Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Akimwangalia Lissu mpaka sasa haelewi anapambana na binadamu au mzimu inabidi awe anashinda kwenye kazi za kanisa. Itamtesa sana hii katika maisha yake hapa duniani.
Kuna kipindi itafikia hatua ya kulala kanisani na haitatosha kuna muda utafika itabidi kitanda cha askofu kiwe karibu na chake mpaka pale atakapo tubu kwa kinywa chake kwamba yeye ndiye shetani aliyetuma wasiojulikana kumdhulu Lissu na baada ya hapo atasamehewa ndipo atakuwa huru.
 
Rais Magufuli amehudhuria misa takatifu ya uzinduzi wa Kanisa la parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino jijini Dodoma.

Misa hii inarushwa mubashara TBC na Channel ten.

Maendeleo hayana vyama!
=========

Baba askofu mkuu amewataka waumini kuzusha macho kuuona uzuri wa kanisa na kuwaasa uzuri wa kwanza ni roho hivyo waumini watamani roho zao zipendeze kama kanisa lao, Baba askofu mkuu amemkaribisha Rais Magufuli ili awamegee busara zake.

Rais Magufuli: Matokeo ya ujenzi wa kanisa hili umefanywa na wakristo wote, wakati wa ujenzi kila mmoja alitoa alichokuwa nacho. Nakumbuka katika siku hiyo mama mzee mmoja alitoa 5,000 yote aliyokuwa nayo katika ujenzi wa kanisa hili, ujenzi umefanywa na waumini wote wa kanisa hili.

Nawashukuru wananchi wengine mbalimbali siku hiyo tukitoa mchango hapa nilikuwa napigiwa simu na baadhi ya watu wengine waislamu nakumbuka nilipigiwa na mtu mmoja kutoka Dar es Salaam na akaja kukabidhi milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hili, wadau ni wengi waliojitolea na mimi nawashukuru sana kwa niaba yenu.

Nawashukuru wasimamizi ambao fedha tulizozichanga hawakuzila na shetani alikimbia mbali kuhubiri roho zao kuzila fedha hizi, tunawashukuru wajenzi hawakupoteza muda chini ya uongozi wa mkuu wa JKT na vijana wake, walikuja na kushiriki katika ujenzi huu. Vijana walioshiriki ujenzi huu si wakristo tu, walikuwepo Waislamu wamejenga, Roman, Wasabato, KKKT, Anglingana na waliookoka wamejenga.

Kikosi cha JKT nilichokiomba tukawapa fedha zilizokuwa zimechangwa na ninyi na zimechangwa na wananchi wengi napenda kuwapongeza kwa niaba yenu kwa sababu wamefanya kazi nzuri sana na huu ndio umoja wa watanzania.

Mhasham baba Askofu mkuu ndio maana mimi nilisita sana kuambiwa mimi ndie mfadhili mkuu kwa sababu ninaamini waliofadhili kanisa hili na kushiriki kwa njia moja au nyingine kukamilisha. Nilisita kubeba heshima hiyo ambayo sistahili, mimi nilitoa mapendekezo nikachangia kidogo nilichokua nacho lakini kimechangiwa kingi na wale walioshiriki kwa hiyo pongezi ni kwetu sisi sote.

Nimefurahi kumuona father Kitima, huyu ni rafiki yangu wa siku nyingi. Alikuwa ndio vice chancellor wa St. Augustine, chuo kikuu cha kule Mwanza na baadae akateuliwa kuwa katibu mkuu wa baraza la maaskofu na leo nimefurahi kuja hapa. Yale mengine mengine maviporo viporo yanayobaki kule na kwa kuwa wewe ndie katibu mkuu wa maaskofu wote, hata hili la fence linaweza likakugusagusa kidogo. Ukaangalia angalia yale yanayobaki huko ili utusaidie sisi.

Parokia ya Chamwino ina raha yake, ina upendo mkubwa hata nyimbo mnaona zinavyogusa na uwepo wa Mungu upo, kwa ruhusa yako baba askofu ilikuwa niombe kitu kimoja. Kanisa hili wameshiriki watu wa madhehebu mbalimbali kulijenga na kiukweli mahali ambako ni makao makuu panatakiwa kuzungukwa na watu wanaomtukuza Mungu. Sio wa dhehebu moja bali yote kadri muda utavyokuwa unaenda, makao makuu lazima paende na uwepo wa Mungu.

