Rais Magufuli azungumza na Wananchi wa Ubungo wakati aliporejea jijini Dar es salaam akitokea Mkoani Dodoma

Rais Magufuli azungumza na Wananchi wa Ubungo wakati aliporejea jijini Dar es salaam akitokea Mkoani Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Ubungo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili wakati akitokea Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mama mwenye Ulemavu wa miguu Nyangoma James kuhusu changamoto ya Usafiri wa Bajaji aliyokuwa akiomba kupewa ili imsaidie kuendesha familia yake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Nyangoma James Mama mwenye Ulemavu wa miguu msaada wa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya kununulia Bajaji ili imsaidie kuendesha Maisha yake. Pia Rais Dkt. Magufuli aliendesha Mchango kwa Wananchi wengine ambapo waliahidi kumchangia mama huyo kiasi cha Shilingi Milioni 3.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mama mwenye Ulemavu wa miguu Nyangoma James mara baada ya kumchangia kiasi cha Shilingi Milioni 5. kushoto aliyekaa ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makore

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama mwenye Ulemavu wa miguu Nyangoma James mara baada ya kumchangia kiasi cha Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ununuzi wa Bajaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza Wimbo wa hamasa pamoja na Wananchi wa Ubungo mara baada ya kuwahutubia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika eneo la Ubungo Darajani mara baada ya kuzungumza na Wananchi.

PICHA NA IKULU

Huyu ni mtu asiyejiamini, myaka mitano yote anafanya kampeni peke yake na bado hajaridhika
 
Komedi shoo zimeanza...

Hakuna waliojivua magwanda na kuvaa magamba?? 😀

Everyday is Saturday...........................😎
 
Kwa watu wanaofikiria kwa urefu wa pua zao,kwa watu wanaofikiria kesho nitakula nini na hafikirii kesho kutwa na mtondogoo,watu wa aina hiyo Magufuli ni yesu.ila kwa wale wanaofikiria kesho,kesho kutwa na mtondogoo,kwa watu wanaofikiria zaidi ya chakula,magu siyo rais
Sasa umeandika nini na wewe? Kwahiyo hao raia wote wa ubungo ni wewe tu ndio mwenye akili?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Sasa umeandika nini na wewe? Kwahiyo hao raia wote wa ubungo ni wewe tu ndio mwenye akili?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
Mkuu usitishwe na wingi.nchi hii Ina watu 55 milioni Ila walipakodi hawafiki milioni tatu according to Magu,Sasa wewe hapo unaelewa nini? Lakini pia umeambiwa ni watu wa stendi ya ubungo,madereva,makonda na wapiga debe Sasa hapo unauliza akili!
 
Ushindi wa kimbunga au maigizo ya kimbunga!

Lini mliwahi kushinda uchaguzi halali? Bila polisi na tume yenu ya uchaguzi nyinyi ni wepesi sana. Na uzuri mnafahamu fika tumeshawachoka kitambo.
Miaka yote CCM inashinda!
 
Mkuu usitishwe na wingi.nchi hii Ina watu 55 milioni Ila walipakodi hawafiki milioni tatu according to Magu,Sasa wewe hapo unaelewa nini? Lakini pia umeambiwa ni watu wa stendi ya ubungo,madereva,makonda na wapiga debe Sasa hapo unauliza akili!
Nenda wewe na Mwenyekiti wako wa maisha tuone kama utapata umati huo!!?
 
Mbona Mwenyekiti wako wa maisha Mbowe humsemi udikiteta wake?

Tafuta popote ninaposupport Mbowe kuwa kiongozi wa cdm zaidi ya miaka kumi. Na sio Mbowe tu, tafuta popote ninapounga mkono kiongozi yoyote kukaa madarakani zaidi ya 10yrs, ukipapata uje tuendelee na mjadala.
 
Ushindi wa kimbunga au maigizo ya kimbunga!

Lini mliwahi kushinda uchaguzi halali? Bila polisi na tume yenu ya uchaguzi nyinyi ni wepesi sana. Na uzuri mnafahamu fika tumeshawachoka kitambo.
Sasa si uwambie viongozi wako msishiriki uchaguzi?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom