Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Nliwahi kumnukuu Pascal Mayalla humu akionyesha chuki zake dhidi ya uislam na waislam.
Duh...!. Mkuu Rilifu Mirizisika, kwanza pole sana kwa ukidhani nina chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu
  1. Nimesoma TSJ, each room kwenye hostel za TSJ, ni shared watu wawili wawili, nili opt ku share room na Muislamu. Sharing ya TSJ ni by choices and preferences.
  2. Nimeajiriwa RTD kwenye batch ya watangazaji 10, pale RTD ofisi ilitupangia shared flats kwa kuchaguana, nime opt kushare nyumba na Muislamu for 5 good years tulitengana tulipo oa!.
  3. During Mwezi Mtukufu wa Ramadan mini nami nilifunga ili kumsindikiza house mate wangu.
  4. Kwenye ujana maji ya moto, Muslim women were my preference, licha ya kukulia OysterBay na kusomea OysterBay lakini nilikuwa naponea Uswazi, na nikiwa DTV nimeponea sana, mitaa ya Gerezani na Kariakoo.
  5. Wakati wa uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi, nilipangiwa Zanzibar, nililowea kule nikafa nikaoza kwa binti wa Kiislamu wa Kizanzibari.
  6. My first wife ni Muislamu na my first born ni Muislamu amefuata dini ya mama yake, almanusura nibadili dini kwa kusilimu!.
Hivyo hoja ya kuwachukia Waislamu na Uislamu sio hoja ya kweli.
Mtu anayeuchukia Uislamu angeweza kupandisha bandiko kama hili?.
Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu, Wakristo, Waislamu, Kuukubali Bila Matatizo!.

Kuahidiwa Mahakama ya Kadhi, kujiunga na OIC kumeleta mshikamano na serikali?

NB. Kitu ambacho baadhi ya watu muflis walinituhumu kuwachukia Waislamu ni kwenye bandiko hili
Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu waliteswa, hasiwa, bakwa, na kuuawa kinyama
Kwenye bandiko hilo nilitoa angalizo hili
Wanabodi,
naomba kutoa Maangalizo muhimu yafuatayo:

1. Tuwe makini sana na watu waliofilisika kiakili ambao watachanganya Uarabu na dini ya Kiislam simply because, Dini ya Kiislamu inatumia lugha ya Kiarabu!. Masikini muflisi hawa, hawajui kuwa hata Ukiristo umeanzia Arabuni. Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mwanae wa kwanza Ismail, aliyezaa na mjakazi wa ki Misri, na Wakristo ni uzao wa Isaka aliyezaa na mkewe Sara. Hata Yesu Kristo, licha ya kuzaliwa Israel, alikulia Misri na alizungumza lugha ya Kiarabu!. Hapa mimi nazungumzia udhalimu wa Waarabu kama jamii na sio dini ya Kiislamu.
Paskali
P
 
CCM hawana jibu, hawawezi kumkubali Gwajima na kukataa ujumbe wake.
Kauli zimetoka kwenye kinywa cha Gwajima! Zipo mitandaoni zinasomeka, ni chuki tu iliyothibitishwa na CCM
JokaKuu Pascal Mayalla
Mkuu Nguruvi3, naomba nikuhakikishie, zile sio kauli za Askofu Gwajima, zile ni photoshop tuu, siye yeye na hayo hajayasema!.

P
 
UFAFANUZI KUHUSU MCHANGO WA FEDHA ULIOCHANGISHWA NA MH. RAIS KANISANI KWA AJILI YA UPANUZI WA MSIKITI.

MIMI NI MUISLAAM, NINAYEIFAHAMU DINI YANGU VIZURI KIASI KWA KUKAA DARASANI KUISOMA...

Awali ya yote ninaomba kwanza TUJITAHIDI KUEPUKA KUZUNGUMZIA MAMBO YANAYOHUSU DINI YA KIISLAAM BILA UFAHAMU SAHIHI WA DINI HII, hata kama wewe ni Muislaam inabidi uisome kwanza ndio uongee...VIVYO VIVYO KWA WASIO WAISLAAM UKIZUNGUMZIA SIASA BASI ZUNGUMZIA SIASA LAKINI KWENYE MASUALA YA DINI YA KIISLAAM NYAMAZA, kama kuna mtu ni Muislaam anatumia Uislaam kufanya UOVU wowote waziwazi DEAL NAE YEYE KAMA YEYE, WALA DINI YAKE HAIHUSIKI NA UOVU WAKE...

