Chief Kabikula
JF-Expert Member
- Jan 1, 2019
- 7,567
- 9,037
Ndio aende akachangishe pesa za ujenzi wa msikiti kanisani we kilaza?We mtoa post umekosea sana na udini unakusumbua,nataka tu kukukumbusha kwamba Rais ni kiongozi wa nchi na nchi haina dini
Duh...!. Mkuu Rilifu Mirizisika, kwanza pole sana kwa ukidhani nina chuki dhidi ya Uislamu na WaislamuNliwahi kumnukuu Pascal Mayalla humu akionyesha chuki zake dhidi ya uislam na waislam.
PWanabodi,
naomba kutoa Maangalizo muhimu yafuatayo:
1. Tuwe makini sana na watu waliofilisika kiakili ambao watachanganya Uarabu na dini ya Kiislam simply because, Dini ya Kiislamu inatumia lugha ya Kiarabu!. Masikini muflisi hawa, hawajui kuwa hata Ukiristo umeanzia Arabuni. Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mwanae wa kwanza Ismail, aliyezaa na mjakazi wa ki Misri, na Wakristo ni uzao wa Isaka aliyezaa na mkewe Sara. Hata Yesu Kristo, licha ya kuzaliwa Israel, alikulia Misri na alizungumza lugha ya Kiarabu!. Hapa mimi nazungumzia udhalimu wa Waarabu kama jamii na sio dini ya Kiislamu.
Paskali
Mkuu Nguruvi3, naomba nikuhakikishie, zile sio kauli za Askofu Gwajima, zile ni photoshop tuu, siye yeye na hayo hajayasema!.CCM hawana jibu, hawawezi kumkubali Gwajima na kukataa ujumbe wake.
Kauli zimetoka kwenye kinywa cha Gwajima! Zipo mitandaoni zinasomeka, ni chuki tu iliyothibitishwa na CCM
JokaKuu Pascal Mayalla
" Hapo nina maswali mawili matatu ".Ndugu zangu , Amani iwe juu yenu pamekuwepo na madai na majitapo mengi kutoka kwa baadhi ya political laymen tangu jana baada ya baba mwenye nyumba kutembeza bakuli kanisani kuomba fedhwa za kujenga msikiti,
Hapo nina maswali mawili matatu.
Moja, Baba mwenye nyumba alitumwa na masheikh kuwaombea michango kanisani, bila shaka mamlaka za waislamu zitatujulisha.
Pili, Je ni upendo wa baba mwenye nyumba kwa wapangaji wake kutaka kuonesha religious equilibrium katika kipindi hiki cha kutafuta political pasture?, sina hakika sana kama iko hivyo.
Tatu, Ni uumini na uchamungu wa kiwango cha juu cha baba mwenye nyumba?, nadhani hili ni jibu sahihi.
Nne, Ni ipi hukumu ya kisheria katika dini ya uislamu kujenga msikiti kwa fedhwa ambazo yakinani zimetokea kanisani bila wasiwasi wowote?
Hapo maulama watatusaidia
Tano, Je hili halina athari yoyote kisiasa khasa wakati huu wa uchaguzi?
Sita, Ni lini msikt wa mfalme wa Moroko utazinduliwa nao waislamu wachangie kanisa?
Shemeji siku hizi unafokea watu sanaTupe summary, je ni halal au siyo halal?
Muda wa kusoma mapayuko hakuna.
Mkuu usitake kunipa kazi ya kuanza kuisaka ile comment ya chuki na kuileta hapaDuh...!. Mkuu Rilifu Mirizisika, kwanza pole sana kwa ukidhani nina chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu
Hivyo hoja ya kuwachukia Waislamu na Uislamu sio hoja ya kweli.
- Nimesoma TSJ, each room kwenye hostel za TSJ, ni shared watu wawili wawili, nili opt ku share room na Muislamu. Sharing ya TSJ ni by choices and preferences.
- Nimeajiriwa RTD kwenye batch ya watangazaji 10, pale RTD ofisi ilitupangia shared flats kwa kuchaguana, nime opt kushare nyumba na Muislamu for 5 good years tulitengana tulipo oa!.
- During Mwezi Mtukufu wa Ramadan mini nami nilifunga ili kumsindikiza house mate wangu.
- Kwenye ujana maji ya moto, Muslim women were my preference, licha ya kukulia OysterBay na kusomea OysterBay lakini nilikuwa naponea Uswazi, na nikiwa DTV nimeponea sana, mitaa ya Gerezani na Kariakoo.
- Wakati wa uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi, nilipangiwa Zanzibar, nililowea kule nikafa nikaoza kwa binti wa Kiislamu wa Kizanzibari.
- My first wife ni Muislamu na my first born ni Muislamu amefuata dini ya mama yake, almanusura nibadili dini kwa kusilimu!.
Mtu anayeuchukia Uislamu angeweza kupandisha bandiko kama hili?.
Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu, Wakristo, Waislamu, Kuukubali Bila Matatizo!.
Kuahidiwa Mahakama ya Kadhi, kujiunga na OIC kumeleta mshikamano na serikali?
NB. Kitu ambacho baadhi ya watu muflis walinituhumu kuwachukia Waislamu ni kwenye bandiko hili
Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu waliteswa, hasiwa, bakwa, na kuuawa kinyama
Kwenye bandiko hilo nilitoa angalizo hili
P
Shemeji siku hizi unafokea watu sana
Hakuna ubaya kuchangishana kujenga nyumba za ibada,,ili wakazi wa maeneo hayo nao wapate pa kuabudia
Wiaslamu tumechelewa katika hilo.Hatuna jeuri wala ujasiri wa kulikemea hilo leo.Reginald Mengi alifuatwa na akachangia misikiti mingi wakati wa Mwinyi...
