Rais Magufuli atengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Ave Maria Semakafu

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Ave Maria Semakafu

Kabisa! Huyu mama katolewa kafara. Uamuzi wa kubadili sera usingeweza kufanyika bila ridhaa ya baraza la mawaziri ambapo Rais ni mwenyekiti, wizara inatekeleza tu.

Sasa hapa eti tunaaminishwa kwamba uamuzi huo ulifanya na NAIBU katibu mkuu? Wala sio katibu mkuu au naibu waziri au waziri? Hizi hadaa nyingine hapana..
Ingawa kamuonea huyo mama,lakini huyo mama anajulikana kwa ujinga wake meingi sana hapo wizarani
 
Keshaa mwongezea ajenda mpya nyingine T.Lissu
Siyo kapata ajenda bali kapata ilani kwani ilani zake huzitunga papo kwa papo toka kichwani kwake. Hana ilani ya maandishi inayoinadi kwenye kampeni zake.
 
Huyo mama anatoka kanda gani. That's very important because we're told it's only Federal System of Government, rather than Unitary System of Government that breeds tribalism and nepotism.
 
Tafadhali Lissu popote ulipo, hili uailiache maana kuna watu wanamshambulia mama Ave Maria na kuonekana amekurupuka.

Najua kuna watu watasema unatetea 'wahalifu' lakini nenda mbele zaidi kwa kuwafumbua wananchi uwepo wa Double standard kwenye Serikali hii kwa sababu haiwezekani suala la kisera na kubwa kama hili-Waziri, Naibu wake, Katibu Mkuu na wakugurenzi baadhi kwenye Wizara bado wanadunda. Huu hauwezi kuwa aumuzi wa Naibu Waziri, tamko limetolewa na mpaka linasainiwa maana yake kuna hatua kadhaa limepitia.

Hatuwezi kuendelea kama tu, kwenye Serikali moja watu walioko timu moja anatumbuliwa mtu ambaye hata sio kiongozi wa timu! Disguisting.
 
Hata hili la kutenguliwa usikute ni uongo likatenguliwa baadae ngoja tuone.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Oktoba, 2020 ametengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu.

Nafasi hiyo itajazwa baadaye.

View attachment 1591621

PIA SOMA
= > Siku ya Mwalimu Duniani: Wizara ya Elimu yafuta rasmi mafunzo ya Ualimu wa shule ya msingi na awali ngazi ya Cheti Tanzania

= > News Alert: - Dodoma: Rais Magufuli apiga simu mubashara kwenye Kongamano la CWT na kukanusha kufutwa kwa Ualimu Ngazi ya Cheti
Magufuli anapingana na ilani anayoinadi? Maana kilichoandikwa katika waraka aliosaini Semakafu kimo ndani ya ilani ya CCM anayotembea nayo.
 
Mwisho wa Fascist umewadia..Watanzania ni wakati wa kurudisha nchi yetu kwa wazawa..mijitu mikatili ya nini?
 
Bahati bukuku. dunia eeh haina huruma.... tunapanga wote likiharibika unanichenjia mbele za watu... dunia oooh haina huruma......
 
Kwamba kafukuzwa kazi kwa kusoma Tangazo? Haya si ni maamuzi ya Wizara na baraza la mawaziri yaani Serikali?

Ni sawa na kumfukuza kazi Afisa habari wa Yanga kwa kutangaza kuwa Yanga imesitisha mkataba na kocha mzungu. Wakati yeye anawasilisha kilichoamriwa na Taasisi yake?
 
Hapo Mbwa kala mbwa.
Japokuwa kile kimama kimeonewa, lakini kile kimama kilikuwa na nyodo za kiCCM sana, kilikuwa kinajiona kimeshafika pale kisa kuteuliwa na Rais. Leo kimetumbuliwa usiku usiku. Huko kilipo lazima kipandishe sukari.

Yote kwa yote walimu walishaamua kuitosa CCM na Magufuli kwenye uchaguzi huu. Oktoba 28, kichapo kipo pale pale. Magufuli ajipange kulizwa tu.
Du eti kimetenguliwa usiku usiku 🙄🙄anachojaribu mgombea huyu aliekata pumzi ni kutaka kukomboa Kura za walimu.
 
Nimesoma comments 96 nimeona comments mbili tu zilizokaa ki LUMUMBA KUMBA hii inaonesha hata hao BOOK SEVEN kina mambo yanawakera likilobaki wanalinda UBWABWA wao tuu
Comment yako tu niya 95, hizo 96 umezisoma wapi ?!
 
Na anaeleweka kwa adhira yake.
Siyo kapata ajenda bali kapata ilani kwani ilani zake huzitunga papo kwa papo toka kichwani kwake. Hana ilani ya maandishi inayoinadi kwenye kampeni zake.
 
Utenguzi huu unafikirisha sana, kwamba kuna haja kwenye sheria na kanuni za uendeshaji nchi kuwe na kipengele cha kumzuia mgombea urais ambaye ndiye Rais aliye madarakani kutofanya teuzi, tenguzi au maamuzi yoyote makubwa katika kipindi cha kampeni ya Urais, kwani teuzi au tenguzi hizo zaweza kushawishi uelekeo wa wapiga kura.

Katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi, watendaji wanapaswa kuwa waangalifu sana, kwani kauli na maamuzi yao yanaweza kushawishi katika kuongeza ama kupoteza kura za chama. Sio siri kwamba uamuzi huu wa vyeti vya waalimu ulikuwa unakwenda kupoteza kura nyingi za chama tawala, hivyo kutengua uamuzi huo maana yake ni kujaribu kuzinusuru kura hizo ili zirudi upande wa chama tawala.

Sina hakika na kigezo kilichotumika kutengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wakati juu yake kuna Katibu Mkuu, Naibu Waziri na Waziri mwenyewe.
 
Kuanzisha stashahada, sio kufuta astashahada
Sasa ndugu kwa position hiyo hiyo moja akija mtu wa stashahada na mwingine wa astashahada kwa logic ya kawaida tu unafikiri nani atakayechukuliwa? Automatic ni wa stashahada.

Nachokiona huyu mama aliamua kuelezea kwa lugha rahisi itakayoeleweka na wengi maana kwenye ilani wamejitahidi kuificha ficha kwa kuiwekea maelezo mengi lkn point kubwa ni mwisho wa siku ifutike.

Kilichotakiwa hapa watoe ufafanuzi kwa nn wameona hilo ni bora kwa mazingira ya sasa na kwenda mbele na sio kuanza kurukaruka kimanga na kutoana kafara ili wengine waonekane ndio wabaya na wengine wazuri wakati issue kama hizi haziamuliwi na mtu mmoja, basi kama ni hivyo apige chini panel nzima iliyopitisha hili suala wizarani na walioliweka kwenye ilani.
 
Back
Top Bottom