Rais Magufuli: Baada ya siku 60 Bodi za Mashirika yasiyotoa gawio zijivunje zenyewe

Rais Magufuli: Baada ya siku 60 Bodi za Mashirika yasiyotoa gawio zijivunje zenyewe

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Rais Magufuli atoa siku 60 kwa Taasisi na Kampuni zenye hisa za Serikali zipatazo 187 ambazo hazikutoa gawio lake Serikalini leo, kufanya hivyo kwa Waziri mwenye dhamana vinginevyo Menejimenti na Bodi zake zivunjwe zenyewe kwa kundika barua

Amesema, “Hapa ni Mashirika 79 tu ndio yametoa gawio, hao wengine kila siku wanasema wanapata hasara lakini wana magari na vingine. Mashirika 187 hayana habari ya kuchangia, lakini wana Bodi na kuna Viongozi uko wanasafiri, wanastarehe na wanalipana posho”

Aidha, amebainisha ”Yapo Mashirika ambayo mishahara yao inalipwa na Serikali, wamepewa hadi nyumba lakini hawajaleta gawio ungekuwa wewe Rais ungefanyaje? Ukute wengine wamelala Hotelini sasa hivi wanatuangalia kwenye TV”

Ameongeza, ”Baada ya miezi miwili (siku 60) Taasisi ambazo hazijatoa gawio basi Ma-CEO wa Taasisi hizo wajihesabu hawapo. Wewe kila siku unapata hasara lakini magari mnanunua si muuze hayo magari mtoe gawio?”

Amesisitiza, “Haya Mashirika kila siku yanasema yanapata hasara si tuyavunje tu? Hayana faida. Hata nyumbani kila siku ukishindwa kuleta hata kisamvu Mkeo anakufukuza na atakunyima ugali, saa nyingine atakunyima vyote mpaka mboga. Nimesema atakunyima vyote mpaka mboga.”

Rais amugiza Waziri wa Fedha Dkt. Mpango

Rais Magufuli alisema: "Sasa Waziri (Dk.Mpango) tumebembelezana sana haiwezekani kukaa na viongozi na bodi za aina hii ambapo tunazungumza hawataki kuelewa na fedha zetu za serikali zinateketea kule never."

"Waandike barua Mwenyekiti kama ni wa kuteuliwa na mimi maana yake siku hiyo sio mwenyekiti tena, kama ameteuliwa na mwingine wajivunje wenyewe bodi isiwapo, Mkurugenzi naye ajihesabu hayupo, wapo wanaolipwa mishahara Sh. milioni 15 kwa mwezi, halafu hakuna gawio hata senti tano why? hufai kuwapo," alisema.

Naye, Waziri Mpango alisema asilimia 70 ya bajeti ya serikali inategemea makusanyo ya ndani na nusu ya makusanyo yasiyo ya kodi yanatokana na gawio na michango kutoka kwa kampuni, taasisi, wakala na mashirika ya umma.

Alisema wanaendelea kufanyia kazi mashirika yanayojiendesha kwa hasara na kwamba mwaka ujao hakutakuwa na hadithi ya mashirika hayo.

Rais awaagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Msajili wa Hazina

"Sasa hawa wengine wenye viburi hivi ni nani? Katibu Mkuu na Msajili baada ya siku 60 ambaye hataleta gawio lolote ajihesabu hayupo, kila siku wewe unapata hasara, lakini za kula na kununua gari unazo si uache basi kununua gari utoe gawio,"alisisitiza.

Awali, Msajili wa Hazina, Dk. Athuman Mbuttuka, alisema mashirika na kampuni 81 za kibiashara kati yao 40 yameshindwa kutoa gawio kutokana na kujiendesha kwa hasara.

============

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 24 Novemba, 2019 amepokea kiasi cha shilingi Trilioni 1.05 zinazotokana na gawio na michango kutoka taasisi, mashirika ya umma na kampuni ambazo Serikali ina hisa.

Hafla ya kupokea gawio na michango hiyo imefanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mabalozi, Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC), viongozi wa Dini na viongozi wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Dkt. Binilith Mahenge.

Katika taarifa yake Msajili wa Hazina Bw. Athuman Mbuttuka amesema fedha za gawio na michango iliyowasilishwa leo kwa Mhe. Rais Magufuli ni ya mwaka wa fedha wa 2018/19 na imetoka katika taasisi, mashirika ya umma na kampuni 79 kati ya taasisi, mashirika ya umma na kampuni zote 266 ambazo Serikali imewekeza mitaji, na kwamba kiasi hicho kimeongezeka kutoka shilingi Bilioni 161.04 zilizokusanywa katika mwaka 2014/15.

