KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
'ruhi' watu wamekazana sana kutaka sote tukubali uigizaji huu kuwa ndio hali halisi.Hivi hiyo mkataba ilikua inatoka China na moja kwa moja adi ikulu? yaani haipiti wizarani? make naona sign inatiwa chini ya wizara husika na mawaziri husika wakiwepo.
Hapa tunamlaumu Mawaziri wa sheria; biashara na wengine kuhusu ishu ya korosho..ila cha kushangaza unaweza kuta huo mkataba inayomkono wa waziri wa ujenzi wa wakati huo JPM.
Na kama rais alisign bila wizara kushirikishwa natambua kuna loophole iliyompa mh Rais mamlaka hayo na kilimkera sana waziri wakati huo akiwa Jpm lakini bado yupo hapo hataki kubadilisha hizo sheria wala kikatiba zikabadilika anasubiri mwenye nia mbaya aje aingie azitumie; mimi nasema na yeye hana nia njema kama walewale.
Kuna ishu ya Rais kugawa vipande vya rasilimali apendavyo kama utalii kule Loliondo kwa Wadubei; cha kushangaza awamu hii wameingia na hawataki kuzibadilisha ata kama katiba inasema wazilete mezani wasibaki kutaka sifaza muda mfupi tu.
Hawaamini kuwa wapo wanaoona na kutambua uigizaji na kuuweka pembeni na kuwaambia ukweli ulivyo.
Ni wajibu wa wanaouona ukweli na kuusema bila kuchoka.
Hawa wanaotafuta kuwalaghai watu wakidhani wote ni wajinga, mwishowe ulaghai wao utaonekana wazi. Jitihada zote za kuzima vyombo vya habari visifanye kazi bila kuingiliwa ni sehemu ya kupumbaza watu na ni njia hizo hizo walizodhani ujinga wa waTanzania utazidi kuenea ili waendelee kulaghai watakavyo.
Huu ni uongozi wa ajabu sana.