Pili, nitazungumzia Kadhia hii kadri Allah atakavyoniwezesha kwa lugha nyepesi ili kila mtu aweze kuelewa na kuiomba jamii kuepuka kulopoka mambo juu ya Uislaam bila ELIMU...HIVYO SITOWEKA NUKUU KUTOKA KWENYE KITABU(QURAN) NA SUNNA(HADITH) ILI TU KUIRAHISISHA NA KUGENERALIZE ILA UKITAKA NUKUU TUTAPEANA KWENYE COMMENT INSHAA ALLAH...

KATIKA MOJA YA MISINGI YA UISLAAM...

1. Kuomba omba katika dini ya kiislaam Ni jambo lisilopendeza, japo inaruhusiwa ukiwa huna namna ILA USIFANYE NDIO KAWAIDA YAKO AU NDIO NJIA YA KUJIPATIA KIPATO(Hili linakupunguzia Iman na mapenzi kwa Allah)...ILA KUJIZUIA KUOMBA NDIO JAMBO AMBALO ALLAH ANALIPENDA...HAIJALISHI UNAYEMUOMBA NI MUISLAAM AU SIO...ILA KUOMBA OMBA HAIPENDEZI KATIKA DINI.

Swali: Vipi tutasaidiana au kujua wahitaji endapo hawatoomba?
Jibu: Uislaam umeweka mfumo ambao Mwenye nia ya kusaidia atamjua Mhitaji bila hata ya kuomba...ila ukiwa BAHILI HUWEZI MJUA MHITAJI UTASUBIRIA UOMBWE, NA UBAHILI KWENYE DINI NI DHAMBI(HARAMU)...NI MCHAMUNGU TU NA MWENYE NIA YA KUSAIDIA NDIYE ANAWEZA MTAFUTA MHITAJI BILA KUOMBWA...

2. UISLAAM UNAPOAMRISHA JAMBO LIFANYWE AU LIACHWE BASI UJUE NI KWA FAIDA YETU WENYEWE BINADAMU...

HIVYO UISLAAM UNAAMRISHA UTIIFU KWAKE YEYE ALLAH KWANZA, KWA MANABII NA MITUME WAKE, WANAWACHUONI WA DINI...

VILE VILE UTIIFU WA WATOTO KWA WAZAZI WAO, WAKE KWA WAUME ZAO, NA WATU KWA VIONGOZI WAO...(Isipokuwa kwenye Maasi ya Kumuasi Allah)...

Kwahiyo ni AMRI YA UISLAAM KWA WAISLAAM KUWATII VIONGOZI WAO HATA WAWE MADHAALIMU KIASI GANI(Wajibu wetu ni Kumtii KIONGOZI awe MUISLAAM AU LA, AKIWA MDHULUMISHI haki yetu sisi ni Kusubiri kuwa wavumilivu, ILA SIO KUTOKA NJE YA UTIIFU KWA VIONGOZI).

TANBIHI 1: NI U. T. I. I. F. U. Sio Kujipendekeza.

TANBIHI 2: UTIIFU HUU SIO KWENYE KUMUASI ALLAH, NA hata kama akikuamrisha kwenye Kumuasi Allah kuna taratibu za kufuata vile vile ili tu USITOKE KWENYE TWAA YA KIONGOZI...

3. NI HARAMU NA HAIFAI KWA ASIYEKUWA MUISLAAM KUFANYA HARAKATI ZOZOTE ZILE KUUENDELEZA MSIKITI(Na hii ni kwa Msikiti tu, ila BAINA YA WATU KUSAIDIANA WENYEWE KWA WENYEWE INAFAA ILA MSIKITI TU HAIFAI HATA Mfano;- HAIFAI Mkristo hata kufagia MSIKITINI...

