa miaka 99, wakati anatarajiwa ku-operate bandari at the maximum of 40 years!!

Sasa hapo ndipo inapokuja hoja kwamba: Kama atapewa mkataba wa miaka 30 au 40 ya kuendesha bandari, kwanini atake kumiliki ardhi kwa miaka 99!!

Kwanini asimilikishwe 33 years (renewable), na kama itaonekana mkataba unaendelea, akamilikishwa kwa miaka mingine 33!!

Kwangu mimi sioni tatizo hapo... ni jambo linalozungumzika!

Hata hilo la msamaha wa baadhi ya kodi, nalo linazungumzika!!!
 
Niliwashangaa sana Chadema kutetea huu mradi, isijekuwa wabunge wa hiki chama walirubuniwa. Nina mashaka sana na Zito kwa sasa. Maana aliutetea sana huu mradi.
Hahahahaa! utaiweka wapi sura yako chief?
 
Ikiwa kila kitu kilikua sawa, na sasa hivi mnahitaji bandari ya bagamoyo kwa nini msiendelee pale mlipoishia? Mazungumzo ya nini tena ikiwa hakukua na shida yoyote?
 
Ikiwa kila kitu kilikua sawa, na sasa hivi mnahitaji bandari ya bagamoyo kwa nini msiendelee pale mlipoishia? Mazungumzo ya nini tena ikiwa hakukua na shida yoyote?
Hivi una habari hadi JK anaondoka madarakani ambacho kilikuwa kimesainiwa ni Initial Framework Agreement na MoU?!

Na hivi una habari kwamba Framework Agreement na MoU sio MKATABA?!

Na hivi una habari, kutokana na framework iliyowekwa, negotiation ilikuwa ifanyike na rais ambae angemfuatia JK?!

Na hivi una habari ni baada ya hayo majadiliano ndipo ungesainiwa mkataba wa ujenzi?!

OH... let me guess!!!

Uliambiwa Awamu ya IV walisaini Mkataba wa Kifisadi, na alipoingia Magu akaupiga chini ule mkataba wa kinyonyaji?!

Hebu jiulize: Hivi unaamini kabisa kwamba mkataba unaweza kupigwa chini kirahisi rahisi namna hiyo?!

Yaani mmeshakubaliana, mmesaini mkataba, halafu bado mnaendelea na mazungumzo?!

Hivi ikiwa issue ya makinikia ya Acaccia tu, nchi iliwaka moto... kila hatua tunaoneshwa ma-Live TV Coverage; kungekuwa na mkataba uliovunjwa mngekosa kuona hizo mbwembwe?!
 
Bagamoyo ikijengwa bandari ya dar ndo itakuwa By By iwe kwa lazima au kwa hilari
Ninaamini eneo hili la dunia litakuwa na mizigo ya kutosha kabisa kukidhi mahitaji ya bandari zote mbili, na hata zaidi. Usione haya ya leo ukadhani ndiyo yatakuwa ya kesho. Omba tu Mungu akupe uhai ushuhudie itakavyokuwa miaka 10 hadi 20 ijayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…