Rais Magufuli awatumbua Kitila Mkumbo, Ole Sendeka na Katambi, awateua Jumanne Fhika, Dr. Aloyce Nzuki, Allan Kijazi, Josephat Paulo, Kemikimba

Kwa mimi sioni cha ajabu hapo na hakuna utumbuaji wowote uliofanyika ni taratibu na kanuni zinafuatwa. Ukishatia nia kuutaka uongozi kwenye mhimili mwingine tofauti na uliokuwepo automatically unakuwa umeuacha uongozi ulionao kwenye mhimili wa kwanza hasa kwenye serikali. Hivyo lazima Rais ateue mwingine ili shughuli za serikali ziendelee kama kawaida kwa kuwa zenyewe huwa hazisimami.

Lakini pia ni kwa faida ya wagombea wengine ili kuwe na usawa wa kuzitafuta kura, isijetokea mtu akatumia madaraka ya ukuu wa mkoa, wilaya, ukurugenzi na vyeo vingine kujinufaisha kisiasa na kuwaamulia wananchi.

Ieleweke tu kwamba hakuna utumbuaji unaoendelea.
 
Picha ndio kwanza linaaanza. Yani hii ni vita ya ndani kwa ndani kwanza kabla ya kwenda kushindana na upinzani. Mungu awasaidie wote na wakishindwa wasirudishwe na wasipewe vyeo tena hawana nidhamu kukiuka amri ya mheshimiwa Rais.
Wengi sana hao , asipo wakumbuka wataitikisa CCM, wapo ambao atawachinja lakini wengi atawapa nafasi za kutafuta riski.
Kwa sababu yapo majembe ya ukweli katika hilo kundi, japo kenge ni wengi pia.

Kwa wingi huo wakienda upinzani CCM lazima kutokwa mashuzi.
 
Niseme kwa dhati kabisa hii ndio comment au reply bora kabisa kwenye Uzi huu, wengine wanarukaruka tu kama maharagwe yanayochemka ,big up
 
Shida iko kwako kwakuwa na uelewe wa panadol
Kama ni hivyo kuna haja gani sasa ya kuchagua Raisi mpya kama kila kitu ni lazima kibakie kama kilivyo alivyokikuta? Raisi wa JMTZ Katiba inamruhusu kufanya anavyofanya, shida iko wapi?
 
Yeye alipokua mwalimu mbona hakuridhika na cheo chake akaenda kugombea ubunge?Ni tamaa au?
Magufuli Alikuwa akifundisha shule ya private sio ya serikali hamia private na wewe uwe free ondoka serikalini
 
Kijazi wa TANAPA ameteuliwa kua Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mali asili huku akiendelea pia na u-boss wake pale TANAPA.

Hao ndio wenye nchi sasa,wanyonge walie na umaskini wao tu.
Hapa hapajakaa vizuri, kofia mbili katika wizara moja!!!
 
Katika uongozi wa juu lazima usafishe nyumba mara tuu baada ya kuingia. Hao matechnocrats ilibidi waondoke tuu hasa wa level ya juu kabisa.

Naamini utakubali kuna nidhamu katika utumishi wa umma leo hii kuliko wakati wowote ule wa tawala zilizo pita, labda wakati wa Nyerere.
 
Kijazi wa TANAPA ameteuliwa kua Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mali asili huku akiendelea pia na u-boss wake pale TANAPA.

Hao ndio wenye nchi sasa,wanyonge walie na umaskini wao tu.
Halafu anatoa povu hataki watu wawe na title mbili
 
Magufuli Alikuwa akifundisha shule ya private sio ya serikali hamia private na wewe uwe free ondoka serikalini
Mna propaganda uchwara na za kiboya sana ,Sengerema Sec School ni Private school tangu lini?
 
Magufuli Alikuwa akifundisha shule ya private sio ya serikali hamia private na wewe uwe free ondoka serikalini
Usipotoshe, Sengerema High School ni shule ya umma , na ilijengwa 1964. Rais ana wanafunzi wake ndani ya Baraza la Mawaziri pia idadi ya kutosha ya Wabunge ambao ni wanafunzi wake..
 
Yeye alipokua mwalimu mbona hakuridhika na cheo chake akaenda kugombea ubunge?Ni tamaa au?

Ualimu ni cheo kidogo sana serikalini, hivyo sio tamaa kugombea, ila PS, DPS, RC, RAS, DC, DAS, DED ni tamaa kabisa, na mm najua Mh. Rais akisema hageuki, alisema anawasubiri, uzuri majina yatamfikia, subiri tuone, sbb wameonyesha dharau kubwa sana aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…