Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Rais Magufuli awateua Humphrey Polepole na Bi. Riziki Said Lulida kuwa wabunge wa Tanzania

Mimi nafikiri mzee wa ‘Nnji’ hii, kwa lile beberu alilotoa pale Himo, apewe nafasi kwenye hivi ‘viti maalumu pia’!!
 
Nathubutu kusema, polepole anafaa kuandaliwa kuwa rais wa nchi hii au waziri mkuu..
Hutaki acha! Safari ya kumuandaa kuelekea huko imeanza

Umewaza kama mimi tu comrade, kwa mrengo wa nchi yetu, ujamaa na kujitegemea Polepole ni mtu sahihi sana, na niliyaona maandalizi yake tangu yupo vyuoni huko, kwenye asasi za kiraia, katiba ya warioba, mwenezi wa CCM, mbunge.

Namuona kama waziri wa ULINZI, au wizara ya KATIBA NA SHERIA
 
Naomba kufahamishwa zaidi juu ya Bi Riziki Said. Je aweza kuwa anaenda kutwaa nafasi ya Umi?

Mkuu Mr Q sidhani kama atapelekwa kwa Madam Umi labda kwa madam Ikupa ili kuwawakilisha watu wenye mahitaji maalum. Kama sijakosea, yeye anatokea Mtwara hivyo pia atawawakilisha wakina mama wa mikoa ya kusini.
 
Na huyo Mama si alikuwa Mbunge Viti Maalum CUF 2015-2020 kumbe aliunga juhudi kimya kimya?


Mbunge Wa (CUF) Riziki Lulida Aomba kurudi CCM:

Riziki Lulida, Mbunge wa Viti Maalum (CUF) ameomba kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipokuwa akichangia bajeti kuu ya Serikali mwaka 2020/21.

Riziki ameeleza kuwa anaomba msamaha kwa wote aliowakosea na yeye amewasamehe wote waliomkosea na anaomba apokelewe CCM ili kuendeleza gurudumu la kumuunga mkon Rais.
 
Ila kwa huyu mama, nameikiliza uongeaji wake na ujengaji wake wa hoja kupitia youtube, binafsi sijajua kigezo kilichotumika...anajua rais mwenyewe na anavyotaka mtumia!
 
Yes, kakisaidia chama na kwa kuwa huu ndiyo muhula wa mwisho wa kwa Rais inabidi apewe shavu - si yeye tu kwa uzoefu wengine watafuata
Wengi wa kutoka kule watafuata hata Pascal Mayalla (Njaa kwisha) safari hii hatakosa kwa kuunga mkono juhudi miaka 5 iliyopita. Mimi niliunga mkono juhudi ni wa huku sina changu!
 
Baada ya kazi kubwa alioifanya POLEPOLE Leo ampa zawadi ya ubunge.
Screenshot_20201129-101521.jpg
 
Nikuambie tu,ninamfahamu Magufuli tangia akiwa nobody,nimesoma,uwezo ninao. Sema mimi sio mwanasiasa. Na kwenye eneo langu la kazi mimi ndo Chief wa service. Iam happy where iam.Ningetaka vyeo vya kisiasa ningeshapata longtime.
Kwani yeye anateua wa vyeo vya kisiasa tu? Wakuu wa taasisi zote za kimamlaka ni wanasiasa?
 
Naomba kufahamishwa zaidi juu ya Bi Riziki Said. Je aweza kuwa anaenda kutwaa nafasi ya Umi?
Acha maskhara mkuu, ummy anarudi kwenye kitu chake cha enzi pale pale wizara ya afya.
 
Mkuu unaelewa nini mtu akisema Ndugu Polepole ni mjengaji mzuri wa hoja? Sitaki kukupinga ila tu nikuambie ukitaka kuuona ujengaji hoja wa mtu yeyote achilia mbali Polepole jiweke neutral.

Ukiwa na upande wa kuegemea tu hutoweza hata kumkosoa mfuasi wako mwenyewe.

Fuatilia vizuri post zangu, kuna mahali nimemwambia kuwa alikuwa mjenga hoja mzuri zamani maana alikuwa neutral, sio sasa hivi akiwa kwenye ulaji, tena kwa serikali hii iliyoingia madarakani kwa kumwaga damu na wizi wa kura wa wazi hivyo.
 
Nilitegemea bashiru nae atakuwepo, labda bashiru mwenyewe hataki ila nae kafanya kazi kubwa sana mwaka huu

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Ya kupanga wizi wa kura? Unafanya kazi kubwa kisha 2/3 ya wapiga kura hawajitokezi, au ndio mambo ya kuvikana vilemba vya ukoka?
 
Back
Top Bottom