KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Kwa hiyo Njonjo alikuwa anakubali uhalali wa "Man eat man society"? Sote tunajua hakuwezekani kuwepo "Man eat nothing society."Pale tunaposhangilia Kutokuwa na bandari badala ya kuwa na Bandari!
Serikali ya awamu ya Tano inanikumbusha msemo maarufu wa Waziri Njonjo wa Kenya aliyeipiga vijembe serikali ya Nyerere baada ya Nyerere kutoa kauli ya kuiikejeli Kenya kwa kusema "Kenya is a man eat man society", Njonjo akasema “Tanzania is a man eat nothing society"!
Kwenye makinikia mliletewa porojo kama hizi kumbe ikaja kujulikana ni uongo mwingi na ukweli kidogoShamba la bibi, kuna mambo lazima tukubali Rais wetu anajitahidi sana kuyaweka vizuri na tumpe heko. Katika kulinda uridhi wetu kwa kweli nampa heko, anajitahidi sana.
Mikataba ya hovyo kama hii ni wizi wa mchana kabisa. Hamna maslahi kwetu kama watanzania. Hii mikataba kama ya mangungo ifutiliwe mbali.
Natamani aingilie mikataba ya gasi pia, kule nako sijui kama tupo salama.
Kama watakubaliana na mkataba ambao ni win win wajenge ila mkataba ambao hatufaidi chochote, hatuhoji chochote yaani tumeuza uridhi wetu kwa miaka 99 bila chochote watu wanachuma tu, tena bado turejeshe gharama na hatuna uwezo wa kufanya chochote mbadala, hapana kwa kweli..khaaa
Heko Rais, tuliendie urithi wetu tutakukumbuka kwa hilo.
Umeona unafiki wa viongozi wa ccm .Ni Tanzania tu ambapo kiongozi aliyekuwa kimya mpaka mkataba wa kinyonyaji ukapita anakuja kusema huo mkataba ulikuwa mbovu! Wakati huo huo hata yeye huo Mkataba hataki kuonyesha nini kiko ndani ya huo mkataba alipokubali upite, kisha akaukataa. Kichekesho ni pale rais huyo huyo anapogomea katiba mpya ili mambo yaendeshwe kwa uwazi zaidi na watu wanashangilia na kusema ni kiongozi sahihi!
Limbukeni kwa kudanganya ni kiboko aisee utafikiri hakuwa anagonga meza kuupitisha mkataba kwa mbwembwe nyingi .Ila hujiulizi nani alikuwa waziri wako wa ujenzi wakati president kikwete anaweka jiwe hili la msingi,why hawaku rise hizi issue?,uoga wao na njaa ya matumbo yao wakawa kimya kulinda vibarua vyao na sasa wanataka kujifanya ni mashujaa,politics za kinafiki zitatuumiza sana nchi hii ,na tukitukanwa kwa kuitwa pithole country tunachukia wakati ndio ukweli wenyewe.
View attachment 1123438
RAIS John Magufuli amesema sababu kubwa ya kusitishwa kwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni masharti magumu yaliyomo katika mkataba wa utekelezaji wa kazi hiyo.
Jiwe la msingi la ujenzi wa bandari hiyo liliwekwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2015 na ulitarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10. Bandari hiyo endapo ingejengwa ingekuwa kubwa zaidi Afrika Mashariki ikiwa na ukubwa wa ekari 3,000 na viwanda 190 vingejengwa.
Akizungumza jana kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliowashirikisha wafanyabishara kutoka wilaya 139 nchini, Rais Magufuli aliweka wazi sababu za kusitishwa kwa ujenzi wa bandari hiyo. Rais Magufuli alisema “kwenye mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo kulikuwa na vipengele vya ovyo”. Rais Magufuli alisema mojawapo ya masharti ni kutojengwa wala kuendelezwa kwa bandari yoyote kuanzia eneo la Tanga hadi Mtwara.