Ila kusaidiana baina ya MKRISTO NA MUISLAAM INAFAA (Isipokuwa tu kwenye Kumuasi Allah).

Mfano;- Mkristo akimpa pesa Muislaam inaruhusiwa kupokea na kuzitumia kwa mahitaji yako, na wala si kazi yako kujua amezipataje...ila ukiwa unafahamu wazi bila shaka MKRISTO HUYU ANAYENIPA PESA, PESA HII AMEIPATA KATIKA NJIA YA HARAMU KATIKA SHERIA YA DINI BASI HAIFAI KUPOKEA...

4. UISLAAM UNATUHITAJI WAISLAAM TUISHI NA WASIOKUWA WAISLAAM KWA WEMA NA KUWATENDEA UADILIFU KAMA VILE VILE TUNAVYOPASWA KUTENDEANA WENYEWE KWA WENYEWE(WAISLAAM)...KATIKA JAMII TUNAZOISHI KWA MCHANGANYIKO IKIWA WASIOKUWA WAISLAAM HAWATUPIGI VITA WALA KUTUZUIA KUTEKELEZA IBADA ZETU ZA LAZIMA...NI WAJIBU KUISHI NA KUAMILIANA KWA WEMA NA UADILIFU...

UKIMDHULUMU ASIYEKUWA MUISLAAM UTAPATA DHAMBI ILE ILE UNGEMDHULUMU MUISLAAM MWENZAKO...TUTENDEANE WEMA NA UADILIFU...

Hayo yanatosha kwa sasa...

Turudi kwenye KADHIA, Kuna mambo yafuatayo kuyajadili:
1. Shida na mahitaji ya WAISLAAM kwenye msikiti wao wanaijua wao wenyewe, HIVYO mpaka imfikie mtu wa nje tena asiyekuwa Muislaam basi kuna mtu kampelekea...

2. Rais sio mjinga apitishe mchango wa upanuzi wa msikiti kama hakupelekewa maombi ya msaada na wahusika...

3. RAIS HANA KOSA KABISA KWA DINI YAKE NA UTARATIBU WAKE KAMA MWANASIASA NI SAHIHI KABISA ALILOFANYA...

4. HATA WALE WAKRISTO WALICHANGIA MULE IWE KWA HIARI AU KISHINGO UPANDE WALA WASILAUMIWE...

5. WAKULAUMIWA WALIOPELEKA MAOMBI YA MSAADA...WANASIHIWE TU KUWA WARIDHIKE NA KUTOSHEKA NA WALICHONACHO...WAACHE TAMAA...WASITAFUTE KUJIFANANISHA NA WASIOKUWA WAISLAAM...

Turudi kwenye Kadhia;
Hela zimepatikana tuzifanyie nini?

@ Kama WALITUMA MAOMBI YA MSAADA HUO BASI HAKUNA NAMNA ZAIDI YA KUZIRUDISHA AU KUOMBA KUBADILI MATUMIZI BADALA KUTUMIA MSIKITI, LAKINI KUZITUMIA KWA DHUMUNI KUSUDIWA LA KWA AJILI YA MSIKITI BASI MJUE MNAENDELEA KUCHUMA DHAMBI...ila wahusika RUDINI KWA MOLA WENU MJITATHMINI MTUBU DHAMBI KUBWA MNO...ACHENI TAMAA...

@ Na kama hawakuomba msaada, basi waielekeze ile pesa pahala pengine na si MSIKITINI KABISA...

ILA KUNA WATU WAMEJIINGIZA KWENYE DINI KUWA VIONGOZI ILA HAWAIJUI DINI YAO...

ALLAH ATUONGOZE...

ALLAH NI MJUZI ZAIDI...

Ahsanteni sana...
 
Ndugu zangu , Amani iwe juu yenu pamekuwepo na madai na majitapo mengi kutoka kwa baadhi ya political laymen tangu jana baada ya baba mwenye nyumba kutembeza bakuli kanisani kuomba fedhwa za kujenga msikiti,

Hapo nina maswali mawili matatu.

Moja, Baba mwenye nyumba alitumwa na masheikh kuwaombea michango kanisani, bila shaka mamlaka za waislamu zitatujulisha.

Pili, Je ni upendo wa baba mwenye nyumba kwa wapangaji wake kutaka kuonesha religious equilibrium katika kipindi hiki cha kutafuta political pasture?, sina hakika sana kama iko hivyo.

Tatu, Ni uumini na uchamungu wa kiwango cha juu cha baba mwenye nyumba?, nadhani hili ni jibu sahihi.

Nne, Ni ipi hukumu ya kisheria katika dini ya uislamu kujenga msikiti kwa fedhwa ambazo yakinani zimetokea kanisani bila wasiwasi wowote?

Hapo maulama watatusaidia

Tano, Je hili halina athari yoyote kisiasa khasa wakati huu wa uchaguzi?

Sita, Ni lini msikt wa mfalme wa Moroko utazinduliwa nao waislamu wachangie kanisa?
" Hapo nina maswali mawili matatu ".
Nami naomba nijibu mawili matatu kwa uwelewa wangu.

Swali namba 1.
Jibu ni kwamba, inawezekana hakutumwa ila inawezekana aliombwa kusaidia. Mara nyingi mambo kama haya yanafanywa na kikundi cha waislamu wanaojiita BAKWATA, na kwa mtazamo wangu kikundi hiki hakina tofauti na tawi la ccm.

Swali namba 2.
Jibu ni kwamba, hakuna upendo wa aina hii katika jambo la kiimani. Kwa sababu kila imani lazima ina sheria na taratibu zake. Hivyo huu sio upendo bali ni unafiki kwa malengo ya kujinufahisha kisiasa.

Swali namba 3.
Jibu ni kwamba, hakuna uchamungu wa aina hiyo zaidi ya unafiki. Kwa sababu imani moja wapo ndani ya ukristo ni kuamini kwamba ALLAH sio mungu wa kweli na uislamu sio dini ya mungu. Na imani moja wapo ndani ya uislamu nikuamini kwamba misikiti ni nyumba za ALLAH kwa ajili yakuabudiwa yeye tu. Sasa ucha mungu unapatikanaje unapotumia nyumba ya ibada kwa imani yako ili kuhimarisha imani nyingine unayo pingana nayo?

Swali namba 4.
Jibu ni kwamba, kwa mujibu wa sheria haifai na kilicho fanyika ni kosa ndani ya uislamu. Kwa sababu sheria ya uislamu ni Qur - aan na hadithi za mtume.
Na Qur - aan sura ya 9 (surat tauba) inasema hivi:
(Aya ya 17) Washirikina hawawezi kuistawisha misikiti ya ALLAH hali wanajishuhudia ukafiri.

(Aya ya 18) Anayestawisha misikiti ya ALLAH ni yeye tu amuaminiye ALLAH na siku ya mwisho, na kusimamisha swala na kutoa zakah na hamwogopi yeyote ila ALLAH.

Swali namba 5.
Jibu ni kwamba, Kwa kuwa ni kipindi cha kuelekea uchaguzi maoni yangu ni kwamba haikuwa sahihi kufanyika jambo hili hasa ukizingatia mwenye kulifanya hili ni mmoja kati ya wagombea. Hivyo kwangu mimi naona ni moja wapo ya hadaa/rushwa ili kujinufaisha kisiasa katika uchaguzi unaokaribia. Kwa maana hiyo lina athari kubwa zote kidini na kisiasa.
 
Mizigo na vifungo vya dini ndo Kama hii!....

Kila Jambo waja hupinga !

Jema ni lipi?

Msaidiwe maneno
Msiposaidiwa lawama !

Mpewe fungu lipi?

Ebu mnipe mm basi hizo pesa !!
 
