Rais Magufuli ataka Polisi kumwachia mmiliki wa shule ya Waislamu Byamungu iliyoungua Kyerwa wakati wakiendelea na upelelezi

Rais Magufuli ataka Polisi kumwachia mmiliki wa shule ya Waislamu Byamungu iliyoungua Kyerwa wakati wakiendelea na upelelezi

Waachie masheikh zaidi ya 70 huko Arusha ambao wako ndani bila kosa lenye mashiko, eti kosa lao ni kuipinga BAKWATA
Comrade unaweza kuileta hapa hati ya mashitaka ya hao masheikh zaidi ya 70 wote tukasoma kuwa wameshitakiwa kwa kuipinga BAKWATA??!
 
Mahabusu watu huwekwa si tu kwa kuwa wana tuhuma, wengine ni kwa ajili ya usalama wao. Magufuli hawatumii vema washauri wake, mara nyingi hutoa maagizo bila kupima athari kwa upande wa pili. Matokeo yake ni kuwaweka njia panda watendaji wake wasiwe na uhakika na nini mkuu atasema wakitekeleza hili au lile kwa mujibu wa sheria na kanuni.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Unatumia kigezo gani kusema hazina mashiko? Tuwekee hapa hati ya mashitaka ili tujiridhishe comrade.

Kamuulize DPP, sitembei na mafaili ya kesi ila najua kesi hii na nyingine ni za kubambikiza tu kwa makosa yasiyokuwepo ili kulinda maslahi binafsi ya kisiasa ya watawala, na hili la Masheikh ni mfano mmojawapo
 
Kamuulize DPP, sitembei na mafailinya kesi ila najua nyingine ni za kubambikiza tu kwa makosa yasiyokuwepo, na hili la Masheikh ni mfano mmojawapo
Shutuma umeandika wewe halafu unataka nikamuulize DPP kama ni kweli au sio kweli??! Comrade Jf sio kichaka cha kuandika uongo na uzushi.
 
Kamuulize DPP, sitembei na mafaili ya kesi ila najua kesi hii na nyingine ni za kubambikiza tu kwa makosa yasiyokuwepo ili kulinda maslahi binafsi ya kisiasa ya watawala, na hili la Masheikh ni mfano mmojawapo
Bakwata ipo kisheria wao wanaanzaje kuikataa?!
 
Hao makosa yao yako dhahiri!
Basi wahukumiwe kwa mujibu wa sheria badala ya ukatili unaofanyika wa kuwasotesha mahabusu - wengine sasa miaka zaidi ya mitano kwa kisingizio cha upelelezi kutokamilika. Huu ni uvunjifu wa haki za kibinadamu na kikatiba.
Nyie mnaounga mkono ukatili huu mgejifunza kutoka kwa yaliyompata mzee Lowassa. Wakati wa mchakato wa Katiba Mpya hususani hatua ya kujadili rasimu ya Warioba, mzee Lowassa na CCM wenzake waliipinga Rasimu (ambayo ilikuwa inasisitiza utawala bora na wa haki, na kupunguza uwezo wa Rais ku-abuse madaraka ya urais) na hivyo tumeendelea na hii iliyochoka na kumfanya rais kuwa alfa na omega. Magufuli ameitendea haki kweli kweli ikiwa ni pamoja na kuwasweka mkwe wa Lowassa na wenzake mahabusu kwa takribani miaka minne kwa kisingizio cha kutokamilika upelelezi, na hatimaye kuwafutia mashtaka alipojisikia kuwafutia kwa sababu hapakuwepo na ushahidi wo wote kuwa walivunja sheria. Lowassa angeunga mkono Rasimu ya Warioba, haya yasingemkuta kama amb avho yasingewakuta watu wanaoonewa tu kutokana na binadamu mwenzako anavyoamka na kujisikia.
 
BAKWATA Inajaribu kuingilia mambo ya Taasisi nyingine za waislamu ambazo nazo zipo kisheria, wakipinga hilo, BAKWATA inaenda kwa "handlers" wake yaani Serikaki ya CCM kuwashughulikia kinyume cha haki
Bakwata ndio taasisi kuu ya waislamu wote!
 
Back
Top Bottom