Magufuli amekosea sana,anaichangia mijitu ambayo huwa inatukana hata imani yake,mijitu hii huwa inawaita wengine makafiri,usikute hata sasa humo mioyoni Mwao inaziita hizo hela kuwa ni za makafiri.mfalme wetu nae apunguze kutushangaza.Gwajima akiwa rais ataleta surprise kwenye hiyo misikiti
Tulikuwa kimya muda mrefu tukisubiri kama atajibu. Ameulizwa hajajibu wala CCM haijamjibia.Mkuu Nguruvi3, naomba nikuhakikishie, zile sio kauli za Askofu Gwajima, zile ni photoshop tuu, siye yeye na hayo hajayasema!.
Mbona kwenye ule mchango wa kanisa alipokea michango kutoka kwa mashehe waliokuwapo na hakukuwa na malalamiko?Magufuli analeta dhana za Church Supremacy nchini, ana portray kuwa waislamu hawawezi kufanya mambo yao wenyewe mpaka huruma ya kanisa!
Ile kitu waislamu wanaita Mfumo Kristo baadhi ya dalili za kukomaa kwake ndiyo hizi!
Ndugu Rais, wewe ni Rais siyo sheikh, wewe ni Mkiristu siyo Muislamu, mambo ya Waislamu waachie Waislamu wenyewe!
Una haki ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matendo ya imani yako lakini huna haki ya kusimama ndani ya nyumba ya imani yako kudictate kipi kifanywe kwa niaba ya watu wa imani nyingine.
Waislamu wana taratibu zao za kujenga nyumba za Ibada zao, wanachangia wao wenyewe au wanatafuta mfadhili wa imani yao wao wenyewe, au wanafanya kwa kufuata taratibu za dini yao, kisha wanajenga msikiti wao!
Umewahi kusikia wapi Waislamu nchini wameendesha harambee makanisani kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kujenga misikiti yao? Au unafikiri Waislamu hawana marafiki Wakiristo wakiwemo maaskofu na mapadre ambao wangeweza kuwaomba wawafanyie harambee wajenge hizo nyumba?
Au lini umewahi kusikia maaskofu na mapadre wameomba michango kupitia misikitini ili Waislamu wachangie ujenzi wa makanisa?
Kuna mambo ni boundary ya kuheshimiana kiimani, nayo ni kutokuingiliana katika namna kila imani inavyoendesha mambo yake!
Najua pengine kibinadamu uliona aibu kutokana na mihela mirefu unayoimwaga makanisani siku hizi kwa jina la sadaka, ukahisi labda umma wa Waislamu utakuona kama mtu anayetumia mafungu yale ya urais yasiyokaguliwa na yeyote kwa ajili ya sadaka hizo, mimi nasema usihofu, maadamu wewe ni Mkatoliki na Mkiristu basi usiuonee haya Ukiristo wako wewe toa tu, Waislamu wanajiweza, wanaweza kujenga misikiti yao wao wenyewe na infact misikiti nchi hii ni mingi kwelikweli na imejengwa na Waislamu wao wenyewe!
Kuhusu misikiti iliyojengwa na Wafalme na marais, hiyo Waislamu tunajua huwa wanatafuta hao wafadhili wao wenyewe, ila sasa kwa kuwa Kiprotokali jambo linalofanywa na mfalme au rais wa Taifa moja katika jingine lazima mfalme au rais wa taifa husika awe na taarifa ndiyo maana taasisi za dini zinaweza kukujulisha ili usaidie kunyoosha mambo! Hii ni tofauti na kwenda kanisani ukaanzisha harambee ya kujenga misikiti! Ndugu Rais ulitumwa au kuombwa na Muislamu gani kutaka kujenga msikiti kupitia fedha za kanisani?
Wakati mwingine naangalia haya mambo na kuona kuwa yamekaa kisiasa. Hata hivyo mambo ya dini ni sensitive sana si vizuri kuchanganya dini na siasa! Mwalimu alionya sana kuhusu mambo haya!
Ipo namna mtu asiye muislamu anavyoweza kuguswa na kuamua kujenga msikiti, kwa mfano, Mwalimu aliguswa moyoni mwake baada ya kustaafu uraisi akaamua kutafuta fedha za kujenga Msikiti Butiama, Mwalimu alikuwa na connection za Vatican, Makanisa makubwa makubwa lakini hakwenda kutafuta fedha makanisani ili ajenge msikiti, Mwalimu alikwenda kwa Ghadafi ndiye aliyempa pesa za kujenga Msikiti huko Butiama!
Nimkumbushe tu ndugu Magufuli kuwa, dini ya Kiislamu pia imeweka misingi ya aina gani ya misikiti inafaa kuswaliwa ndani yake, Quran inasema ile misikiti iliyojengwa kwa dhamira safi ndiyo misikiti ya Mungu na ndiyo inayofaa kuswaliwa bali ile iliyojengwa kwa dhamira isiyo njema, yenye malengomalengo fulani hivi hiyo haina baraka za Mungu na haifai kuswaliwa ndani yake!
Nashauri Ndugu Rais awe makini sana na haya mambo ya dini, haya ni mazito sana, akiyakosea yataiweka heshima nzima ya taasisi ya urais rehani halafu kuja kurekebisha taswira hiyo inaweza kutumia gharama kubwa.
MAMBO YA WAISLAMU WAACHIWE WAISLAMU WENYEWE. NDUGU RAIS FANYA YALE YA IMANI YAKO AU YALE UTAKAYOOMBWA UFANYE KAMA UKIPENDA!