Duh...!. Mkuu Rilifu Mirizisika, kwanza pole sana kwa ukidhani nina chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu
  1. Nimesoma TSJ, each room kwenye hostel za TSJ, ni shared watu wawili wawili, nili opt ku share room na Muislamu. Sharing ya TSJ ni by choices and preferences.
  2. Nimeajiriwa RTD kwenye batch ya watangazaji 10, pale RTD ofisi ilitupangia shared flats kwa kuchaguana, nime opt kushare nyumba na Muislamu for 5 good years tulitengana tulipo oa!.
  3. During Mwezi Mtukufu wa Ramadan mini nami nilifunga ili kumsindikiza house mate wangu.
  4. Kwenye ujana maji ya moto, Muslim women were my preference, licha ya kukulia OysterBay na kusomea OysterBay lakini nilikuwa naponea Uswazi, na nikiwa DTV nimeponea sana, mitaa ya Gerezani na Kariakoo.
  5. Wakati wa uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi, nilipangiwa Zanzibar, nililowea kule nikafa nikaoza kwa binti wa Kiislamu wa Kizanzibari.
  6. My first wife ni Muislamu na my first born ni Muislamu amefuata dini ya mama yake, almanusura nibadili dini kwa kusilimu!.
Hivyo hoja ya kuwachukia Waislamu na Uislamu sio hoja ya kweli.
Mtu anayeuchukia Uislamu angeweza kupandisha bandiko kama hili?.
Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu, Wakristo, Waislamu, Kuukubali Bila Matatizo!.

Kuahidiwa Mahakama ya Kadhi, kujiunga na OIC kumeleta mshikamano na serikali?

NB. Kitu ambacho baadhi ya watu muflis walinituhumu kuwachukia Waislamu ni kwenye bandiko hili
Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu waliteswa, hasiwa, bakwa, na kuuawa kinyama
Kwenye bandiko hilo nilitoa angalizo hili

P
Mkuu usitake kunipa kazi ya kuanza kuisaka ile comment ya chuki na kuileta hapa
 
Hv nyie waislam mnajionaga nyie ni spesheli sana. Sasa nawambia hv, ombenj sana Mungu, mimi nisje kuwa raisi wa JmT.
Raisi ni mkuu wa nchi, anayo haki za msingi kuunganisha watu.
 
Hakuna ubaya kuchangishana kujenga nyumba za ibada,,ili wakazi wa maeneo hayo nao wapate pa kuabudia

Nasemaha mara nyingi sana. Kuna mjijtu wanatamani kusikia Tanzania ni dola ya kiislam au imekuwa kama msumbiji nk. Hili tendo ni tendo la amani kabisa. Tena very pure. Raisi asipofanya ishara hizi wangemwita shetani, asiyemjua Mungu.
 
Wiaslamu tumechelewa katika hilo.Hatuna jeuri wala ujasiri wa kulikemea hilo leo.Reginald Mengi alifuatwa na akachangia misikiti mingi wakati wa Mwinyi...

Bro, naheshimu maoni yako. Lakni naona waislam wengi wanaweka dini mbele sana bila utu, ubinadamu, na nchi.

Hebu kwa criterions alizotumia huyu mtoa mada, je Diamond anafaa kutoa pesa za msikiti?

Kuna watu wanagapi pes wanazo haramu wamejenga misikiti na makanisa.

Kosa la raisi hapa ni lipi? Unajua muda mwingine ni bora kuwa na watu wachache kuliko wengi wajinga. Kudos to you my brethren brother.
 
Magufuli amekosea sana,anaichangia mijitu ambayo huwa inatukana hata imani yake,mijitu hii huwa inawaita wengine makafiri,usikute hata sasa humo mioyoni Mwao inaziita hizo hela kuwa ni za makafiri.mfalme wetu nae apunguze kutushangaza.Gwajima akiwa rais ataleta surprise kwenye hiyo misikiti

Tatizo JPM ni raisi wa wote hata wale washenzi na magaidi katika hao bado kuna watz wema. Hawa wengine wanataka kusikia misikiti inatoka urabuni huko na bakheresa ndio roho zao zinasuuzika
 
Mnaogopa kuchangiwa pesa za mbuzi katoliki haaa,

Mengi ni kama aliwahi jenga misikiti kwani hamuitumii.

Msiogope bana hawawezi kubadili madrasa kuwa nyumba za Sunday school, ni misemo tu haiwezi tokea.
 
