Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Ndugu rais, wewe ni Rais siyo sheikh, wewe ni Mkiristu siyo Muislamu, mambo ya Waislamu waachie Waislamu wenyewe!

Una haki ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matendo ya imani yako lakini huna haki ya kusimama ndani ya nyumba ya imani yako kudictate kipi kifanywe kwa niaba ya watu wa imani nyingine.

Waislamu wana taratibu zao za kujenga nyumba za Ibada zao, wanachangia wao wenyewe au wanatafuta mfadhili wa imani yao wao wenyewe, au wanafanya kwa kufuata taratibu za dini yao, kisha wanajenga msikiti wao!

Umewahi kusikia wapi Waislamu nchini wameendesha harambee makanisani kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kujenga misikiti yao? Au unafikiri Waislamu hawana marafiki Wakiristo wakiwemo maaskofu na mapadre ambao wangeweza kuwaomba wawafanyie harambee wajenge hizo nyumba?

Au lini umewahi kusikia maaskofu na mapadre wameomba michango kupitia misikitini ili Waislamu wachangie ujenzi wa makanisa?

Kuna mambo ni boundary ya kuheshimiana kiimani, nayo ni kutokuingiliana katika namna kila imani inavyoendesha mambo yake!

Najua pengine kibinadamu uliona aibu kutokana na mihela mirefu unayoimwaga makanisani siku hizi kwa jina la sadaka, ukahisi labda umma wa Waislamu utakuona kama mtu anayetumia mafungu yale ya urais yasiyokaguliwa na yeyote kwa ajili ya sadaka hizo, mimi nasema usihofu, maadamu wewe ni Mkatoliki na Mkiristu basi usiuonee haya Ukiristo wako wewe toa tu, Waislamu wanajiweza, wanaweza kujenga misikiti yao wao wenyewe na infact misikiti nchi hii ni mingi kwelikweli na imejengwa na Waislamu wao wenyewe!

Kuhusu misikiti iliyojengwa na Wafalme na marais, hiyo Waislamu tunajua huwa wanatafuta hao wafadhili wao wenyewe, ila sasa kwa kuwa Kiprotokali jambo linalofanywa na mfalme au rais wa Taifa moja katika jingine lazima mfalme au rais wa taifa husika awe na taarifa ndiyo maana taasisi za dini zinaweza kukujulisha ili usaidie kunyoosha mambo! Hii ni tofauti na kwenda kanisani ukaanzisha harambee ya kujenga misikiti! Ndugu Rais ulitumwa au kuombwa na Muislamu gani kutaka kujenga msikiti kupitia fedha za kanisani?

Wakati mwingine naangalia haya mambo na kuona kuwa yamekaa kisiasa. Hata hivyo mambo ya dini ni sensitive sana si vizuri kuchanganya dini na siasa! Mwalimu alionya sana kuhusu mambo haya!

Ipo namna mtu asiye muislamu anavyoweza kuguswa na kuamua kujenga msikiti, kwa mfano, Mwalimu aliguswa moyoni mwake baada ya kustaafu uraisi akaamua kutafuta fedha za kujenga Msikiti Butiama, Mwalimu alikuwa na connection za Vatican, Makanisa makubwa makubwa lakini hakwenda kutafuta fedha makanisani ili ajenge msikiti, Mwalimu alikwenda kwa Ghadafi ndiye aliyempa pesa za kujenga Msikiti huko Butiama!

Nimkumbushe tu ndugu Magufuli kuwa, dini ya Kiislamu pia imeweka misingi ya aina gani ya misikiti inafaa kuswaliwa ndani yake, Quran inasema ile misikiti iliyojengwa kwa dhamira safi ndiyo misikiti ya Mungu na ndiyo inayofaa kuswaliwa bali ile iliyojengwa kwa dhamira isiyo njema, yenye malengomalengo fulani hivi hiyo haina baraka za Mungu na haifai kuswaliwa ndani yake!