Bw. Mbuttuka amebainisha kuwa mafanikio ya kuongezeka kwa makusanyo hayo yametokana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuhakikisha taasisi, mashirika ya umma na kampuni ambazo Serikali ina hisa zinaendeshwa kwa tija na kuzalisha gawio, ambapo idadi ya taasisi, mashirika ya umma na kampuni zinazotoa gawio na michango zimeongezeka kutoka 24 mwaka 2014/15 hadi kufikia 79 mwaka 2018/19.

Amebainisha kuwa maelekezo ya Mhe. Rais Magufuli pia yamesaidia kuongeza hisa za Serikali katika kampuni ya Airtel kutoka 40 hadi 49, kuongeza hisa za kampuni UDART hadi asilimia 85, kurudisha umiliki wa hisa kwa asilimia 25 katika kampuni ya MECO kutoka asilimia 2, na majadiliano yanaendelea kwa kampuni nyingine.

Bw. Mbuttuka ameongeza kutokana na maelekezo ya Mhe. Rais Magufuli, Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na ofisi yake zimenusuru mali za Serikali zilizokuwa hatarini kutoweka ambapo katika mikoa 10 iliyopitiwa, Serikali imetambua mali 531 na kufanikiwa kurejesha Serikalini majengo 337, viwanja 140, mashamba makubwa 10, maghala 41 na mali zingine 3 pamoja na kurejesha umiliki wa asilimia 100 katika kampuni ya Songwe Water Company Ltd na asilimia 40 kwa kampuni ya Liquid Storage Company Ltd.

Akizungumza baada ya kupokea gawio, Mhe. Rais Magufuli amezipongeza taasisi, mashirika ya umma na kampuni 79 zilizotoa gawio na michango kwa Serikali na ametoa siku 60 kwa taasisi, mashirika ya umma na kampuni 187 ambazo hazikutoa gawio na michango, kutoa gawio na michango hiyo vinginevyo bodi zake zitavunjwa na uteuzi wa watendaji wakuu kutenguliwa.

Mhe. Rais Magufuli amefafanua kuwa Serikali imewekeza mitaji ya kiasi cha shilingi Trilioni 59.6 katika taasisi, mashirika ya umma na kampuni 266 ikitarajiwa kuwa zitaendeshwa kwa tija badala ya kuwa tegemezi kwa Serikali ama kuendeshwa kwa hasara.

Amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kuhakikisha taasisi, mashirika ya umma na kampuni hizo 187 zinawasilisha gawio lake ndani ya muda huo vinginevyo achukue hatua.

Mhe. Rais Magufuli ameeleza kuwa utendaji kazi wa taasisi hizo ni moja kati ya vyanzo muhimu vinavyopaswa kuchangia katika maendeleo ya nchini ikiwemo miradi mikubwa inayotekelezwa nchini, na amerejea kauli yake kuwa kutokana na fursa zilizopo hapa nchini zikiwemo maji, ardhi, madini, gesi, mifugo na nguvu kazi, hakuna sababu ya Watanzania kujiona masikini.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kuongezeka kwa gawio na michango kutoka taasisi hizo bado makusanyo kutoka vyanzo vya kikodi na visivyo vya kikodi hayatoshi na hivyo ametoa wito kwa taasisi hizo pamoja na wadau wengine kuongeza juhudi katika uzalishaji na ukusanyaji wa kodi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameahidi kufanyia kazi maelekezo ya Mhe. Rais Magufuli huku akibainisha kuwa kwa sasa bajeti ya Serikali inategemea mapato ya ndani kwa asilimia 70 na amesisitiza kuwa uchumi wa Tanzania utajengwa na Watanzania wenyewe.

Kesho tarehe 25 Novemba, 2019 Mhe. Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa maadhimisho ya kitaifa Ikulu Chamwino, ataweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) katika eneo la Kikombo, ataweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa jengo la Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) na ataweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Jijini Dodoma.