Mkuu Nguruvi3, naomba nikuhakikishie, zile sio kauli za Askofu Gwajima, zile ni photoshop tuu, siye yeye na hayo hajayasema!.
Tulikuwa kimya muda mrefu tukisubiri kama atajibu. Ameulizwa hajajibu wala CCM haijamjibia.
Hata hivyo, zile clip kama ile ya Uislam Ulaya haiwezi kuwa Photoshop hata kidogo.

Ni hivi jamaa kayasema, hana ujasiri wa kusimama na kuyakanusha na wala CCM haina ujasiri huo

Kwasasa Sheikh Ponda ataongea tu, ukimgusa utaulizwa na Gwajima je!
 
Hizi ni hasira zisizokuwa na maana yoyote. Jengo la msikiti siyo msikiti wenyewe. Msikiti ni jengo na watu wanaolitumia; watu wakiacha kulitumia likageuzwa kuwa danguro, linakuwa siyo msikiti tena.

Kuna mifano mingi sana ya majengo ya msikiti yaliyoachwa, na jinsi gani majengo ambayo hayakuwa misikiti yalivyokuwatransfromed kuwa misikiti. Unatakliwa ulalamikekie jengo ambalo linatumiwa kwa ibada, siyo jenga ambalo linatayarishwa kutumika kwa ibada.

Video hii chini inaonyesha hafla iliyofanyika karibu mwaka mmoja uliopita kujenga jengo la msikiti huko Chato; mbona huikulalamikiwa? Hasa pale kuanzia pale dakika ya 41?



Mwaka 1987 Nyerere alijenga jengo la msikiti pale Butiama na kuwa mlezi wa kamati ya kuendeleza jengo lile lle hadi wakati kifo kinamkuta mbona pia hakukuwa na malalamiko ya namna hii. Jengo la msikiti ni jengo tu, msikiti wenyewe ni watu wanaolitumia jengo hilo? Pale chuo Kikuu cha Dar es Salaama kuna jengo la masjidi lililojengwa na serikali kwa msaada wa serikali ya Israle mbona hata Profesa Malima na Dr. Bilali walikuwa wanalitumia?
 
Magufuli analeta dhana za Church Supremacy nchini, ana portray kuwa waislamu hawawezi kufanya mambo yao wenyewe mpaka huruma ya kanisa!

Ile kitu waislamu wanaita Mfumo Kristo baadhi ya dalili za kukomaa kwake ndiyo hizi!
Mbona kwenye ule mchango wa kanisa alipokea michango kutoka kwa mashehe waliokuwapo na hakukuwa na malalamiko?

Badala ya kutumia matukio kama haya kuwasogeza waislamu na wakristo pamoja wewe una filosofi ya kuwa wakristo na waislamu hawazi kushirikiana hata siku moja. Hizo ni filosofi mbovu ambazo ndizo zilzoleta ugaidi wa akina al-qaida, al-shabab na ugaidi mwingine wa aina hiyo sehemu mbalimbali za dunia. Ni filosofi zilizojengwa kwa msingi wa mashindano ya kidini badala ya kuwavuta watu kuwa karibu na mungu wao.

Kwako wewe matukio kama haya hapa yatakuwa yanakuudhi sana

1598320764869.png



1598320926603.png
 
Photosho="Pascal Mayalla, post: 36463792, member: 17813"]
Mkuu Nguruvi3, naomba nikuhakikishie, zile sio kauli za Askofu Gwajima, zile ni photoshop tuu, siye yeye na hayo hajayasema!.

P
[/QUOTE]
Photoshop ya visual niliona video yenye audio
 
Ndugu Rais, wewe ni Rais siyo sheikh, wewe ni Mkiristu siyo Muislamu, mambo ya Waislamu waachie Waislamu wenyewe!

Una haki ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matendo ya imani yako lakini huna haki ya kusimama ndani ya nyumba ya imani yako kudictate kipi kifanywe kwa niaba ya watu wa imani nyingine.

Waislamu wana taratibu zao za kujenga nyumba za Ibada zao, wanachangia wao wenyewe au wanatafuta mfadhili wa imani yao wao wenyewe, au wanafanya kwa kufuata taratibu za dini yao, kisha wanajenga msikiti wao!

