Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Ok
 
Viongozi wa dini wenyewe wamekaribisha vituko hivi kwa kukubali kushiriki eti kamati za amani kwa ufadhili wa serikali.
 
Hoja yangu hunaielewa, hoja yangu ni kuwa Mola wako unayemwabudu aliabudiwa katika sinagogi lilojengwa na wakristu. Ima kama wewe waabudu tofauti unijulishe niache kuchangia
Kujenga sio hoja mkuu wangu.

Na pia hili linatoka nje ya mada iliyopo mezani.

Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake akiwa na miaka sita tu aligoma kuingia kwenye nyumba iliyokuwa na sanamu. Leo Luna mdau ananiambia tumuachie alhadi ndio atusemee sisi maamuma tukae tumsikilize tu.

Labda hivyo ndivyo nyinyi wenzetu msio waislam mnavyofundishwa
 
Basi wazikatae hizo pesa tujue
Waislam wanazarauliwa sana 5sizoni, yaani eti hawana elimu hawateuliwi, eti hawana fedha wanatembezewa bakuli makanisani, gwajembe akipita tutaanzia kwake kuigeuza misikiti kuwa sh/jumapili. Maana hawajitambui. Labda Ponda asipoufyata awaamshe huu uchanganyaji dini na siasa
 
Kuna sehemu kwenye Quoran inasema " Rafiki wa muislam ni mkristo" Urafiki katika shida na raha ikiwepo kuchangiana kama ilivyo kwenye Sherehe za harusi.
Ni sehemu gani hiyo?? Niwekee verse number
 
Story za Madaraja watu walisha zichoka
 
CCM walijiaminisha kwa kuwanunua waunga juhudi basi wameua upinzani... Ni kweli wana hali mbaya sana kuliko wakati wowote ule.
 
Nia ya Rais ni kufanya Chamwino iwe na nyumba za ibada nzuri. Ila kwa wenzetu wengine kila kitu ni makosa. Rais waache maana sidhani kama kuujenga msikiti kwa harambee ni dhambi mnayoisimulia. Iweje kujenga kwa kodi za umma sio tatizo?

Sikiliza ndugu yangu!

Ikulu ya nchi kujengwa nyumba za Ibada ni jambo zuri kwa sababu humo ndani ya Ikulu kuna watumishi na wakazi wa Ikulu watahitaji huduma za kiroho.

Lakini Msikiti wa Waislamu ukatafutiwe fedha kanisani?

Unataka Wakiristo baadae wawasimsnge waislamu kila watakapokuja na madai halali ya haki zao kuwa "Nyie acheni kusumbuasumbua, tungekuwa na ubaguzi tungewajengea Msikiti Ikulu?"

Wewe umeona chuo tu cha morogoro ambacho kilijengwa kwa kodi za wote lakini kimekuwa ni kichaka cha kuwasimanga waislamu pindi wakidai usawa na haki nchini kuwa mbona serikali iliwapa chuo cha umma?
 
Nyumba za ibada zinageuzwa kuwa za minada!
Tena mbaya zaidi minada ya maigizo na propaganda za siasa
 
Wewe umeona chuo tu cha morogoro ambacho kilijengwa kwa kodi za wote lakini kimekuwa ni kichaka cha kuwasimanga waislamu pindi wakidai usawa na haki nchini kuwa mbona serikali iliwapa chuo cha umma
Masimango yataisha waislam wakionesha mfano kwa kujenga vyuo vikuu, ila kwasasa tupokee tu. Labda vyuo vijengwe na hicho mnachosimangiawa kirejeshwe kwa serikali
 
Ndugu rais, wewe ni Rais siyo sheikh, wewe ni Mkiristu siyo Muislamu, mambo ya Waislamu waachie Waislamu wenyewe!
Hiyo ni 'sunna' siyo 'faradha', Mkuu. Allah ndiye atakaye muhukumu kwa tendo hili. Ila nina imani. Allah amefurahishwa kwa namna 'watu wa kitabu' wanavyomthamini.

Pole kwa kutolijua hili kabla.
 
Kuna majengo (misikiti) iliharamishwa kuswaliwa bali ilijengwa na waislam (wanafiki) seuze mshirikina? Tupunguzieni maajabu awamu hii wandugu! Mnaona fahari kuvunja recod hata za kutia madoa? Acheni acheni acheni.
 
Magufuli analeta dhana za Church Supremacy nchini, ana portray kuwa waislamu hawawezi kufanya mambo yao wenyewe mpaka huruma ya kanisa!

Ile kitu waislamu wanaita Mfumo Kristo baadhi ya dalili za kukomaa kwake ndiyo hizi!
Sahihi Mfumo Kristo,
Hawatokubali,kusikia,unauongelea
Kwa maana,wamejificha nyuma ya dini kututawala kwani waweza sema waumini wema kumbe hakuna wanazo ajenda zao kisiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…