Rais Magufuli awaambia Waandishi wa Habari wawe makini, hawako huru kihivyo...

Rais Magufuli awaambia Waandishi wa Habari wawe makini, hawako huru kihivyo...

Subiri.jpg
 
Ebu fuatilieni miradi ya maendeleo muone mambo yanavyokwenda. Nyie mmekalia Rais, rais. Huyo ndiye Rais, ukiona vipi hama nchi.

Labda kile kiwanja cha ndege cha Chato,lakini mpaka sasa hivi hakuna cha maana zaidi ya kelele na kulaumu upinzani.Sijawahi kusikia Rais anayeweza kuangalia kipindi kama kile cha SHILAWADU,ukitaka kujua tabia ya mtu angalia rafiki zake.Kwa urafiki wa RAis na Makonda nimeshajua tabia ya Rais wetu.Sina sababu ya kuhangaika naye
 
Watu wa Kyela msifanye makosa tena
Mlisema hivi last time mbona bado alipita.!! Sasa wizara imepata waziri. Mh Mwakyembe hana uswahili kabisa. Huyu anaweza kukaa na Dr Magufuli wakazungumza. Maana wote ni watu wa kazi na sio porojo. Sio yule mwingine.
 
kwani vyombo hivi vimefunguliwa ama kuendeshwa na ruzuku ya serikali yeye aende akajambe huko uhuru publication na Tanzania News Standard anaowalipa . mie chombo changu nimeanzisha mwenyewe sikuomba mkopo kwa mtu najiamini asiniingilie tena akifanya hivyo ndo napoteza kabisa. Vijana wangu wa NEWS room nasema chapeni kazi bila kuogopa mimi bosi wenu niko na nyinyi mtu yeyote asiwatishe akiendelea na haya madrama yake kama ya jana na yeye mnambashite tuu . sitaki fyokofyoko kwenye media yangu
 
Watu wa media msiposimama kidete mtapotea, shujaa wenu Nape ameishatolewa kafara sasa ni wakati wa wana habari kupaza sauti kupinga ukandamizaji huu wa wana habari
Wanahabari wakiungana na bunge pamoja na wanasheria kwa umoja wao.Serikali inaweza salimu amri!
 
Utawala wa awamu ya nne, mlikuwa siku zote kumtukana mzee kikwete kwamba anatumia pesa za umma kwa safari, kwamba yeye wakati wote ni kuchekacheka, mlilalamikia ubarifu wa mali za umma zilivyokuwa zinapondwa na wachache na mengine mengi. Leo mmepata Magufuli, hasafiri, hacheki, anabana matumizi, wabadhirifu kwake kiama. Mnabezabeza kila anachokifanya. Kama mmetumwa na mnatumika kizembe hivyo, hameni nchi
 
Magu yupo makini mno. Hivi siku ile mengi alila Clouds au mbona alifika clouds mapema mno
 
Mlisema hivi last time mbona bado alipita.!! Sasa wizara imepata waziri. Mh Mwakyembe hana uswahili kabisa. Huyu anaweza kukaa na Dr Magufuli wakazungumza. Maana wote ni watu wa kazi na sio porojo. Sio yule mwingine.

Katibu Mwakyembe wakina shilole wanakusubiri waziri wao
 
Aliyeongea na waliokuwa wanamsikiliza ni vilaza.lazima wajue tupo temporary tu
 
Back
Top Bottom