Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Wafanyakazi wa mifuko kama NSSF wanajilipa allowance za kutosha yaani kufuja tu ela za mifuko, ila wanachama njaa Kali sana, huyu Irene na wenzie wanatakiwa washitakiwe kabisa huu ulikuwa ufisadi asee
 
Inategemea. Kuna watu wakiwa wanajenga nyumba utasema wao ndo mafundi, wanaelekeza kila kitu. Ss Kama alikuambia tutumie cement, nondo na matofali ya aina flani ukamwambia No tumia ya aina ninayotaka mm na ukamnunulia ukapeleka, halafu ukampangia na ajenge kwa ratio gani ule Ufa Utakuwa unakuhusu wewe sema unaweza mlaumu tu sababu yeye Ndo mkandarasi.
Kuhusu huyu aliyesimamishwa kazi ni sawa, hata mm ningemsimamisha maana utetezi wa 25 to 20% kwe runinga sijui alitumia nn kufikiri.
Nadhani mkandarasi aliyeelimika na kujua majukumu yake hawezi kukubali amri za kijinga hata kama zimetolewa na mwenye mali! Hilo ndilo jambo la kujifunza.
 
Wewe unaumwa. Waziri anasain regulations yeye hazitengenezi. Regulations zinatengenezwa na idara wenye sheria. Mfano, Sheria ya ardhi ikitungwa, regulations zake zinatengenezwa na Kamishana wa Ardhi hivyo waziri wa ardhi huperekewa kusain tu.
Kati ya hao wawili anayesaini na aliyezitunga nani kisheria huhesabika ndiye kazitunga hizo "Regulations"
 
Kama unapata shida kuona kosa lake ngoja nikupe mfano huu: Umempa mkandarasi mkataba wa kujenga nyumba. Baadae ukakabidhiwa nyumba yako na kuichukua. Baada ya siku mbili nyumba ikapasuka ufa! Je mkandarasi hatawajibika kwa sababu tu wewe ulikubali kuipokea ile nyumba?

Mfano irrelevant. Wapinzani walipiga kelele toka mwanzo. Unapokea nyumba mbovu, tena baada ya wataalamu (bunge) wako kupitia ubora wa nyumba na kusema wameridhika na ubora, wakati huo huo kuna wataalamu wengine (wapinzani) wanasema hiyo nyumba haina ubora, kwakuwa unaongozwa na upofu wa itikadi unaamua kuwasikiliza na kukubali kwa kuweka saini kwakuwa unawakubali hao wengi wajinga. Matokeo yake siku chache aibu inakukuta kwamba hiyo nyumba(sheria) kweli ni mbovu. Hapa wakulaumiwa ni rais na wabunge wa ccm. Ni sheria nyingi mbovu hupitishwa na wabunge wengi wajinga wa ccm.
 
Kama unapata shida kuona kosa lake ngoja nikupe mfano huu: Umempa mkandarasi mkataba wa kujenga nyumba. Baadae ukakabidhiwa nyumba yako na kuichukua. Baada ya siku mbili nyumba ikapasuka ufa! Je mkandarasi hatawajibika kwa sababu tu wewe ulikubali kuipokea ile nyumba?
mfano huo ni irrelevant

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafanyakazi wa mifuko kama NSSF wanajilipa allowance za kutosha yaani kufuja tu ela za mifuko, ila wanachama njaa Kali sana, huyu Irene na wenzie wanatakiwa washitakiwe kabisa huu ulikuwa ufisadi asee
Umeambiwa atapangiwa kazi nyingine, maana yake aliyofanya AlitumwA afanye ila imeshindikana. Hayakuwa maamuzi yake
 
Kuna waziri nahisi atakua amepata tumbo la kuharisha anarefresh App zake kila baada ya dakika moja kuona kama kuna jipya.. Sleepless night, lonely night.
 
Jenista Mhagama hapa anappnajee! Nilitegemea na yeye afyekwe

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom