Rais Magufuli atengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Ave Maria Semakafu

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Ave Maria Semakafu

Avemaria ni mwanaccm damudamu kabisa. Ni wale ambao wako tayari kuacha kupitia familia wakikimbilia mambo ya chama. Ila ni mkorofi kupindukia. Kuna watu watakuwa wamefurahia sana.
Basi ok mtashangilia na kusifu pamoja nae huko Lumumba
 
Akina mama hawana traits za ukurukupukaji hata siku mmoja - hivi kweli huyu naibu waziri/katibu anaweza kuibuwa mambo/kauli controversial out of the blue kweli, yaani kajitungia yanayo mjia kichwani - I don't think so.
 
Nimjuavyo mwalimu Ave maria Semakafu. Ni mama jasiri asiyeyumba na anasimamia anachokiamini. Mapungufu yake ni kwamba alishindwa kuendana na tabia za kinafiki za ccm wenzake haswa wizarani.

Hakuna mtu kaipindua sekta ya elimu kama waziri Ndalichako kwa mgongo wa ithibati. Na hili alitakiwa atumbuliwe ndalichako sio naibu katibu mkuu lakini hawezi tumbuliwa. Huyu mama wizarani alishindwa kueleweka sababu waswahili wana tabia zao za kufanya kazi bila kutumia akili na weledi
 
Alichokosea huyo Naibu katibu Ni kutangaza,ila kiuhalisia mafunzo ya certificate ualimu yalishafutwa kitambo before 2015.Hakuna Chuo kinachukua wanafunzi was kwenda kusomea ualimu grade A Certificate.Hivyo huyo Naibu katibu Mkuu alikuwa sahihi
 
Huyu aliyotamuka alinishangaza sanaaa.. nilifikiri apo kwa nchi ingine na sio hapa TZ.. natumaini mkwanja alishapokea.. kabla ya kutumbuliwa.. akaufaidi vizuri..😃😃😃
 
Alichokosea huyo Naibu katibu Ni kutangaza,ila kiuhalisia mafunzo ya certificate ualimu yalishafutwa kitambo before 2015.Hakuna Chuo kinachukua wanafunzi was kwenda kusomea ualimu grade A Certificate.Hivyo huyo Naibu katibu Mkuu alikuwa sahihi

Cheo chake hicho.. alikuwa wapi siku zote kutangaza.. huyo kataka kula huku na kule.. kanaswa.. paaaaaap.. kukubali bila kufikiria kazi za upinzani..
 
Huyo ni mwanasisiem kindakindaki, usijidanganye namfahamu vema mno.
Mwanaccm kwa tumbo ila kifikra ni mpinzani kweli kweli, wengi hawamjui huyu mama kwamba ni pasua kichwa.Ila pamoja na hayo naamini kaonewa, amekuwa kama mbuzi wa hitma.
 
Kama yapi?! Ya kumfuta mtu kazi kwa sababu ya kutangaza sera ya serikali yake mwenyewe, au?! Hivi kwa akili yenu mnaamini kabisa Naibu Waziri anaweza kuchukua uamuzi mgumu kama huo pasipo na kuridhiwa na serikali?! Pasipo na kupitishwa na Baraza la Mawaziri?!

But this sounds good kwa sababu kina-reflect kile kile ambacho mara kwa mara tumekuwa tukisema hapa endeleeni kushangilia udhalimu wa hii serikali kwa sababu mnadhani mkiwa ni wapiga makofi mtakuwa salama but none is safe!!!
Naibu Waziri ? Au Naibu Katibu Mkuu ?uwe unatulia kabla ya kuandika
 
Hujui kitu huyo ni mpinzani kabisa, alitaka kuchafua hali ya hewa akaluwa kichwa, chezea JPM wewe
Ofcourse semakafu ni kada kindakindaki..yule ukikata mshipa damu inatoka ya kijani. Ila kwa huyu no.1 hiyo siyo kitu..akiona itamsaidia kisiasa..atakutoa kafara tu.
 
Subiri kimbunga tarehe 28/10/2020. Uone JPM anavyopendwa
Tukisema haya wengine tunaonekana hatumpendi ila kumbe huu ndo ukweli wenyewe. Watanzania wenye akili timamu ni wengi sana na watanzania wasio na akili timamu ni wachache sana. Sioni mtanzania mwenye akili timamu atakayempa kura yake Magufuli hapo 28 oktoba. Sioni kwa kweli
 
Naibu Waziri ? Au Naibu Katibu Mkuu ?uwe unatulia kabla ya kuandika
Does it make any difference?! Ongea hoja za maana sio hoja ambayo hata kama ningesema ni Balozi bado isingebadilisha maana!!

