Rais Magufuli awaambia Waandishi wa Habari wawe makini, hawako huru kihivyo...

Rais Magufuli awaambia Waandishi wa Habari wawe makini, hawako huru kihivyo...

nilivyoelewa yakitokea matukio ya ajabu yasiripotiwe na yasiandikwe kwa magazeti page za mbele ikiwizekena yasiandikwe kabisa ata kama watu wamepoteza maisha wakati mwengine ata kama sheriza za nchi zimevunjwa la muhimu zaidi tuijikite tu kwenye habari za maendeleo kama yapo
 
huyu jamaa hapendi kabisa kukosolewa na leo amemind magazeti yote kufunikwa na nape, na kuna sehemu kapiga mkwara itv bila kutaja jina kuwa wao habari za maandamano ya wakulima na wafugaji ndio habari wakae macho!

Twafwaaaaa!
 
aa5a930ec14eaa49104b034192165e7a_-online-casino-cat-meows-funny-meow-memes_500-370.jpeg
 
Kumbe huyu mjamaa wetu toka chaa tuu huwa anashinda humu jf kufuatilia wadau wanavomchana mubashara! Basi atapasuka na alivo na gubu kama ashangedere.
 
Niseme ukweli leo Mtukufu Rais nimeeielewa sana hii kauli yake.

My Take; Na hasa wa vijijini.
 
hata baada ya uchaguzi wa marekani kuisha na DJT kuchukua nchi, Democrats walisema DJT amepata kura nyingi kutoka nkwa wamarekani 'wa vijijini'.
 
Huko vijijini ndo kuna Waalimu wengi, Madaktari, Vifaa tiba, Maji, MajoshMh.Nape sio jambazi, hana record za uhalifu.Kitendo cha kutolewa bastora si cha kitanzania na si cha kiaskari,Nimemuagiza IGP achukue hatua.o, Mbolea nyingi
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John P. Magufuli, leo amewaapisha Dr Harrison Mwakyembe na Prof Palamagamba Kabudi pamoja na mabalozi kadhaa Ikulu Jijini Dar.

Mwakyembe ameapishwa kuwa Waziri mpya wa habari, Profesa Kabudi kaapishwa kaapishwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria.
==>Haya ni mambo machache aliyoyasema Rais Magufuli Leo
1.Kuna wengine walisema Kinana leo angezungumza na waandishi, wakati nimemtuma India ambapo atakuwa kwa zaidi ya siku 10
2.Tunataka kuitoa nchi katika hali ya mazoea kuipeleka katika mstari ambao ni sahihi
3.Ukiangalia siku iliyofuata baada ya Rais wa Benki ya Dunia kuja, magazeti yote yaliandika habari nyingine tofauti-
4.Niwatake waandishi wa habari muwe wazalendo, Tanzania ikiharibika na nyie pamoja na wanaowatuma muandike wote mtaharibikiwa
5.Hata magazeti ya leo yana picha ya mtu mmoja ambaye amefanya kosa moja, utadhani kosa ni linaungwa mkono na serikali
6.Niwatake wamiliki wa vyombo vya habari muwe waangalifu, kama mnadhani mna uhuru wa namna hiyo, kuweni makini sana
7.Kuna vyombo vingine vya habari sehemu yenye ugomvi ndio wanapeleka kamera na habari hizo zinapewa muda mrefu, 'watch out'
8.Vyombo vingine haviandiki mazuri ya mtu, lakini wakipata mabaya yake ndiyo yanajaza kurasa
 
hata mimi alipo sema hiyo "hasa wa vijijini" nilimuelewa sana anatamani wote tuwe na akili za kijijini kama koromije!
 
Sijui nitakamatwa?nataka nichapushe tshirt "..naeleweka vijijini "
 
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ametoa onyo kwa vyombo vya habari nchini humo kwa madai vinaandika habari zisizo za kizalendo.

Kiongozi huyo amemtaka waziri mpya wa Habari Dkt Harrison Mwakyembe kuvichukulia hatua za kisheria.

"Kila kitu chenye nia ya uchochezi fulani fulani, wao ndio stori. Sasa Mwakyembe kafanye kazi. Nataka ukafanye kazi. Kama wapo waliokuwepo waliokuwa wanashindwa kuchukua hatua wewe kachukue," amesema Dkt Magufuli alipokuwa anamwapisha Dkt Mwakyembe na mabalozi ikulu.

"Kwa ni mwanasheria mzuri, msomi, umesomea mambo ya habari, kafanye kazi. Serikali ipo. Hatuwezi tukaiacha serikali ikaangamia kwa sababu ya wat wachache.
Rais Magufuli ameonyesha kuchukizwa na habari zilizopamba ukurasa wa juu katika magazeti ya leo ambapo magazeti mengi yameweka picha ya aliyekuwa waziri wa habari Nape Nnauye akitolewa bastola katika vurugu zilizotokea jana.

"Hata kasomeni tu leo magazeti ya leo. Picha yote heading ni picha ya mtu ambaye alifanya kosa moja, kana kwamba kitendo hicho kilifanywa na serikali. Kwanza ukurasa wa pili, huyu anatoa anafanya hivi....nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari, tahadharini. Kama mnafikiri mna uhuru wa namna hiyo, haujafikia huko."
 
Back
Top Bottom