Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Umeona nalilia hapa jukwaani kama ww? Dogo umejichanganya huku ndani, hii ni bundersliga league ya wagumu.
Niko kwenye kilinge cha Internet na forum kabla hata hujaiona computer wewe! Wakati unaziita ''video''
 
Huenda ameangalia sana maslahi ya waajiri kuliko wafanyakazi husika na kuwasahau madhila wanayopata kwenye kupata mafao madogo.

Na hiyo ni kushinikizwa na waajiri hao kuweka kikokotoo cha asilimia ndogo.
Kuchangia ni ile ile 5% mtumishi na serikali 15%. Hivyo kwa waajiri imebaki vilevile ila pension ndiyo hivyo unapewa kidogo. Ilikuwa wasahihishe kosa tu na siyo kumwadhibisha kikubwa hivi.
 
Watanzania mshapotezwa yaani alietunga hiyo sheria na aliesaini sheria wala hamuwajadili tena ila mnamjadili mtu ambae alikuwa analetewa tu mashinikizo toka kwa wanasiasa
 
Mfano unamhusu mkurugenzi. Najua masikio yako yanapenda kuambiwa kuwa rais ni mtu mbaya. Hili halishangazi! Ila kama rais angeingilia wakati wabunge wanapitisha wewe ungekuwa wa kwanza kusema analiendesha bunge kwa rimoti. Kwangu mimi rais amefanya vizuri sana kwani ameacha maji yafuate mkondo wake ili wengi tujue ni wapi kwenye ubovu na wapi kwenye ubora. Kwa hali hii wabunge waliopitisha hiyo sheria keshokutwa watatafakari kabla ya kupitisha mambo mengine.

I will indulge you.

Wazo la kwamba Rais angeingilia wakati liko bungeni huyo bwana angesema hayo unaalitoa wapi? Hata kama kungekuwa na sauti ambazo zingesema ana interfere bunge shida iko wapi? Lingefika hapa? Una tatizo na kuangalia ishu kwa pande zake zote au unatengeneza mchawi mwenyewe kujustify kumpiga?

Nani kakuambia bunge litabadilika kesho kutwa? Ni mara ya kwanza bunge kupitisha sheria zilizokuja kulalamikiwa na rais? Una uhakika gani huu muswada haukupitia kwenye vikao vya wabunge wa vyama kabla ya kupigiwa kura bungeni? Uaamini tatizo liko na linaishia kwenye bunge? Kabla ya leo ulikuwa unaona bunge halina shida?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuchangia ni ile ile 5% mtumishi na serikali 15%. Hivyo kwa waajiri imebaki vilevile ila pension ndiyo hivyo unapewa kidogo. Ilikuwa wasahihishe kosa tu na siyo kumwadhibisha kikubwa hivi.

Ingekuwa hivyo basi mpira ulikuwa upande wa Irene, angemaliza hilo badala ya kusubiri kikao na raisi.
 
Niko kwenye kilinge cha Internet na forum kabla hata hujaiona computer wewe! Wakati unaziita ''video''

Mimi computer nimeanza kuziona mwaka huu, tena huku kwenye forum ni mtu ananisaidia kulog in na kulog out. Asipokuwepo sitii mguu. Una jingine?
 
Sio anajichanganya uyo alikuwa anashinikizwa na wanasiasa sasa nafsi ilikuwa inafanya kitu anajua si sawa. Hapo katolewa kafara tu mmeacha kimjadili aliesaini sheria na kuipitisha tena mnampongeza kabisa
Huyo dada kutolewa kafara ni sahihi kabisa msomi unatakiwa usimamie kile unachokiamini na sio ujinga aliouleta huyu PHD holder wa mkorogo, hili litakuwa ni fundisho kwake hata wakati mwingine kama atapata tena nafasi ya kusimamia maslahi ya wananchi.
 
Mkuu hii treni umeidandia huku ikiwa kwenye mwendo. Sisemi kuwa waziri hawajibiki na ikiwezekana naye afukuzwe kazi lakini nakataa hoja ya kumwona huyu dada kama mtu asiyehusika na kikokotoo (kwamba ameonewa).
Hueleweki unachoandika.
 
Raisi hajatengua maamuzi, ameya ahirisha hadi 2023, wanaonufaika ni watumishi wa umma pekee, wale wa NSSF wanaendelea na 25% kama kawaida. Hizi ni tips muhimu, watu wasianze kutoa macho baadae, maana naona watu wanashangilia tu....
 
Watanzania mshapotezwa yaani alietunga huo mswada na aliesaini ikawa sheria wana hamuwajadili tena ila mnamjadili mtu ambae alikuwa analetewa tu mashinikizo toka kwa wanasiasa
yule dada usomi wake bado haujamsaidia, wengi wanadhani elimu walizonazo ni za kwao pekee yao kumbe si hivyo.
 
I will indulge you.

Wazo la kwamba Rais angeingilia wakati liko bungeni huyo bwana angesema hayo unaalitoa wapi? Hata kama kungekuwa na sauti ambazo zingesema ana interfere bunge shida iko wapi? Lingefika hapa? Una tatizo na kuangalia ishu kwa pande zake zote au unatengeneza mchawi mwenyewe kujustify kumpiga?

Nani kakuambia bunge litabadilika kesho kutwa? Ni mara ya kwanza bunge kupitisha sheria zilizokuja kulalamikiwa na rais? Una uhakika gani huu muswada haukupitia kwenye vikao vya wabunge wa vyama kabla ya kupigiwa kura bungeni? Uaamini tatizo liko na linaishia kwenye bunge? Kabla ya leo ulikuwa unaona bunge halina shida?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mazee sioni mantiki kwenye hoja yako.Rais aliacha maji yafuate mkondo na baade akaingilia. Rais hawezi kuwa kila mahali akifanya kila kitu. Hufanyia kazi yale anayoletewa na yale yenye uharaka! BTW mimi nimefurahi jinsi alivyojipa muda kushughulikia kwani imekuwa ni somo tosha kwa wengi.
 
Back
Top Bottom