Na hoja hapa ni kwamba HAIWEZEKANI jambo kama hilo lisiridhiwe na Baraza la Mawaziri... anzia hapo sasa, na kama huna hoja, SYFU!!
 
Does it make any difference?! Ongea hoja za maana sio hoja ambayo hata kama ningesema ni Balozi bado isingebadilisha maana!!

Na hoja hapa ni kwamba HAIWEZEKANI jambo kama hilo lisiridhiwe na Baraza la Mawaziri... anzia hapo sasa, na kama huna hoja, SYFU!!
Mkuu, sijui mmeanzia wapi 'kusigana' kwa maneno na Mkuu 'nizakale', hata hivyo najikita kwenye hoja yako ya 'kwamba jambo lazima lilidhiwe na baraza la mawaziri'. Mkuu mchakato wa kuitisha baraza la mawaziri unataratibu zake. Mchakato huu uambata na maandalizi kamambe wa kuandaa mambo ya kujadiliwa huko kwenye baraza.

Kwa uelewa wangu, kama nakosea nitaomba nielekezwe zaidi jinsi utaratibu unavyokwenda; mambo yanayojadiliwa kulekwenye baraza la mawaziri uandaliwa na wizara zote zinazowakilishwa kwenye baraza hilo na mawaziri husika ama kwa kushirikiana ama kwa wizara moja pekee. Maandalizi ya mambo hayo ya kujadiliwa kwenye baraza, ufanywa na watendaji wakuu wa wizara. Hapa ndipo makatibu wakuu na wasaidizi wao wanapohusika moja kwa moja! Waziri 'in a way ni 'kiongozi wa kisiasa zaidi ama kwa mambo ya jumla jumla kuliko utendaji wa kila siku wa wizara hiyo...!

Ni kwa msingi huu huu nilioeleza hapo juu, nivigumu sana hao watendaji wakuu wa wizara kukwepa lawama kutokana na kilichofanyika. Pia, mbali na utendeji wao wizarani, nasisitiza kuwa walipaswa kusoma alama za nyakati. Maana utendaji wao unaathiriwa na maamuzi ya kisiasa. Katika kipindi hiki cha kampeni, kuwafanya wapigakura (in this case, walimu wenye ngazi ya cheti) kuwa na wasiwasi ni kitendo kinachoonyesha uzembe wa kiwango cha 'wastani'!

Karibu Mkuu, kama unalingine juu ya hili.
 
Mkuu TUJITEGEMEE,

Umesema jambo la maana kwamba utajikita kwenye hoja, nami ndipo nitakapojikita kueleza ni kwanini naamini hakutendewa haki!!

Mosi, nakubaliana na wewe kwamba issue kama hizo penye kosa anayetakiwa kusurubiwa ni Katibu Mkuu na watu wake na sio waziri ingawaje waziri nae anaweza kujiwajibisha kwa ajili ya collective responsibility!!

Lakini hoja ya msingi ni kwamba hilo suala sio geni!!

Nakuhakikisha suala la kufuta certificate sio la jana wala leo... kwa mara ya kwanza suala hilo alitangaza aliyekuwa Waziri wa Elimu awamu ya IV, yaani Dr. Shukuru Kawambwa mwaka 2014!

Bila shaka nadhani unafahamu suala la watu kumlaumu kama sio kumlaani JPM kwa hatua yake ya kupeleka walimu wenye shahada kufundisha. Hilo nalo kama ni kulaumiwa ni JK na sio JPM! Nimeleta hilo suala kwa sababu haya mambo mawili yalienda pamoja!

How did it all happen!!

Sina shaka kwamba tunakubaliana kwamba moja ya mafanikio makubwa kabisa ya JK kudahiri wanafunzi wengi with incentives ili wakasomee ualimu kwa ngazi ya shahada! Incentives kubwa zilikuwa ni uhakika wa mkopo na ajira, na kweli walimu wengi sana wakaajiriwa to the point ikafikia hatua Walimu wa masomo ya art ikawa wamefurika mashuleni!!