Nashauri Ndugu Rais awe makini sana na haya mambo ya dini, haya ni mazito sana, akiyakosea yataiweka heshima nzima ya taasisi ya urais rehani halafu kuja kurekebisha taswira hiyo inaweza kutumia gharama kubwa.

MAMBO YA WAISLAMU WAACHIWE WAISLAMU WENYEWE. NDUGU RAIS FANYA YALE YA IMANI YAKO AU YALE UTAKAYOOMBWA UFANYE KAMA UKIPENDA!
Natamani ausome huu waraka umeandika fact tupu
 
Hiyo ni 'sunna' siyo 'faradha', Mkuu. Allah ndiye atakaye muhukumu kwa tendo hili. Ila nina imani. Allah amefurahishwa kwa namna 'watu wa kitabu' wanavyomthamini.

Pole kwa kutolijua hili kabla.
Watu wa kitabu??? Hahahahaahahahahaha

Ahlul kitaab ni watu wa zaburi (ya kweli), injili (ya kweli) na tauraat (ya kweli).

Sio watu wa biblia mkuu hahahahaahahahhah
 
Kuna majengo (misikiti) iliharamishwa kuswaliwa bali ilijengwa na waislam (wanafiki) seuze mshirikina? Tupunguzieni maajabu awamu hii wandugu! Mnaona fahari kuvunja recod hata za kutia madoa? Acheni acheni acheni.
Haswaaa
 
We mtoa post umekosea sana na udini unakusumbua,nataka tu kukukumbusha kwamba Rais ni kiongozi wa nchi na nchi haina dini
Rais anaruhusuliwa kuchangia dini yeyote kadri atakavyojisikia .shida ni sehemu aliyotumia kuchangia hiyo pesa .huwezi kusimama Kwenye madhabahu alafu eti ukanzisha harambee yakuwachangia waislamu.sio sawa kabisa.Angekuwa anazo zakumtosha alitakiwa aombe kwa Paroko kuwa ibada ikiisha anaomba waongozane mpk hapo kwa Jirani anataka kufanya harambee kidogo nae Jirani akue. Lkn so kama alvyo fanya kuchangisha ndani ya kanisa tena madhabahuni.
 
Someni ufunuo sura ya Tisa panahistotia ya kiunabii kuhusu uislamu na ukatoriki(jihad and crusade) dini hizi mbili ni mahasimu wa muda mrefu na historia iliyowazi sana.kwa kilchofanyika Islamic wa zamani wasingekubari kabisa,hawa was Leo wanshida sehemu
 
Uko sahihi, hata Dar aliwaombea kwa Mfalme wa Morocco wajengewe msikiti wa kisasa. Na tayari umekamilika!
Wiaslamu tumechelewa katika hilo.Hatuna jeuri wala ujasiri wa kulikemea hilo leo.Reginald Mengi alifuatwa na akachangia misikiti mingi wakati wa Mwinyi.Juzi Kigoma Diamond Platinum,mwanamuziki (haramu katika Uislamu,Mzinzi (kwa ushahidi wa kuwa na watoto nje ya ndoa)kajenga msikiti n akaukabidhi huku akiambatana na kimada.
Hospitali za Misheni zinatibia watu wote bila kubagua.
Kwa hili,msimlaumu JPM amefanya kile kilichomsukuma kukifanya.
Waislamu tujitafakari.
 
Mohamed Said nimemsoma mara kadhaa humu jamnvini. Ni kweli amekuwa akituhumu sana kuwa Tanzania kuna mfumo kristo. Suleiman Takadir nimemgoogle sasa hivi na kwa kweli historia yake imenihuzunisha sana.
Lakini sijaona chochote hapo kinachohusu wakatoliki kuwachukia waislam na waislam kuwachukia wakatoliki/wakristo.
Katika jamii outliers huwa hawakosekani. Lakini outliers hawafanyi jamii nzima ya waislam kuwachukia wakatoliki au jamii nzima ya wakrtisto kuwachukia waislam.
Tukiwa objective unaweza kukuta kuna waislam wengi saaana wanamapenzi makubwa sana kwa wakristo na wakristo wengi sana wana mapenzi makubwa sana kwa waislam.
Mkuu,

Unaonekana ni mtu wa maana sana. Sina uhakika na hilo. But yeah at least unaonekana ni mtu!

