zagarinojo
JF-Expert Member
- Jul 26, 2020
- 2,622
- 2,846
Yeah kitu muhimu ni kuheshimu madaraka na uwezo wa mwenzie katika uongozi..Mkuu sijapinga watakuja wengine wa kufanya mambo mazuri zaidi. Ninachohuzunika ni pale kiongozi anayefuata anaona wa nyuma yake hawajafanya kitu. Kila mmoja anafanya alivyojaliwa hivyo wengine wanapokea kijiti kuendekeza na kuongeza vingine. Huo ndiyo uongozi na si kunanga waliopita.
Mimi siangaliagi wala sisikilizagi hizo mambo, naumiaaaWakuu naomba niwaulize kitu.
Wakati nasikiliza hiki kipande machozi yamenitoka. Ni kila mmoja wetu yamemtokaaa au ni mimi tu na watu wachache. Nikimaanisha kweli kunaambae ataangalia hiki kipande asitokwe na machozi kabisa?
Je yule ambaye hayajatoka machozi kwamba yuko stronger than sisi tuliotokwa machozi??!!
Hem naombeni michango yenu ktk hili maana dah basi binadam tutakua tunatofautiana sana tena.
nilie [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wakuu naomba niwaulize kitu.
Wakati nasikiliza hiki kipande machozi yamenitoka. Ni kila mmoja wetu yamemtokaaa au ni mimi tu na watu wachache. Nikimaanisha kweli kunaambae ataangalia hiki kipande asitokwe na machozi kabisa?
Je yule ambaye hayajatoka machozi kwamba yuko stronger than sisi tuliotokwa machozi??!!
Hem naombeni michango yenu ktk hili maana dah basi binadam tutakua tunatofautiana sana tena.
Ni msiba mzito halipingiki sote ni yetu njia. Alijitahidi kutufikisha sehemu kama taifa hakuna mkamilifu zaidi ya Muumba kizuri ameacha WOSIA.Pole sana Jpm huu ni msiba mzito sana kwako. Mungu akutie nguvu. Najua huko magetoni hapakaliki ni kilio mwanzo mwisho
Hebu niulize wakuu hapa:Kama kweli alikuwa ni shujaa wake amuenzi kwa kulifanyia kazi ombi la Mkapa ili Tume Huru ipatikane kabla ya uchaguzi wa 2020.
Hebu niulize wakuu hapa:
Kwani Tume ya kusimamia uchaguzi inahitaji watu wenye utaalam wa aina gani?
Tukikusanya maaskofu kadhaa na Masheikh wa kutosha na kuwakabidhi jukumu la kusimamia uchaguzi kwa haki, hawa watu hawawezi wakaifanya hiyo kazi kwa ufanisi katika muda huu mfupi uliobaki kabla ya uchaguzi?
Lakini CCM hawataki hata kulisikia hili; na kwa kustaajabisha kabisa, hata wapinzani halionyeshi kuwaumiza vichwa!
Mbona hili ni rahisi sana mkuu 'Tripo9.'Wakuu naomba niwaulize kitu.
Wakati nasikiliza hiki kipande machozi yamenitoka. Ni kila mmoja wetu yamemtokaaa au ni mimi tu na watu wachache. Nikimaanisha kweli kunaambae ataangalia hiki kipande asitokwe na machozi kabisa?
Je yule ambaye hayajatoka machozi kwamba yuko stronger than sisi tuliotokwa machozi??!!
Hem naombeni michango yenu ktk hili maana dah basi binadam tutakua tunatofautiana sana tena.
Kwahiyo kalipiza kunyweshwa sumu kwa kutaka kumuua lisu?Hata we ukija kuwa raisi utakuja kuona jinsi ilivyokuwa ngumu kuongoza kila kashfa nzito kwenye nchi utahusishwa wewe...
Hata yeye aliwahi kunyeshwa sumu na hata akakaribia kukata tamaa ya uongozi..
Huyu mzee alitulea wote kama taifa,sioni hasara kwa mzee magu kumwaga chozi,we ve to learn how to appreciate
RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli, amejikuta akitokwa machozi hadharani baada ya shindwa kujizuia wakati akielezea mazungumzo yake ya mwisho na Rais mstaafu awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam
Hilo limejitokeza leo Jumanne tarehe 28 Julai 2020 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kulipokuwa kunafanyika shughuli ya kuaga Kitaifa mwili wa Mkapa aliyefariki dunia Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 saa 3:30 usiku kwa mshituko wa moyo.
