Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Toa ushahid, ucongee tu kwa matamanio ni sura gani na aya ya ngap imeruhusu hilo?
Unaonekana so muislam umedandia tu hoja ili kukidhi kiu yako ya kisiasa
Uislam inaruhusu kujengewa msikiti na asie muislam au hata kupewa pesa za kujengewa msikiti
Msikiti wameombewa waislam,wewe kinakuuma Nini?
 
Ndugu rais, wewe ni Rais siyo sheikh, wewe ni Mkiristu siyo Muislamu, mambo ya Waislamu waachie Waislamu wenyewe!

Una haki ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matendo ya imani yako lakini huna haki ya kusimama ndani ya nyumba ya imani yako kudictate kipi kifanywe kwa niaba ya watu wa imani nyingine.

Waislamu wana taratibu zao za kujenga nyumba za Ibada zao, wanachangia wao wenyewe au wanatafuta mfadhili wa imani yao wao wenyewe, au wanafanya kwa kufuata taratibu za dini yao, kisha wanajenga msikiti wao!

Umewahi kusikia wapi Waislamu nchini wameendesha harambee makanisani kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kujenga misikiti yao? Au unafikiri Waislamu hawana marafiki Wakiristo wakiwemo maaskofu na mapadre ambao wangeweza kuwaomba wawafanyie harambee wajenge hizo nyumba?

Au lini umewahi kusikia maaskofu na mapadre wameomba michango kupitia misikitini ili Waislamu wachangie ujenzi wa makanisa?

Kuna mambo ni boundary ya kuheshimiana kiimani, nayo ni kutokuingiliana katika namna kila imani inavyoendesha mambo yake!

Najua pengine kibinadamu uliona aibu kutokana na mihela mirefu unayoimwaga makanisani siku hizi kwa jina la sadaka, ukahisi labda umma wa Waislamu utakuona kama mtu anayetumia mafungu yale ya urais yasiyokaguliwa na yeyote kwa ajili ya sadaka hizo, mimi nasema usihofu, maadamu wewe ni Mkatoliki na Mkiristu basi usiuonee haya Ukiristo wako wewe toa tu, Waislamu wanajiweza, wanaweza kujenga misikiti yao wao wenyewe na infact misikiti nchi hii ni mingi kwelikweli na imejengwa na Waislamu wao wenyewe!

Kuhusu misikiti iliyojengwa na Wafalme na marais, hiyo Waislamu tunajua huwa wanatafuta hao wafadhili wao wenyewe, ila sasa kwa kuwa Kiprotokali jambo linalofanywa na mfalme au rais wa Taifa moja katika jingine lazima mfalme au rais wa taifa husika awe na taarifa ndiyo maana taasisi za dini zinaweza kukujulisha ili usaidie kunyoosha mambo! Hii ni tofauti na kwenda kanisani ukaanzisha harambee ya kujenga misikiti! Ndugu Rais ulitumwa au kuombwa na Muislamu gani kutaka kujenga msikiti kupitia fedha za kanisani?

Wakati mwingine naangalia haya mambo na kuona kuwa yamekaa kisiasa. Hata hivyo mambo ya dini ni sensitive sana si vizuri kuchanganya dini na siasa! Mwalimu alionya sana kuhusu mambo haya!

Ipo namna mtu asiye muislamu anavyoweza kuguswa na kuamua kujenga msikiti, kwa mfano, Mwalimu aliguswa moyoni mwake baada ya kustaafu uraisi akaamua kutafuta fedha za kujenga Msikiti Butiama, Mwalimu alikuwa na connection za Vatican, Makanisa makubwa makubwa lakini hakwenda kutafuta fedha makanisani ili ajenge msikiti, Mwalimu alikwenda kwa Ghadafi ndiye aliyempa pesa za kujenga Msikiti huko Butiama!

Nimkumbushe tu ndugu Magufuli kuwa, dini ya Kiislamu pia imeweka misingi ya aina gani ya misikiti inafaa kuswaliwa ndani yake, Quran inasema ile misikiti iliyojengwa kwa dhamira safi ndiyo misikiti ya Mungu na ndiyo inayofaa kuswaliwa bali ile iliyojengwa kwa dhamira isiyo njema, yenye malengomalengo fulani hivi hiyo haina baraka za Mungu na haifai kuswaliwa ndani yake!

Nashauri Ndugu Rais awe makini sana na haya mambo ya dini, haya ni mazito sana, akiyakosea yataiweka heshima nzima ya taasisi ya urais rehani halafu kuja kurekebisha taswira hiyo inaweza kutumia gharama kubwa.

MAMBO YA WAISLAMU WAACHIWE WAISLAMU WENYEWE. NDUGU RAIS FANYA YALE YA IMANI YAKO AU YALE UTAKAYOOMBWA UFANYE KAMA UKIPENDA!
[/QUOTE Je wewe wamekutuma uje uwasemee hapa?
 
Hizo michango angechangisha Tundu Lisu hii mada ingekua vise versa
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri asipoelewa hapa sidhani kama kuna mahali ataweza kuelewa. Hilo hela alizochangisha bora akazichukue an kizipelela mahali pengine. Nimehisi kifedheheshwa sana na hili tukio.
 
JPM kawashika pabaya hadi siku ya uchaguzi mtakonda tu!
 
Hivi Rais Magufuli anajua kuwa kwa Waislam, mathalani muislam akawa ameoa mke ambaye siyo muislam, ikifika wakati wa mfungo, mwanaume yule hawezi kufuturu chakula kilichoandaliwa na yule mke ambaye siyo muislam?


Hichi kitu umepata wapi???
 
Hakuna ubaya kuchangishana kujenga nyumba za ibada,,ili wakazi wa maeneo hayo nao wapate pa kuabudia
Shule na uhuru halisi wa kuabudu ni muhimu zaidi kuliko nyumba za ibada.
Nyumba nyingi za ibada zina migogoro kuliko utumishi maana wengi si ucha Mungu unaowaongoza bali uchatumbo na uchavyeo...
 
Msikilize Mufti, au ww unajua uislam kuliko Mufti.? Ww sio msemaji wa Waislam, hivyo sio mtu sahihi kuzungumzia ya waislam hata kidogo.

Mh. Rais Magufuli, songa mbele, supporter wako tuko wengi zaidi ya wanao kupinga, na Mh. Rais nikutie moyo, hata Yesu alikataliwa na binadamu hawa hawa, hivyo hata utende wema kiwango gani bado wako watakao kupinga tu. Hivyo usikate tamaa hata kidogo.









Wivu utawamaliza jamani, Mh. Rais hakuanza jana au juzi kusaidia ujenzi wa misikiti au makanisa...

Mbona hajawahi kwenda msikitini kuomba waislamu watoe sadaka ya kuchangia ujenzi wa kanisa?
 
Kingine sina Hakika kama Mungu wa waislamu ndo Mungu wa Wakristo.

Hapa mtu unaweza ukajikuta unachuma dhambi bila kujua.

Sisi wakristo tunajua Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu. Siwezi kuchangia ujenzi wa msikiti au ujenzi wa shaulin temple ili Mungu mwingine aka abudiwe. Kwa imani yangu iyo ni dhambi.
Aisee, umeongea kitu kikubwa sana na cha mantiki kubwa! Wakristo wanaamini Mungu wa Kiislam ni wa kweli? Je, waislam wanaamini Mumgu wa Kikristo ni wa kweli? Dah point kubwa sana! Sijui wangapi wameona hii madini!
 
Mahusiano mazuri ya nchi yetu na nchi nyingine awamu zilizopita ziliwafanya waislam wapate misaada mikubwa sana toka kwenye nchi zenye Waumini wa Kiislamu na kujenga misikiti nchi nzima.

Awamu hii nafikiri misaada toka kwa nchi marafiki wa imani ya kiislam imepungua sana na ujenzi wa misikiti haukufanyika kwa kiwango cha awamu zilizopita.
Kwa hiyo ni sawa kwa mkuu kuwaliwaza wahanga wa awamu yake kama anavyofanya kila anapopita kumwaga pesa kwa watu bila kufanya kazi.
Yani kama jackpot bingo.
Hapa pesa tu.
 
Unaonekana so muislam umedandia tu hoja ili kukidhi kiu yako ya kisiasa
Uislam inaruhusu kujengewa msikiti na asie muislam au hata kupewa pesa za kujengewa msikiti
Msikiti wameombewa waislam,wewe kinakuuma Nini?
Waambie hao muft kabombey hawana walijualo
 
Ni kweli mkuu,
Mbona huku mitaani watoto wa madrasa wanatupitishia sana madaftari ya michango tunachangia fresh tu. Kwa nini wasichangishane dini moja tu.

Mambo mengine ni kuvunga tu.
Na jana nimechanga Mkatoliki mie [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom