Rais Magufuli azungumza na Wananchi wa Ubungo wakati aliporejea jijini Dar es salaam akitokea Mkoani Dodoma

Wafanyakazi kadi za mifuko ya jamii mnazo muwe mnahakiki wenyewe kama michango imeenda mbona mifuko ikitoa kadi zao waweza hakiki mtandaoni tu bila kwenda ofisi zao na ukaprint statement? Kama mwajiri hajapeleka mkomalie mapema usisubiri hadi ustaafu uanze ohhh Raisi tusaidie!!! Kuna mabaraza ya wafanyakazi,vyama vya wafanyakazi nk hata kibinafsi komaa na mwajiri apeleke michango kabla kustaafu ili usisumbue raisi
 
Hivi Rais anaweza akakaa mkoani Dodoma akajihisi ni Rais kamili wa nchi?
Dar ni habari nyingine...
 
Hahah ndio muda wenyewe huu,wanyonge(bodaboda,mamantilie,walemavu,wamachinga) mtanyenyekewa sana tu kipindi hiki cha kampeni

Kuleni maisha arifu.
Mku mbona huyu mwamba miaka yote mitano yupo na vijana wake hao wamachinga,BodA BofA,mama ntilie na walemavu!au ndo umerudi nchini hivi karbuni
 
Hapa hatuzungumzii kadi za uwanachama wa mifuko ya jamii. Tunazungumzia wateule wa raisi kushindwa kupeleka makato na vyama vya wafanyakazi kuto pata ushirikiano kutoka kwa wa ajiri. Ndio sababu hili suala limefika hapo. Usiingizize siasa na hamnazo kwenye kuhitaji haki ambayo hata mahakama imeiona. Kama suala hulifahamu kaa kimya sio lazima uandike. Una bahati kama katika familia yako au wazazi wako hawa kuteseka kutokana na masuala ya pension.
 
Hivi ni Rais au ni mgombea urais?
 
Kwani mkuu ana raba pea moja hiyohiyo pamoja na jaketi moja tu...???
Wasaidizi wake, ebu oneni aibu basi...[emoji23][emoji23]
Angevaa nyingine mwingine angesema jamaa anatumia hela za wananchi vibaya
 
Dah umati wa Ubongo leo watu kama utitiri, yaani fly over ilifurika balaa, JPM atapata over 95% ya vote aisee..

This pic will go viral worldwide, JPM mtu wa watu duh

 
Wahusika, kuelekea kipindi cha kampeni, hizo bunduki na ma-combat yapunguzeni sasa.
kiongozi wetu ni mpendwa sana, sasa hayo mabunduki yanaonesha picha nyingine kabisa.
naamini ulinzi unaweza fanyika vingine. Ni ushauri tuu.
 

PICHA NA IKULU




Touching and very special.
 
Ni pesa za Watumishi wa Umma hizo alizo wadhulumu tangu mwaka 2016 kwa kisingizio cha uhakiki. Naamini atazirudisha tu zote mara baada ya kutoka madarakani. Jasho la mtu halipotei kirahisi tu.
Acha uongo wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…