Akihutubia taifa katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya waombolezaji uwanjani hapo, Rais Magufuli amesema “hakuna mtu anayeweza kumwelezea vizuri Mzee Mkapa zaidi alivyojieleza mwenyewe vizuri kwenye kitabu chake cha My Life, My Purpose.” (Maisha Yangu, Kusudio Langu).
Katika hotuba yake, Rais Magufuli ambaye alikuwa mara kadhaa anatulia, akilengwa lengwa na machozi akisema kifo cha Mkapa ni pigo kwani ilizoeleka katika matukio makubwa anaungana na marais wenzake wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Mrisho Kikwete ‘lakini leo hapa hayupo.”
“Mzee Mkapa alinilea kama mtoto wake, alikuwa ni shujaa wangu, alinionyesha upendo,
“Hata kwenye shida Mzee Mkapa hakuniacha kamwe, hakutaka nianguke, alinilea kama mtoto wake. Wakati wote alikuwa ananionyesha upendo, hivyo basi kuondoka kwake ni pigo kubwa kwangu, nimepoteza mtu muhimu kwangu.”
“Saa nyingine machozi yanakuja tu msinishangae sana, hata Mzee Kikwete nilimuona juzi anadondosha machozi tena Kikwete ni Kanali ila alitoa chozi kwahiyo msinishangae mimi,” amesema Rais Magufuli
“Nilipata fursa ya kuongea na Mzee Mkapa kwa simu akiwa hospitalini saa chache kabla hajafariki, nakumbuka aliniambia John usiwe na wasiwasi naendelea vizuri sikujua kwamba maneno yale yalikuwa ya kuniaga. kazi ameikamilisha,” amesema Rais Magufuli huku akitulia na kutoa kitambaa kufuta machozi.
Sasa kama mkapa ndio alikuweka hapo ulipo, yaani ulivyokuwa mtu wa kubebwa bebwa, without merit, na kwa sababu umetuambia wazi watanzania kwamba hapo ulipo sio kwa kura za wananchi, sasa Oktoba unaondoka.
Atatokwa na machozi pia Oktoba mwaka huu. Kauli mbiu #Miaka Mitano Inatosha.
Aliwahi msifia wakati ule mkapa akizindua kitabu chake my life my purposeHaya maneno alitakiwa ayaingee wakati Mkapa yuko hai. Maana mzee Mkapa angeona fahari kwamba kuna kuna fadhila ana rudishiwa.
Lakini kumsifu marehemu haileti faida zaidi ya kuongea.
Tulizowea kusikia Mh JPM akituambia watangulizi wake hawakufanya kitu. Na nchi imeliwa sana. Kumbe sio kweli? Leo ana tuambia Mzee Mkapa ndie royal model wake. Ndie mwanzilishi wa karibu vitu vyote anavyo endeleza. Tushike lipi? /RIP BABA Mkapa.
Mjumbe na kauli zakePole sana Rais
Tupo pamoja nawe..
Tafuta uzi humu kuhusu legacy ya mzee mwinyi uelewe kwa undani mchango wa mzee mwinyi katika taifa hili.Swali zuri sana. Nimesikia kuwa kulikuwa na kodi ya kichwa, baiskeli na mifugo wakati huo! Lakini usishangae wanasiasa wakampamba Mwinyi kuliko Mkapa. Tuombe tu uzima.
Upo uzi humu ukieleza kwa undani legacy ya mzee mwinyi.Kwa mujibu wa sifa zilizotolewa katika kipindi hiki ni wazi kuwa Mkapa alipokea taifa toka kwa Mzee Mwinyi likiwa KOPO TUPU. Sasa sijui Mzee Mwinyi sifa zake zitakuwa zipi akifa.
Hapana, jk amestaafu jeshini mwaka 1992 akiwa na cheo cha Luteni kanali.Kanali
Alistaafu akiwa luteni kanali 1992Hivi Kikwete alistaafu au aliacha jeshi akiwa na cheo gani #luteni au #kanali? Magufuli nimemsikia akisema alikuwa ni #kanali lipi jibu sasa?