Mkuu
TUJITEGEMEE,
Umesema jambo la maana kwamba utajikita kwenye hoja, nami ndipo nitakapojikita kueleza ni kwanini naamini hakutendewa haki!!
Mosi, nakubaliana na wewe kwamba issue kama hizo penye kosa anayetakiwa kusurubiwa ni Katibu Mkuu na watu wake na sio waziri ingawaje waziri nae anaweza kujiwajibisha kwa ajili ya collective responsibility!!
Lakini hoja ya msingi ni kwamba hilo suala sio geni!!
Nakuhakikisha suala la kufuta certificate sio la jana wala leo... kwa mara ya kwanza suala hilo alitangaza aliyekuwa Waziri wa Elimu awamu ya IV, yaani Dr. Shukuru Kawambwa mwaka 2014!
Bila shaka nadhani unafahamu suala la watu kumlaumu kama sio kumlaani JPM kwa hatua yake ya kupeleka walimu wenye shahada kufundisha. Hilo nalo kama ni kulaumiwa ni JK na sio JPM! Nimeleta hilo suala kwa sababu haya mambo mawili yalienda pamoja!
How did it all happen!!
Sina shaka kwamba tunakubaliana kwamba moja ya mafanikio makubwa kabisa ya JK kudahiri wanafunzi wengi with incentives ili wakasomee ualimu kwa ngazi ya shahada! Incentives kubwa zilikuwa ni uhakika wa mkopo na ajira, na kweli walimu wengi sana wakaajiriwa to the point ikafikia hatua Walimu wa masomo ya art ikawa wamefurika mashuleni!!
Kutokana na hilo, ndipo serikali iliyopita ikatangaza walimu wenye shahada ya masomo ya sanaa watakaoajiriwa baada ya hapo, majority wataenda kufundisha primary school lakini stahiki zao zitabaki pale pale.
Sasa kwavile serikali ilishafikia hatua ya kuajiri walimu wenye shahada kwenda primary school, ikaonekana hakuna tena ya kuendelea na ngazi ya certificate!!
Changamoto ambayo ilibaki ni ya walimu wa sayansi kwa sababu hata hao wanaomaliza Form VI kwa masomo ya sayansi, na wenyewe ni wachache, na wengi hawaendi ualimu!!!
Sasa kwavile ilishaonekana certificate ni "useless", ndipo ikaanziswha ile 3 years Special Diploma (Science & Maths) pale UDOM ili walimu watakaopatikana, wakafundishe sekondari na primary school!!
Diploma ninayoizungumzia ni ile ambayo baada ya JPM kuingia tu, akaifuta na kudai wale madogo ni vilaza!
Sasa baada ya serikali kuweka hiyo mipango miwili, ndipo Waziri Shukuru Kawambwa akautangazia umma lengo lake la kufuta mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti, na watakaoenda kusoma ualimu kutokea Form IV ni wale watakaopata kuanzia C kwa ajili ya kusomea ualimu ngazi ya diploma (3 years)!
Do your home work, utaliona hilo tangazo la serikali mwaka 2014, au nikipata muda, nitakutafutia!!
Now tell me: Kama serikali tayari ilishatangaza hadharani zaidi ya miaka 5 iliyopita, huyu Avemaria anahukumiwa kwa lipi?!!
Aidha, baada ya Kawambwa kutangaza, ikabaki ni namna gani suala hilo liwe implemented especially kwa wale walimu ambao tayari wana certificate!!
Jibu la hilo swali kalifafanunua vizuri sana Avemaria kwamba wale wenye certificate sio kwamba watafutwa kazi bali kutakuwa na programs za wao kujiendeleza kwa njia ya masafa huku wakiendelea na kazi! Yaani ni kama ilivyokuwa imefanyika kwa watumishi wa umma ambao ni Std VII Leavers!!
Again, kosa hapo lipo wapi?!
Labda awe amefutwa kazi kwa jambo lingine lakini kama ni suala la kutangaza kufutwa mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya cheti, basi anafutwa kazi kwa kutangaza jambo tayari lipo... jambo ambalo tayari serikali hiyo hiyo ya CCM ilishatangaza since 2014!