"Yaani kwenye eneo lote kuanzia Tanga hadi Mtwara kusijengwe bandari yoyote. Bandari ya Kilwa tusiiendeleze, Bandari ya Mtwara ambayo itawezesha mikoa ya kusini kupokea mafuta badala yake Dar es Salaam kisha yarudi huko, hatutakiwi kuiendeleza, Barabara kutoka Mtwara hadi Bamba Bay ambayo itatuwezesha kusafirisha mizigo hadi Msumbiji tusiijenge," alisema Rais Magufuli
Pia alisema wawekezaji hao wangeweza kumiliki ardhi kwa hati ya miaka 99 pamoja na kutoruhusiwa kuuliza nani anamiliki eneo hilo. Rais Magufuli alisema sharti lingine ni gharama zitakazotumiwa na mwekezaji huyo katika ujenzi wa bandari hiyo kutakiwa kurejeshwa.
Niliwashangaa sana Chadema kutetea huu mradi, isijekuwa wabunge wa hiki chama walirubuniwa. Nina mashaka sana na Zito kwa sasa. Maana aliutetea sana huu mradi.
Mchina sio mtu wa mchezo mchezo,yaani ukizubaa tu sekunde anakumaliza!aya banah
Mchina sio mtu wa mchezo mchezo,yaani ukizubaa tu sekunde anakumaliza!
Kwanini hukufanya comparison masharti ya hiyo bandari???? Tatizo hamtaki kumuamini kiongozi na kumuacha afanye kazi, mmempa jukumu na kuongoza nchi basi muamininiMikatabba ya Kiwanja cha ndege cha Chato, ya Stiegler's Gorge, ya ununuzi wa ndege pia viwekwe hadharani, ili watanzania wafanye comparisons!!!
Hawa ni wadogo, hakuna wengine maarufu zaidi hata kimadaraka?Msukuma na kibajaji
Kwa hiyo Njonjo alikuwa anakubali uhalali wa "Man eat man society"? Sote tunajua hakuwezekani kuwepo "Man eat nothing society."
Hivi hiyo mkataba ilikua inatoka China na moja kwa moja adi ikulu? yaani haipiti wizarani? make naona sign inatiwa chini ya wizara husika na mawaziri husika wakiwepo.Hiyi ilikuwa kazi kuu ya serikali ya awamu ya nne na watendaji wake wakuu!! Halafu unaona watu wanakenua!! Hata mababu zetu ambao hawakuwa wamepata elimu ya hata kindergarten ya Kimangaribi(Western education) hawakuwa na akili finyo kama za wasomi wa vyuo vikuu wenye Masters na PhDs!!!! Kudos Rais Dr Magufuli.
Ameongea kwa uchungu mwingi hadi nimemhurumia mzee wa watu, sio kwa wawekezaji, sio kwa Watanzania, kila mtu mpigaji. Makajanja wa Dar walikwenda Bagamoyo wakatia kapuni mabilioni ya hela na kuwaacha wazawa na wakazi wa Bagamoyo mikono mitupu, nao wawekezaji wanaonekana kuja na masharti ya kiajabu ajabu.
Lakini tatizo hamsemi kimoja mueleweke nini sababu haswa za kusitishaa huo mradi, maana hapa rais amesema mengi ambayo hayajawahi kutajwa kati ya yote ambayo huwa mnayasema, halafu kama kweli hajaongeza chumvi, then ina maana rais Kikwete alikua anairubuni nchi yenu, kama kweli Kikwete alikubaliana na yote hayo yaliyotajwa humo, aisei nitamshangaa sana huyo rais wenu wa zamani, alikua ameipokeza nchi kwa watu mchana peupe.
Japo pia ni vigumu kuamini ukweli bila kuskliza upande wa pili, maana kila siku tunaskia ya nyie, hatujaskia naye muwekezaji kama kweli alikua na masharti kama hayo ya kuikoloni na kuifilisi nchi ya Tanzania.
Huna haja ya kubisha mkuu for the sake ya kubisha. MK254 kasema kweli sana tuRais Akisema hatuhitaji kusikia upande wa pili,
Besides, Kikwete was not Different from Uhuru Kenyatta and William Ruto.