Ameongea kwa uchungu mwingi hadi nimemhurumia mzee wa watu, sio kwa wawekezaji, sio kwa Watanzania, kila mtu mpigaji. Makajanja wa Dar walikwenda Bagamoyo wakatia kapuni mabilioni ya hela na kuwaacha wazawa na wakazi wa Bagamoyo mikono mitupu, nao wawekezaji wanaonekana kuja na masharti ya kiajabu ajabu.
Lakini tatizo hamsemi kimoja mueleweke nini sababu haswa za kusitishaa huo mradi, maana hapa rais amesema mengi ambayo hayajawahi kutajwa kati ya yote ambayo huwa mnayasema, halafu kama kweli hajaongeza chumvi, then ina maana rais Kikwete alikua anairubuni nchi yenu, kama kweli Kikwete alikubaliana na yote hayo yaliyotajwa humo, aisei nitamshangaa sana huyo rais wenu wa zamani, alikua ameipokeza nchi kwa watu mchana peupe.
Japo pia ni vigumu kuamini ukweli bila kuskliza upande wa pili, maana kila siku tunaskia ya nyie, hatujaskia naye muwekezaji kama kweli alikua na masharti kama hayo ya kuikoloni na kuifilisi nchi ya Tanzania.