Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Great thinkers wameisha kabisa JamiiForums. Mmeambiwa kabisa kwamba atapangiwa kazi nyingine eti watu wanapoongeza ametumbuliwa. Maana yake alifanya kazi yake ipasavyo, ila tu mambo yamehalibika hivyo watampa kazi nyingine. Maslahi yake pale pale. Sisi mazuzu tunadhani ametumbuliwa
 
Sasa Jenista anabakije? Huyu kweli ni Rais wa wanyonge?
 
Sheria haijatenguliwa mkuu kilichotenguliwa ni kanuni na kanuni hiyo ni kipengele kimoja cha kikokoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mh John Pombe Joseph Magufuli kwa kutuondolea huyu mama "Dr" Irene, ambaye huko nyuma nilitilia wasi wasi sana "Phd" yake.
Huyu mama alishindwa kabisa kelezea 20% wanayochangia wafanyakazi kwenye mfuko wa pendheni, na 25% ambayo mfanyakazi analipwa kutokana na jumla ya makato yote.

Sisikitiki na nilimdharau sana kwa kujaribu kueleza vitu ambavyo ni dhahiri alikuwa havijui kabisa mantiki yake.

Swali langu ninkwamba alifikaje hapo?
Kulikuwepo na due diligence, vetting ya elimu yake na uwezo?
 
Mimi siko kwenye hizo complication zenu za kichadema! kudandia kila kinachopita mbele yenu. Ona wenzako mpaka sasa hawaoni kuwa wanatetea suala la fastjet na wanasema bila haya waruhusiwe kurusha ndege na suala la usalama lifumbiwe macho!
 
Magufuli huwa hapendi ujinga na watu kufanya kazi kwa mazoea. kauli ya hapa kazi tu inaendelea kuwa wazi na lazima ieleweke Magufuli anaposema hapa kazi anamaanisha nini anasema.
Wakati yeye ndo mjinga namba moja.No raid gan aliisain hiyo sheria? Mwenyekiti wa baraza la mawaziri ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

wala tusipoteze muda kuuliza na kubuni sababu za kutengua uteuzi. uzuri Rais wetu anatabirika sana. kwa kuwa hili jambo la kikokotoo limeshafanywa kete ya kisiasa na kujitafutia umaarufu wa kupendwa kama mtetezi wa wafanyakazi, mpeni muda tu.. siku sio nyingi ataropoka kwenye matukio yake sababu za kutengua...hata kama atatengeneza sababu na kuacha ukweli pembeni
 
Kwanini asingejiondoa kwenye hiyo nafasi ya ukurugenzi, kuendelea kuwepo hapo ina mana alikubaliana na mambo aliyoletewa kuyasimamia kuhusu mafao ya watumishi.
 
Mmeambiwa kabisa kwamba atapangiwa kazi nyingine..
Hiyo huwa ni statement tu kuua soo. Ninawafahamu vigogo watatu “walioenguliwa” kwa gear ya kupangiwa kazi nyingine tangu mwaka jana. Wapo tu wizarani wanasugua benchi huku wakisoma magazeti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…