Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Mapema leo Rais Magufuli alifanya kikao cha wazi na Viongozi waTUCTA, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA) kujadili masuala yahusuyo Mafao ya wafanyakazi hususani KIKOKOTOO na Rais Magufuli alifikia hitimisho kwamba Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika).
Pia soma
> Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika) - JamiiForums
Mbuzi wa kafara huyo katolewa...katika watu walioumizwa saana na uamuzi mbovu saana na wakipuuzi uliofanywa na Baraza la mawaziri na Jiwe akiwemo katika kuwaumiza wananchi huyu dada ni mmojawapo kwani alibebeshwa mzigo usio wa kwake..Hii stahili ya kukili makosa kwa kuwatoa kafara watu wengine wasio na hatia ni laana...Anyway mimi sijaelewa kuhusu FAO la kujitoa mustakabali wake utakuwaje au nalo litabaki kama zamani ukimaliza mkataba wako kwa mwajiri unachukua chako choote? ufafanuzi plse
 
Aiseh kawatumikia wengi ni kheri kuliko kumtumikia mmoja
Mwanadamu siku zote hategemeki
Pole sana mama maisha ni mzunguko hakuna aijuaye kesho kamba uliyoitegemea imekatika
 
Mbuzi wa kafara. Muswada ulpelekwa bungeni na waziri na ndiye aliyeupeleka kwa rais baada ya wabunge wa ccm kuupitisha, nadhani ingekuwa vyema kama ingeanzia kwa waziri, wabunge wa ccm ndipo afuate huyo mkurugenzi
 
Nyie watu mkoje? Hivi hili swali si lilitetewa bungeni? Yaani sijui hamna akili ama huwa mnajitoa akili. Irene kwani alikuwa anapanga mwenyewe bila ya kupitisha kwa wenye mamlaka ya kutunga kanuni?

Kikokotoo hutengenezwa na Waziri mwenye dhamana, mkurugenzi wa SSRA hausiki!
Nchi imejaa vichaa baada ya kichaa kujitangaza kuwa yeye ni kichaa,
Nchi ya ajabu ktk hii dunia ni TZ pekee, Irene alifanya kazi yake vizuri na kitaalamu sana kwa faida ya kizazi kijacho, tamko la mtu mmoja kwa sifa za kisiasa litaiangamiza nchi mda si mrefu.
Lord have mercy
 
Jestina Mhagama ni aje? Naye inabidi uteuzi wake utenguliwe mara moja.

View attachment 979879
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isaka.

Mapema leo Rais Magufuli alifanya kikao cha wazi na Viongozi waTUCTA, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA) kujadili masuala yahusuyo Mafao ya wafanyakazi hususani KIKOKOTOO na Rais Magufuli alifikia hitimisho kwamba Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika).
Pia soma
> Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika) - JamiiForums
 
Alitakiwa siku nyingi awe amefukuzwa kazi huyu mama, ni mzinguaje sana toka enzi za jakaya, hata sijui alisurvive VP mpaka leo
 
Ni vichaa Mkuu hawa kama Kichaa Mkuu nchini.

Nyie watu mkoje? Hivi hili swali si lilitetewa bungeni? Yaani sijui hamna akili ama huwa mnajitoa akili. Irene kwani alikuwa anapanga mwenyewe bila ya kupitisha kwa wenye mamlaka ya kutunga kanuni?

Kikokotoo hutengenezwa na Waziri mwenye dhamana, mkurugenzi wa SSRA hahusiki!
 
Back
Top Bottom