Kutokana na hilo, ndipo serikali iliyopita ikatangaza walimu wenye shahada ya masomo ya sanaa watakaoajiriwa baada ya hapo, majority wataenda kufundisha primary school lakini stahiki zao zitabaki pale pale.

Sasa kwavile serikali ilishafikia hatua ya kuajiri walimu wenye shahada kwenda primary school, ikaonekana hakuna tena ya kuendelea na ngazi ya certificate!!

Changamoto ambayo ilibaki ni ya walimu wa sayansi kwa sababu hata hao wanaomaliza Form VI kwa masomo ya sayansi, na wenyewe ni wachache, na wengi hawaendi ualimu!!!

Sasa kwavile ilishaonekana certificate ni "useless", ndipo ikaanziswha ile 3 years Special Diploma (Science & Maths) pale UDOM ili walimu watakaopatikana, wakafundishe sekondari na primary school!!

Diploma ninayoizungumzia ni ile ambayo baada ya JPM kuingia tu, akaifuta na kudai wale madogo ni vilaza!

Sasa baada ya serikali kuweka hiyo mipango miwili, ndipo Waziri Shukuru Kawambwa akautangazia umma lengo lake la kufuta mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti, na watakaoenda kusoma ualimu kutokea Form IV ni wale watakaopata kuanzia C kwa ajili ya kusomea ualimu ngazi ya diploma (3 years)!

Do your home work, utaliona hilo tangazo la serikali mwaka 2014, au nikipata muda, nitakutafutia!!

Now tell me: Kama serikali tayari ilishatangaza hadharani zaidi ya miaka 5 iliyopita, huyu Avemaria anahukumiwa kwa lipi?!!

Aidha, baada ya Kawambwa kutangaza, ikabaki ni namna gani suala hilo liwe implemented especially kwa wale walimu ambao tayari wana certificate!!

Jibu la hilo swali kalifafanunua vizuri sana Avemaria kwamba wale wenye certificate sio kwamba watafutwa kazi bali kutakuwa na programs za wao kujiendeleza kwa njia ya masafa huku wakiendelea na kazi! Yaani ni kama ilivyokuwa imefanyika kwa watumishi wa umma ambao ni Std VII Leavers!!

Again, kosa hapo lipo wapi?!

Labda awe amefutwa kazi kwa jambo lingine lakini kama ni suala la kutangaza kufutwa mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya cheti, basi anafutwa kazi kwa kutangaza jambo tayari lipo... jambo ambalo tayari serikali hiyo hiyo ya CCM ilishatangaza since 2014!
 
Mkuu TUJITEGEMEE,

Wakati tunajadili nilidhani serikali ya JPM ilisitisha mpango wa serikali ya JK! Leo nilipoingia tovuti ya Wizara ya Elimu, nimekuta hili tangazo:-

TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA AWALI, MSINGI NA SEKONDARI MWAKA WA MASOMO 2020/2021​

Unaona hapo, ingawaje ni mafunzo kuanzia elimu ya awali, msingi, na sekondari lakini mafunzo yenyewe ni ngazi ya stashahada (diploma) na sio certificate kwa sababu ilishafutwa kitambo!!

Na baadhi ya programu husika ni hizi hapa:-

Cheti.png


Utaona hapo, ndo kile kile nilichosema mwanzo kwamba tangazo la kufuta ngazi ya cheti ni since 2014, na sasa ni 3 years diploma Div I-III kwa waliomaliza Form IV, na serikali ya JPM kumbe tayari imeshaanza kufanyia kazi kwa vitendo!

Full tangazo, linapatikana hapa!

Hapo ndipo tunajiuliza, unamtimua vp kazi mtu anayeujuza umma jambo ambalo kumbe hata serikali yenyewe imeshaanza kutekeleza kwa vitendo?!
 
Unga tu kwanza mkono utumbuaji huo
💯mkuu
Ukipewa kazi na serikali hii ya John Pombe Magufuli inabidi ufanye kazi zako kwa uadilifu na viwango huku ukitambua kabisa kwamba unatakiwa kutembea kulekule inapotembea serikali.

Kufanya maamuzi yanayohitaji idhini ya serikali na yanayogusa maslahi ya watu bila idhini na kuyatangaza na kuyatekeleza ni hujuma kwa waliotakiwa kuidhinisha.
Alivuna alichopanda
 
Back
Top Bottom