Rais Magufuli atembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba maalumu ya Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete

Sheria za kibaguzi.

Watu ambao hawana uwezo wa kuwa na nyumba, wafanyakazi wa chini serikalini hawasaidiwi kupata makazi.

Watu wenye uwezo wa kuwa na nyumba hawa marais, tena wana nyumba zao tayari, ndio wanajengewa nyumba.

Maajabu ya dunia hayo.
 
Changa la macho hilo, jamaa maji ya shingo, huku Lissu kule Alshabab, ameenda kuomba ushauri baada ya Ben kurest in peace.

Si alikuwa anajifanya hamnazo mwaka huu ataisoma no na bado mpaka alale kifudifudi Kama alivyosema Lissu Dodoma jana.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
JK anastahili heshima kwa kazi nzuri aliyoifanyia Taifa letu.

Tuwaenzi wazee wetu.

Umeonesha mfano wa Kuigwa Dr. Magufuli.
 
mkuu,muache mzee JK ale maisha tuwe na shukrani wakati mwingine,kwani akijengewa hilo jumba itapunguza nini kwenye taifa ? mbona Nyerere alijengewa hamku mind

Nyerere aliingia mikataba yoyote ya wizi hapa nchini? Pamoja na mapungufu yake, lakini Nyerere hakutumia madaraka yake kujilimbikizia mali, na hata hiyo nyumba waliyomjengea hakuwa anaitaka. JK ana miaka 70, anajengewa jumba kubwa hivyo ili iweje wakati ana nyumba tayari na familia yake wote wana maisha ya uhakika?
 
Dawa ya haya yote ni uwepo wa katiba mpya.
 
Hizo fedha zingejenga nyumba zaidi ya 25 za walimu na manesi wanaohangaika na vyumba 2 vya kupanga ambavyo havitoshi size ya familia yao. MTU amekuwa waziri 15 years na Rais 10yrs na hapo alipo anamiliki kijiji pale Msoga na magorofa kibao Dar, mke ni mbunge, mtoto mbunge bado anajengewa kasri, eti Mimi Rais wa wanyonge, kweli aliyenacho ataongezewa.
 
Ya Mwinyi imejengwa masaki kakabiziwa leo 18-10-2020.
Serikali ilikiwa wapi kujenga nyumba hiyo mapema.wamesubiri mzew wa watu amebakiza miaka michacjhe ndiyo wanamjengea.ataaishi muda mfupi halafu itakuwa ya Ridhiwani na wadogo zake

ya Mwinyi inajengwa wapi,?
 
Sasa hiyo ni nyumba au ni lijihoteli?!

Kama ni nyumba, sasa ni nyumba ya rais mstaafu au ni lijijumba la ukoo wa rais mstaafu?!

Moja ya mambo ambayo sijawahi kuyajutia maishani mwangu ni kutotetereka kuhusu tabia za kifisadi za Mkapa hata kama kuna watu wanataka kutuaminisha kwamba the guy was clean kama ambavyo mwenyewe alipenda kujiita Mr. Clean!!!
 
BADO WANAONGEZEWA NA NYUMBA NYINGINE TENA? WATANZANIA TUNAPASWA KUKATAA HUU UNYONYAJI. SI SAWA HATA KIDOGO.
 
Ni kweli, tuwaenzi na wazee wetu wastaafu wa kada za udaktari, polisi na ualimu kwa kuwajengea nyumba na wao pia.
JK anastahili heshima kwa kazi nzuri aliyoifanyia Taifa letu.

Tuwaenzi wazee wetu.

Umeonesha mfano wa Kuigwa Dr. Magufuli.
 
Kwenda kipindi hiki cha kampeni ni kumsimanga JK
 
Si alikuwa anamponda. Leo maji ya shingo ndio anamfanya wa karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…