Point niliyoiona mimi, kwa kuzingatia mada zangu ni pale aliposema kulipa mabilion ya pesa kwamba Wachina wanataka kujenga viwanda Kigamboni, lakini hapo hapo akazungumzia suala la kujenga Bandari Kigamboni...
Now tell me: NI Wachina gani walitaka kujenga Bandari Kigamboni?!
Au tuseme alikusudia kusema Bagamoyo, na hivyo viwanda of course, ilikuwa ni huko huko Bagamoyo kwenye Bagamoyo Special Economic Zone!!
Kwa mfuatiliaji anafahamu Bagamoyo Special Econmic Zone iliyokuwa inatarajiwa kujengwa viwanda, ni mradi uliokuwa uende pamoja na Ujenzi wa Bandari!! Sasa alitarajia aone viwanda gani wakati Mradi wa Bandari ulipigwa stop?!
On top of that, JPM anasema Wajenzi walitoa masharti ya kipumbavu kwamba:-
Huyo ndo JPM mmoja, but another version of JPM is here:-
Hivi yule aliyesema ni "ni mambo ya kipumbavu kabisa yamefanyika ndo huyo huyo hapo juu, au ni watu wawili tofauti?
Lakini kwa upande mwingine nao, Deusdedit Kakoko, aliyekuwa Mkurugenzi wa Bandari nae anasema kuanzia dakika ya 4 kwamba:-
Sasa nijuze wewe! Kumbe Bandari ya Bagamoyo ilikuwa iwe export port na sio competitor wa bandari zilizopo, na ndo maana hapo hapo palitakiwa kujengwa viwanda!!
Sasa how come tena unatoa masharti ya kutojenga bandari ingine ambazo zisingekuwa competitor?!
Na msikilize hata huyo Kakoko mwenyewe alivyo mwongo! Eti kule Sri Lanka hadi ikatokea vita! Na wengi wamekuwa wakihusisha Bandari ya Hambantonta (ya Sri Lanka) na umafia wa Wachina!!
Sasa ni lini Sri Lanka ilitokea vita inayohusishwa na hiyo bandari?!
Kila anayefuatilia mambo anafahamu vita ambavyo vilidumu Sri Lanka ni vile kati ya Serikali na Tamil Tiger!! Kama nawe ni mfuatiliaji... hivyo vita vilipiganwa lini hadi lini na Bandari ya Hambantonta ilijengwa lini?!
Na miongoni mwa propaganda ambazo zilisambazwa sana Tanzania na wale wale mliokuwa mnawashingilia, ni suala la Wachina kuichukua hiyo Bandari ya Sri Lanka ili kujilipa deni lao! Watu tukasema hapa hizo ni habari za uongo zilizoanzishwa na Trump Administration ili ku-discredit Belt & Road Initiative!!
Mkasema tumenunuliwa!
Hata Wamarekani nao waliingizwa chaka na propaganda za Trump Administration hadi pale Wasomi wa Harvard na John Hopkins University walivyoanza kutilia wasiwasi habari hizo! Ili kupata ukweli wa kile wanachoambiwa na serikali yao, wakaamua kupeleka watu field kufanya research ili kufahamu ukweli!
Abstract ya research husika
inasema:-
View attachment 2016615
Hivi mlikuwa mnaambiwaje vile kuhusu Wachina na Bandari ya Sri Lanka?!