Rais Magufuli atembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba maalumu ya Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete

Rais Magufuli atembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba maalumu ya Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete

Sheria za kibaguzi.

Watu ambao hawana uwezo wa kuwa na nyumba, wafanyakazi wa chini serikalini hawasaidiwi kupata makazi.

Watu wenye uwezo wa kuwa na nyumba hawa marais, tena wana nyumba zao tayari, ndio wanajengewa nyumba.

Maajabu ya dunia hayo.
 
Changa la macho hilo, jamaa maji ya shingo, huku Lissu kule Alshabab, ameenda kuomba ushauri baada ya Ben kurest in peace.

Si alikuwa anajifanya hamnazo mwaka huu ataisoma no na bado mpaka alale kifudifudi Kama alivyosema Lissu Dodoma jana.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
JK anastahili heshima kwa kazi nzuri aliyoifanyia Taifa letu.

Tuwaenzi wazee wetu.

Umeonesha mfano wa Kuigwa Dr. Magufuli.
 
mkuu,muache mzee JK ale maisha tuwe na shukrani wakati mwingine,kwani akijengewa hilo jumba itapunguza nini kwenye taifa ? mbona Nyerere alijengewa hamku mind

Nyerere aliingia mikataba yoyote ya wizi hapa nchini? Pamoja na mapungufu yake, lakini Nyerere hakutumia madaraka yake kujilimbikizia mali, na hata hiyo nyumba waliyomjengea hakuwa anaitaka. JK ana miaka 70, anajengewa jumba kubwa hivyo ili iweje wakati ana nyumba tayari na familia yake wote wana maisha ya uhakika?
 
Hapana huwezi kuwa na sheria mbili katika nchi moja, hawa wakistaafu walipwe 80% ya mshahara wa wakati huo kwa maana nyingine siku akija rais kichaa kuongeza mshahara 300% basi nao 80% ila kwa wastaafu wengine pamoja na kufanya kazi zaidi ya miaka 30 mazingira magumu lakini wanalipwa pesa ileile hata kama maisha yamebadilika. kama kuna mtu alistaafu 1990 sasa sijui mishahara ilikuwa kiasi gani usishangae kukuta mtu analipwa alfu 20. Hawa viongozi wamejenga nyumba nyingi tu walizipata kivipi sijui ila kwanini kuwajengea tena? Si walilipwa stahiki zao. kwa hili hapana basi ingekuwa hata nyumba ya kiasi nyumba utasema Mall. Wewe katizame wanajeshi wakistaafu utatamani kulia.
Dawa ya haya yote ni uwepo wa katiba mpya.
 
Hizo fedha zingejenga nyumba zaidi ya 25 za walimu na manesi wanaohangaika na vyumba 2 vya kupanga ambavyo havitoshi size ya familia yao. MTU amekuwa waziri 15 years na Rais 10yrs na hapo alipo anamiliki kijiji pale Msoga na magorofa kibao Dar, mke ni mbunge, mtoto mbunge bado anajengewa kasri, eti Mimi Rais wa wanyonge, kweli aliyenacho ataongezewa.
 
Ya Mwinyi imejengwa masaki kakabiziwa leo 18-10-2020.
Serikali ilikiwa wapi kujenga nyumba hiyo mapema.wamesubiri mzew wa watu amebakiza miaka michacjhe ndiyo wanamjengea.ataaishi muda mfupi halafu itakuwa ya Ridhiwani na wadogo zake

ya Mwinyi inajengwa wapi,?
 
Sasa hiyo ni nyumba au ni lijihoteli?!

Kama ni nyumba, sasa ni nyumba ya rais mstaafu au ni lijijumba la ukoo wa rais mstaafu?!

Moja ya mambo ambayo sijawahi kuyajutia maishani mwangu ni kutotetereka kuhusu tabia za kifisadi za Mkapa hata kama kuna watu wanataka kutuaminisha kwamba the guy was clean kama ambavyo mwenyewe alipenda kujiita Mr. Clean!!!
 
BADO WANAONGEZEWA NA NYUMBA NYINGINE TENA? WATANZANIA TUNAPASWA KUKATAA HUU UNYONYAJI. SI SAWA HATA KIDOGO.
 
Ni kweli, tuwaenzi na wazee wetu wastaafu wa kada za udaktari, polisi na ualimu kwa kuwajengea nyumba na wao pia.
JK anastahili heshima kwa kazi nzuri aliyoifanyia Taifa letu.

Tuwaenzi wazee wetu.

Umeonesha mfano wa Kuigwa Dr. Magufuli.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli leo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba maalumu ya Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Ujenzi wa Nyumba hiyo inajengwa na Serikali kwa mujibu wa Sheria namba 3 ya Mwaka 1999 inayoainisha ujenzi wa Nyumba maalumu kwa ajili ya makazi ya waheshimiwa Marais mara wanapostaafu.

View attachment 1604017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba ambayo Dkt. Kikwete anajengewa na Serikali eneo la Kawe Beach jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 18, 2020.

View attachment 1604019
View attachment 1604020
Kwenda kipindi hiki cha kampeni ni kumsimanga JK
 
Si alikuwa anamponda. Leo maji ya shingo ndio anamfanya wa karibu
 
Back
Top Bottom