Rais Magufuli azungumza na Wananchi wa Ubungo wakati aliporejea jijini Dar es salaam akitokea Mkoani Dodoma

Rais Magufuli azungumza na Wananchi wa Ubungo wakati aliporejea jijini Dar es salaam akitokea Mkoani Dodoma

Magufuli hongera kwa kumpa mlemavu pesa. Tunaomba uwape basi wastaafu wa ATCL pesa zao za pension maana PSSSF wanasema hujapeleka za ATCL.. Mbona hawa wazee wanapigwa dana dana na wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Mara pesa zitatoka Hazina mara ATCL mara hazija tolewa na wizara ya Fedha.
Raisi wa wanyonge wasaidie hawa wazee. Kama tunavyo muimbea mzazi wake Mungu amponye vivyo hivyo tuna muomba Mungu akupe maono uwalipe hawa wazee wastaafu wa ATCL.
Wafanyakazi kadi za mifuko ya jamii mnazo muwe mnahakiki wenyewe kama michango imeenda mbona mifuko ikitoa kadi zao waweza hakiki mtandaoni tu bila kwenda ofisi zao na ukaprint statement? Kama mwajiri hajapeleka mkomalie mapema usisubiri hadi ustaafu uanze ohhh Raisi tusaidie!!! Kuna mabaraza ya wafanyakazi,vyama vya wafanyakazi nk hata kibinafsi komaa na mwajiri apeleke michango kabla kustaafu ili usisumbue raisi
 
Hivi Rais anaweza akakaa mkoani Dodoma akajihisi ni Rais kamili wa nchi?
Dar ni habari nyingine...
 
Hahah ndio muda wenyewe huu,wanyonge(bodaboda,mamantilie,walemavu,wamachinga) mtanyenyekewa sana tu kipindi hiki cha kampeni

Kuleni maisha arifu.
Mku mbona huyu mwamba miaka yote mitano yupo na vijana wake hao wamachinga,BodA BofA,mama ntilie na walemavu!au ndo umerudi nchini hivi karbuni
 
Hapa hatuzungumzii kadi za uwanachama wa mifuko ya jamii. Tunazungumzia wateule wa raisi kushindwa kupeleka makato na vyama vya wafanyakazi kuto pata ushirikiano kutoka kwa wa ajiri. Ndio sababu hili suala limefika hapo. Usiingizize siasa na hamnazo kwenye kuhitaji haki ambayo hata mahakama imeiona. Kama suala hulifahamu kaa kimya sio lazima uandike. Una bahati kama katika familia yako au wazazi wako hawa kuteseka kutokana na masuala ya pension.
 
Kwani mkuu ana raba pea moja hiyohiyo pamoja na jaketi moja tu...???
Wasaidizi wake, ebu oneni aibu basi...[emoji23][emoji23]
Angevaa nyingine mwingine angesema jamaa anatumia hela za wananchi vibaya
 
Dah umati wa Ubongo leo watu kama utitiri, yaani fly over ilifurika balaa, JPM atapata over 95% ya vote aisee..

This pic will go viral worldwide, JPM mtu wa watu duh

IMG-20200619-WA0009.jpg
 
Wahusika, kuelekea kipindi cha kampeni, hizo bunduki na ma-combat yapunguzeni sasa.
kiongozi wetu ni mpendwa sana, sasa hayo mabunduki yanaonesha picha nyingine kabisa.
naamini ulinzi unaweza fanyika vingine. Ni ushauri tuu.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Ubungo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili wakati akitokea Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mama mwenye Ulemavu wa miguu Nyangoma James kuhusu changamoto ya Usafiri wa Bajaji aliyokuwa akiomba kupewa ili imsaidie kuendesha familia yake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Nyangoma James Mama mwenye Ulemavu wa miguu msaada wa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya kununulia Bajaji ili imsaidie kuendesha Maisha yake. Pia Rais Dkt. Magufuli aliendesha Mchango kwa Wananchi wengine ambapo waliahidi kumchangia mama huyo kiasi cha Shilingi Milioni 3.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mama mwenye Ulemavu wa miguu Nyangoma James mara baada ya kumchangia kiasi cha Shilingi Milioni 5. kushoto aliyekaa ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makore

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama mwenye Ulemavu wa miguu Nyangoma James mara baada ya kumchangia kiasi cha Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ununuzi wa Bajaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza Wimbo wa hamasa pamoja na Wananchi wa Ubungo mara baada ya kuwahutubia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika eneo la Ubungo Darajani mara baada ya kuzungumza na Wananchi.


PICHA NA IKULU

1592582207724.png



Touching and very special.
 
Back
Top Bottom