Kama utaniruhusu, tutumie siku ya leo pia tuchange angalau tuanze kujenga msikiti wa ndugu zetu waislamu ambao msikiti wao ni mdogo nao wapo pale kwa ajili ya kumtukuza Mungu na baadhi ya wasaidizi wangu wengine ni waislamu na nataka niwatajie mmoja tu, kuna Alhaji, ameshaenda kuhiji mpaka Makka lakini ni msaidizi wangu. Ninapoingia humu inabidi lazima aingie humu kanisani lakini inapofika siku ya kwenda kumtukuza Mola wake, nimeambiwa ule msikiti bado haujawa mkubwa vizuri.

Baba Askofu, uniruhusu leo nichukue kikapu ili kama sitachukua muda wako mwingi niwaombe wakristo wenzangu tuanze kuchangie, tutamuomba baba Paroko akaziwasilishe kwa shekhe kwenye msikiti wetu na tutajipanga taratibu namna tutakavyoweza kuukarabati.

Tukimaliza hivyo tutaendelea tena katika kanisa jingine kama ni Anglikana, KKKT, Wasabato ili utukufu wa Chamwino katika kumtukuza Mungu ukasimame.
======

Rais Magufuli amechukua kikapu na mtu wa kwanza kuchangia ni baba Askofu ambae ametoa laki mbili na msaidizi wake ambae ni Alhaji atachangia lakini tatu.

Katibu mkuu wa baraza la maaskofu nae kachangia laki moja na ameeleza amemfahamu Rais tangu mwaka 2001 na alikuwa karibu sana na maaskofu na amemfahamu kupitia kwao hata leo anachokifanya inaonyesha namna gani anawapenda watanzania na amefanya vingi vinavyofanya nchi iende mbele kama rushwa iliyokuwa inaelekea kutushida,a anasema ukipita kila mahali wanasema tupeni sisi Rais Magufuli.

Jumla ya fedha zilizochangwa ni 48,021,000/= Mifuko ya simenti 48 na lori tano za mchanga.
Kweli Rais wetu Ana moyo sana, naona anawakumbuka na upande wa pili

Ova
Screenshot_20200823-112938.jpg

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Mtu yeyote ukitaka kumuua halafu Bahati mbaya ukamkosakosa kila ukimuona lazima uweweseke.
Alie mpiga huyoo jaamaa yenuuu, muuulizeni mwenyewe na dereva wake wanawajua. Maana haiwezekani mtu apigwe risasi kwenye gari aumie mguu wa kuria huku dereva wake akitoka bila mchubuko wowote, huku mkijua magari yote mengi ya Tanzania tunaendeshea mkono wa kushoto, hivyo anae kaa mbe le kama abiria anakua mkono wa kuria wa derevaaaa. Sasa inakuaje apigwe mguu wa kuria? Au siku hiyo yeye ndo alikua dereva?
Halafu baada ya tukio hill jamaa akawa amekidhi kugombea uraisi, yaaniiii kupigwaa kwake yeye iwe ni dhabihu ya kuwa raisi. Hiii haikubariki kabisa. Watanzania sio wajingaaa.
 
Siyo mbaya kwa wenzetu Wakristo kutuchangia, lakini kwa uwelewa wangu finyu nadhani hii haiko sawa. Hawa tunaowaita makafiri watajengaje nyumba yetu ya ibada?

Mh.Rais Magufuli amechangisha fedha za kujenga msikiti huko chamwino Dodoma akiwa katika ibada ya Jumapili leo tarehe 23/8/2020.

Huku mtaani mbona tunachangishwa sana, kuna maeneo kila ijumaa ukipita utakutana na sheikh amebeba daftari na kapu lake anaomba mchango wa kujenga msikiti.
 
Huu wema wa ku act ni fake kwa kadiri ya ufahamu wangu huyu ni chui alevaa ngozi ya kondoo tutampiga kipigo cha mbwa koko kwenye sanduku la kura, asijifanye mwema na akati ni muumiani anaenyonya damu za watz kila uchao amediriki hadi kufuga kundi la wauaji dhidi ya watz wasio na hatia na anawalipa kodi zetu huku akiwabatiza kwa jina la wasiojulikana.
 
Alie mpiga huyoo jaamaa yenuuu, muuulizeni mwenyewe na dereva wake wanawajua. Maana haiwezekani mtu apigwe risasi kwenye gari aumie mguu wa kuria huku dereva wake akitoka bila mchubuko wowote, huku mkijua magari yote mengi ya Tanzania tunaendeshea mkono wa kushoto, hivyo anae kaa mbe le kama abiria anakua mkono wa kuria wa derevaaaa. Sasa inakuaje apigwe mguu wa kuria? Au siku hiyo yeye ndo alikua dereva?
Halafu baada ya tukio hill jamaa akawa amekidhi kugombea uraisi, yaaniiii kupigwaa kwake yeye iwe ni dhabihu ya kuwa raisi. Hiii haikubariki kabisa. Watanzania sio wajingaaa.