Umewahi kusikia wapi Waislamu nchini wameendesha harambee makanisani kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kujenga misikiti yao? Au unafikiri Waislamu hawana marafiki Wakiristo wakiwemo maaskofu na mapadre ambao wangeweza kuwaomba wawafanyie harambee wajenge hizo nyumba?

Au lini umewahi kusikia maaskofu na mapadre wameomba michango kupitia misikitini ili Waislamu wachangie ujenzi wa makanisa?

Kuna mambo ni boundary ya kuheshimiana kiimani, nayo ni kutokuingiliana katika namna kila imani inavyoendesha mambo yake!

Najua pengine kibinadamu uliona aibu kutokana na mihela mirefu unayoimwaga makanisani siku hizi kwa jina la sadaka, ukahisi labda umma wa Waislamu utakuona kama mtu anayetumia mafungu yale ya urais yasiyokaguliwa na yeyote kwa ajili ya sadaka hizo, mimi nasema usihofu, maadamu wewe ni Mkatoliki na Mkiristu basi usiuonee haya Ukiristo wako wewe toa tu, Waislamu wanajiweza, wanaweza kujenga misikiti yao wao wenyewe na infact misikiti nchi hii ni mingi kwelikweli na imejengwa na Waislamu wao wenyewe!

Kuhusu misikiti iliyojengwa na Wafalme na marais, hiyo Waislamu tunajua huwa wanatafuta hao wafadhili wao wenyewe, ila sasa kwa kuwa Kiprotokali jambo linalofanywa na mfalme au rais wa Taifa moja katika jingine lazima mfalme au rais wa taifa husika awe na taarifa ndiyo maana taasisi za dini zinaweza kukujulisha ili usaidie kunyoosha mambo! Hii ni tofauti na kwenda kanisani ukaanzisha harambee ya kujenga misikiti! Ndugu Rais ulitumwa au kuombwa na Muislamu gani kutaka kujenga msikiti kupitia fedha za kanisani?

Wakati mwingine naangalia haya mambo na kuona kuwa yamekaa kisiasa. Hata hivyo mambo ya dini ni sensitive sana si vizuri kuchanganya dini na siasa! Mwalimu alionya sana kuhusu mambo haya!

Ipo namna mtu asiye muislamu anavyoweza kuguswa na kuamua kujenga msikiti, kwa mfano, Mwalimu aliguswa moyoni mwake baada ya kustaafu uraisi akaamua kutafuta fedha za kujenga Msikiti Butiama, Mwalimu alikuwa na connection za Vatican, Makanisa makubwa makubwa lakini hakwenda kutafuta fedha makanisani ili ajenge msikiti, Mwalimu alikwenda kwa Ghadafi ndiye aliyempa pesa za kujenga Msikiti huko Butiama!

Nimkumbushe tu ndugu Magufuli kuwa, dini ya Kiislamu pia imeweka misingi ya aina gani ya misikiti inafaa kuswaliwa ndani yake, Quran inasema ile misikiti iliyojengwa kwa dhamira safi ndiyo misikiti ya Mungu na ndiyo inayofaa kuswaliwa bali ile iliyojengwa kwa dhamira isiyo njema, yenye malengomalengo fulani hivi hiyo haina baraka za Mungu na haifai kuswaliwa ndani yake!

Nashauri Ndugu Rais awe makini sana na haya mambo ya dini, haya ni mazito sana, akiyakosea yataiweka heshima nzima ya taasisi ya urais rehani halafu kuja kurekebisha taswira hiyo inaweza kutumia gharama kubwa.

MAMBO YA WAISLAMU WAACHIWE WAISLAMU WENYEWE. NDUGU RAIS FANYA YALE YA IMANI YAKO AU YALE UTAKAYOOMBWA UFANYE KAMA UKIPENDA!

Waambie wazikatae sasa .. unabwatukia mitandaoni so what? Akili Za kitoto hizi..! Wewe Una Jicho la Kujua Dini Kuliko viongozi wako? Kama Ndivyo Hivyo basi uwe Imam au Sheick mkuu wewe! Acha Kupalilia Mbegu ya Udini wewe!
 
Back
Top Bottom