Unajua mimi sijasema kwamba huu mchukiano ni two way traffic, kaa yupo anaesema hivyo aje atoe hoja zake.

Mimi ninachosema historia ya nchi yetu ni kwamba wakristo hususan wakatoliki wamekuwa wakiwachukia waislam (historically) na labda niseme hili ni tatizo la kimfumo zaidi kuliko individuals maana sote tunaishi vizuri kwa nje.

Hoja ikaja kwamba, aliyoyafanya Mheshimiwa rais magufuli ndio yanapingwa hapa na mimi nikafikia kuelezea kwamba hakutokuwa kamwe na mapenzi hayo ambayo yeye Mheshimiwa rais ametaka kuya portray kwa sababu chuki kutoka kwao (wakristo hususan wakatoliki) kwa uislam au waislam ni kubwa zaidi kuliko mapenzi yao.

Hebu imagine tu brother, katika umri wako na pengine kwa elimu yako eti Leo ndio Unamjua Sheikh Suleiman Takadir?? Sikulaumu mkuu ni mfumo ndio uliopelekea hivyo. Kwa hiyo lililofanyika ni geresha tu au danganya toto na wala si kwa mapenzi ya dhati ya wakristo juu ya uislam. Ukweli ni ule aliousema GWAJIMA juu ya miskiti, kwamba ataugeuza kuwa Sunday schools ile ni chuki ya hali ya juu na yale ni machache tu aliyoyasema ambayo kwa chuki ilimvyomjaa alishindwa kuendelea kukaa nayo moyoni.

Allah anatuambia kwamba ubaya wao (makafiri) waudhihirishao dhidi yetu (waislam) ni mdogo mno ukilinganisha na ule waufichao vifuani mwao.

Ukweli ni ule wa waziri lukuvi juu ya kauli anazozitoa kuhusu Zanzibar na mengine mengi mno mno mno mno.

Kwa hiyo ndugu yangu kimfumo, huu upendo kamwe hautokuwepo. Ile kuchangisha pesa ni geresha tu au nyinyi mnaita siasa tu.
 
Ungekuwa humpingi JPM kila siku. Pengine ningesoma. Naomba kuuliza kabla ya kuandika. Ulifikiria Kama. Mwislamu au kama mpinzani wa JPM. Fuatilia miaka 5 hii ya JPM na waislamu. Una akili ndogo sana. Duniani Kuna watu wana nia njema. Usiasa wa kijinga unakufanya upoteze hata akili yako. Unakuwa mtumwa wa chuki Zako.
Ndani ya miaka 5 hii ndio wahadhiri wakuu na waandamizi na baadhi ya wafanyakazi wa UDOM waliondolewa wote wakiwa ni waislam (kwa chuki za kidini) na kuwa replaced na wote waliokuwa sio waislam (kwa maslahi ya kidini).

Una hoja?
 
Ukiwa kanisani,mtaani au huko msikitini?
Hahaha usichotaka ni nini, pesa yangu au dhehebu langu au kanisa ninalo sali?
Mbona tunapoombwa michango sisi hatujali kiivyo, nyie mna mind nini sasa?!

Jijengeeni misikiti na ofisi zenu msiombe ombe.
 
Nimesoma hadi mwisho sijaruka kipengele chochote, japo sikujua kinachoendelea lakini umeelezea vizuri nikapata mwanga,

Binafsi nakazia kwa msumari yote uliyoyaandika, Dini isichanganywe na Siasa.
Hilo linafanyiwa kazi kwa upinzani lkn ccm kwao ni ruksa kuchanganya
 
Back
Top Bottom