Rekebisha kidogo mkuu kwenye hiyo Kuria iwe kulia, pia “abiria anakua mkono wa kuria wa dereva”
 
Alie mpiga huyoo jaamaa yenuuu, muuulizeni mwenyewe na dereva wake wanawajua. Maana haiwezekani mtu apigwe risasi kwenye gari aumie mguu wa kuria huku dereva wake akitoka bila mchubuko wowote, huku mkijua magari yote mengi ya Tanzania tunaendeshea mkono wa kushoto, hivyo anae kaa mbe le kama abiria anakua mkono wa kuria wa derevaaaa. Sasa inakuaje apigwe mguu wa kuria? Au siku hiyo yeye ndo alikua dereva?
Halafu baada ya tukio hill jamaa akawa amekidhi kugombea uraisi, yaaniiii kupigwaa kwake yeye iwe ni dhabihu ya kuwa raisi. Hiii haikubariki kabisa. Watanzania sio wajingaaa.
Huu ni mwanzo tu itafikia utakuja kutuambia ulisimama upande upi wa wakati wa kushuti na bashite pekee alikupa mafao ya tsh ngapi na kisha kamongo wa burigi akakupa ngapi muuaji mkubwa weye
 
Nhisi raisi hajui taratibuza waislamu.
Labda bakwata wamempa muongozo wa aina ya uislamu wao .
lakini nijuavyo mimi Misikiti hujengwa na Waislamu Tuu kwa nia ya Kuamuabudu ALlah, kitu ambacho ni ibada kuujenga kwake.
Qur-an suratu ya 9- Tawba

aya ya :-
17. Haiwi kuwa makafiri ndio waamirishe misikiti ya Mwenyezi Mungu, hali wanajishuhudishia wenyewe ukafiri. Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika, na katika Moto watadumu.

18. Hakika wanao amirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na wakashika Sala, na wakatoa Zaka, na wala hawamchi(hawaabudu) ila Mwenyezi Mungu (pekeyake asiye na mtoto wala mshirika). Basi huenda hao wakawa katika waongofu.

29. Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa walio pewa Kitabu(wakiristo na mayahudi), mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wamet'ii

Kwa aya izo hapo juu inaonesha wazi kuwa Muislamu hatakiwi kuchukua msaada wowote kutoka kwa wasiokuwa waislamu ili kujenga nyumba za Mungu, Msikiti huoo utakuwa Ghirara- (nyumba ya ibada ya wanafiki).

Kama Magu angelikuwa anawpenda waislamu angeliwatowa Mashekh Jela.
 
Alie mpiga huyoo jaamaa yenuuu, muuulizeni mwenyewe na dereva wake wanawajua. Maana haiwezekani mtu apigwe risasi kwenye gari aumie mguu wa kuria huku dereva wake akitoka bila mchubuko wowote, huku mkijua magari yote mengi ya Tanzania tunaendeshea mkono wa kushoto, hivyo anae kaa mbe le kama abiria anakua mkono wa kuria wa derevaaaa. Sasa inakuaje apigwe mguu wa kuria? Au siku hiyo yeye ndo alikua dereva?
Halafu baada ya tukio hill jamaa akawa amekidhi kugombea uraisi, yaaniiii kupigwaa kwake yeye iwe ni dhabihu ya kuwa raisi. Hiii haikubariki kabisa. Watanzania sio wajingaaa.
Wewe ni afisa upelelezi wa serikali au unaongea kwa sababu una mahaba na ccm?
 
Kuna kipindi itafikia hatua ya kulala kanisani na haitatosha kuna muda utafika itabidi kitanda cha askofu kiwe karibu na chake mpaka pale atakapo tubu kwa kinywa chake kwamba yeye ndiye shetani aliyetuma wasiojulikana kumdhulu Lissu na baada ya hapo atasamehewa ndipo atakuwa huru.
Kweli kabisa
 
Hasa kitendo cha kutaka kumua kitamtesa sana. Ndio maana anaomba aombewe kila siku. Kuna dhambi ambazo zinatesa sana.
Akimwangalia Lissu mpaka sasa haelewi anapambana na binadamu au mzimu inabidi awe anashinda kwenye kazi za kanisa na misikiti. Itamtesa sana hii katika maisha yake hapa duniani.
 
Bila shaka hatakuwa na ujasiri wa kumpa mkono.
Nahisi siku akikutanishwa na Lissu anaweza akatimua mbio aisee! Maana hataamini kama ni Lissu yule yule aliyeshambuliwa kule Dodoma mchana kweupe wakati ule, au ni mzimu.
 
Back
Top Bottom