Chanzo: Ikulu
 
Huyu ndiye kiongozi tuliyemuomba miaka mingi kwa Mungu. Heko Magufuli kwa kuipaisha Tanzania
We kweli unaitendea haki kazi yako. Yawezekana malipo yako ni tofauti na wenzako, maana hoja ikitolewa huna hata muda wa kutafakari bali kudandia na kuanza kusifu.
Ila kama umeoa lazima unapigiwa, ndivyo walivyo watu wa aina yako! Sio mimi nisemaye bali tafiti
 
Amesisitiza. Hata nyumbani kila siku ukishindwa kuleta hata kisamvu Mkeo anakufukuza na atakunyima ugali, saa nyingine atakunyima vyote mpaka mboga. Nimesema atakunyima vyote mpaka mboga.”
Msisitizo umezingatiwa.
 
Hii ndo inatakiwa sana haiwezekani wewe CEO kila mwaka unataka hasara ile hali unalipwa Safari, Gari iko full tank na inaingia service kila muda pia unalipwa mshahara on time halafu hakuna dividend unapeleka hao Mzee timua kabisa tena wengi wamebweteka hawataki kabisa kuona mawazo constructive makazini wao na ujinga wao tu Very static Vijana wapo kibao tu mtaani swala la uzoefu pia wapo walio nao..Watu ni kupiga allowance kibao halafu at the end anakuambia tumepata hasara
 
We kweli unaitendea haki kazi yako. Yawezekana malipo yako ni tofauti na wenzako, maana hoja ikitolewa huna hata muda wa kutafakari bali kudandia na kuanza kusifu.
Ila kama umeoa lazima unapigiwa, ndivyo walivyo watu wa aina yako! Sio mimi nisemaye bali tafiti
Tuambie wewe jinsi ulivyotafakari kabla ya kumkosoa mwenzio
 
Privatization ilikwenda wapi? Mzee wetu Mkapa alishatuwa mzigo,tu.Mashirika yanatakiwa yatoe nafasi kwa wananchi wanunue hisa from DSM stock exchange,hili waweze kukuza mitaji yao .Serikali ijitoe kufanya biashara na mashirika isipokuwa ikusanye kodi kotoka mashirika hayo badala yakupata GAWIO(DIVIDEND) ambayo sometimes inawezekana haikutokana na faida halisi ya shirika husika.
 
Influenza,

Kiukweli mashirika ya umma yenye uwezo wa kiukweli wa kutoa gawio hayazidi 5. Nayo ni kama TPA, NSSF,TRA, nk.

Hayo mengine itakuwa ni maigizo tu. Yatatoa kwa mkono wa kushoto na kurudisha kwa mkono wa kulia.

Imagine shirika kama TTCL linapata wapi ziada na kwa biashara gani? Kwenye biashara ya simu 95% iko dominated na Vodacom, Tigo, Airtel na Halotel. Hiyo 5% ndipo TTCL na Smile, Benson wana share. Sasa TTCL watapata wapi mabilioni ya kurejesha kama gawio?

Mwezi Mei TTCL walikuwa wanaiomba Serikali itoe dhamana wakakope Tsh 1.7 Trilioni ili waboreshe miundombinu yao. Wakati huo huo wakaipa Serikali gawio la Tsh 2.1 Bilion.

Gawio kwa kiingereza ni dividend na inatafasiriwa ifuatavyo;

A dividend is a payment made by a corporation to its shareholders, usually as a distribution of profits. When a corporation earns a profit or surplus, the corporation is able to re-invest the profit in the business (called retained earnings) and pay a proportion of the profit as a dividend to shareholders.

Shurti upate ziada inayotokana na biashara, utoe kiasi cha uwekezaji ndiyo upate cha kugawana na wanahisa.

Hii magawio ya Mashirika ya Tanzania ni usanii mtupu.
 
Privatization ilikwenda wapi? Mzee wetu Mkapa alishatuwa mzigo,tu.Mashirika yanatakiwa yatoe nafasi kwa wananchi wanunue hisa from DSM stock exchange,hili waweze kukuza mitaji yao. Serikali ijitoe kufanya biashara na mashirika isipokuwa ikusanye kodi kotoka mashirika hayo badala yakupata GAWIO(DIVIDEND) ambayo sometimes inawezekana haikutokana na faida halisi ya shirika husika.

Mkuu hii mada yako ya ubinafsishaji na serikali kutofanya biashara ni mjadala mkubwa sana.

Ngudu zetu Kenya walibinafsisha Kenya Airways na kuiingiza soko la hisa lakini sasa serikali inataka kuimiliki tena kwa 100% kwa kununua hisa zote na kisha kjiondoa ktk soko la hisa baada ya kuwa inaleta hasara na kuongeza madeni kwa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom