Rais Magufuli anazungumza na watanzania kupitia mkutano wake na wananchi wa Dar es salaam.
Tukio liko mubashara katika runinga zote
Updates;
Waziri Bashungwa: Nimesimama hapa mheshimiwa Rais kukushukuru sana kabla ya mkutano huu wa hadhara umetupa heshima ya kuzindua Magic FM Radio pamoja na Uhuru FM pamoja na TV ya channel 10, Mheshimiwa Rais tunakushukuru sana kwa heshima hiyo ya kutuzindulia vyombo hivi vya habari
Nitumie nafasi hii kuwashukuru sana chama changu cha mapinduzi kwa uwekezaji huu mzuri ambao utatoa ajira, utawahabarisha watanzania, tunawapongeza sana.
Vyama vingine hapa nchini tumeona vikiwekeza kwenye kuwa vibaraka wa nchi fulani, kwenye majungu, kejeli na matusi lakini chama cha mapinduzi kinawekeza katika maendeleo ya watu na kutengeneza ajira, hongereni sana chama cha mapinduzi.
=======
Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inastahili kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, na haijapendelewa. Ameongeza kuwa, hata katika mapato wanaongoza.
Amesema Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambayo jana ilipandishwa hadhi na kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar pamoja na Naibu Meya wanastahili kuwa Mameya wa Jiji hilo.
Ameeleza, "Najua watu walikuwa wanatazama nafasi hiyo, wengine wakiwa wamejipanga kugombea. Hakuna cha kugombea wewe ndio Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam"
===
Katika Mkutano wa Hadhara wa Rais Magufuli uliofanyika Mnazi Mmoja Dar es Salaam. Rais ametoa wito kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuwa waaminifu katika kazi zao.
Amesema kuna watumishi huwa wanawakadiria wafanyabishara kodi kubwa sana na wanaposhindwa kulipa basi hutaka kugawana kile kiasi kidogo ambacho mfanyabiashara anakuwa nacho.
Amewataka TRA wajifunze kutoa haki kwa wafanyabishara ambao wanania ya kulipa kodi. Amesema TRA kuna wafanyakazi wala rushwa, hivyo ni lazima wajirekebishe.
Ameiambia Wizara ya Fedha kuwa wakasimamie suala hilo, kwa kuwa nchi inahitaji kodi, inahitaji ushuru lakini uwe wa haki.