Rais Magufuli: Baada ya siku 60 Bodi za Mashirika yasiyotoa gawio zijivunje zenyewe

Rais Magufuli: Baada ya siku 60 Bodi za Mashirika yasiyotoa gawio zijivunje zenyewe

Kwa hiyo anataka viongozi wa hayo mashirika ya umma wasijilipe mishahara minono ili wakapeleke gawio kwake!
Huu ni uwendawazimu.
 
Ni mashirika gani ambayo hayajapeleka gawio..?
Haya hapo
tapatalk_1574623605938.jpeg

Haya yalopeleka
 
Nov 2, 2018
Mbwembwe na kauli mbiu /slogans nyingi lakini hakuna wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi wanachofanya vizuri zaidi hata baada ya 'kufundwa'
MSAJILI HAZINA AWAFUNDA WENYEVITI WAPYA WA BODI ZA WAKURUGENZI WA TAASISI ZA UMMA

Source: MAELEZO TV
 
Kwani lazima wapeleke cash?wapige magumashi tu ahadi hewa mpenda sifa atafurahi hata akidanganywa!
 
Mkurugenzi wa Shirika la Posta nadhani hataweza kulala kwa siku zote 60..mpaka kibarua kipotee..
 
Hii ndo inatakiwa sana haiwezekani wewe CEO kila mwaka unataka hasara ile hali unalipwa Safari, Gari iko full tank na inaingia service kila muda pia unalipwa mshahara on time halafu hakuna dividend unapeleka hao Mzee timua kabisa tena wengi wamebweteka hawataki kabisa kuona mawazo constructive makazini wao na ujinga wao tu Very static Vijana wapo kibao tu mtaani swala la uzoefu pia wapo walio nao..Watu ni kupiga allowance kibao halafu at the end anakuambia tumepata hasara
Asilimia 80 ya CEOs na Bodi zao kipindi hiki cha mwamba magu Ni vijana.
Ujana sio uchapakazi uliotukuka.
 
Gawio la trilioni 1.05, miaka yote hizi ndizo pesa zilizokuwa zinajenga mahekalu ya Dar karibu na fukwe.

Hizi ndizo pesa ambazo mabosi walikuwa wanazitafuta na warembo kwenye mahoteli ya Dubai na New York.

Sasa zinakwenda hazina zikapangiwe kazi zenye tija kwa Watanzania.
 
Rais Magufuli atoa siku 60 kwa Taasisi na Kampuni zenye hisa za Serikali zipatazo 187 ambazo hazikutoa gawio lake Serikalini leo, kufanya hivyo kwa Waziri mwenye dhamana vinginevyo Menejimenti na Bodi zake zivunjwe zenyewe kwa kundika barua

Amesema, “Hapa ni Mashirika 79 tu ndio yametoa gawio, hao wengine kila siku wanasema wanapata hasara lakini wana magari na vingine. Mashirika 187 hayana habari ya kuchangia, lakini wana Bodi na kuna Viongozi uko wanasafiri, wanastarehe na wanalipana posho”

Aidha, amebainisha ”Yapo Mashirika ambayo mishahara yao inalipwa na Serikali, wamepewa hadi nyumba lakini hawajaleta gawio ungekuwa wewe Rais ungefanyaje? Ukute wengine wamelala Hotelini sasa hivi wanatuangalia kwenye TV”

Ameongeza, ”Baada ya miezi miwili (siku 60) Taasisi ambazo hazijatoa gawio basi Ma-CEO wa Taasisi hizo wajihesabu hawapo. Wewe kila siku unapata hasara lakini magari mnanunua si muuze hayo magari mtoe gawio?”

Amesisitiza, “Haya Mashirika kila siku yanasema yanapata hasara si tuyavunje tu? Hayana faida. Hata nyumbani kila siku ukishindwa kuleta hata kisamvu Mkeo anakufukuza na atakunyima ugali, saa nyingine atakunyima vyote mpaka mboga. Nimesema atakunyima vyote mpaka mboga.”
 
Ukisikia watu wanakufa kwa pressure ndiyo sasa. maana miaka kadhaa hakuna gawio, just siku 60 lipatikane !1 tutaaamini kuwa walikuwa napiga!
na mtego wakipeleka agawio means hata huko nyuma walikuw2a wanaweza bali walikuwa wazembe hivyo kuondoka kuko pale pale
 
dr Magu tunaomba list nasi tuwawone hapa please ili tukuisaidie kama kweli wanapata hasara tunaomba upublisha MAJINA YAO, na wale waliotoa nao tuombe majina yao na mgao waliotioa
 
Mkuu hii mada yako ya ubinafsishaji na serikali kutofanya biashara ni mjadala mkubwa sana.

Ngudu zetu Kenya walibinafsisha Kenya Airways na kuiingiza soko la hisa lakini sasa serikali inataka kuimiliki tena kwa 100% kwa kununua hisa zote na kisha kjiondoa ktk soko la hisa baada ya kuwa inaleta hasara na kuongeza madeni kwa muda mrefu.
Mashirika ya usafiri wa anga ya serikali yanabeba brand ya nchi sasa kama biashara imekwenda mrama hawawezi kuacha life maana wataua brand ya nchi
Nadhani wakati wa mdororo wa uchumi huko Amerika na ulaya ulisikia serikali ili inject pesa kwenye taasisi binafsi ili kunusuru hayo mashirika kufirisika na kuporomosha uchumi.Ko sometime huwa kuna mazingira ya biashara yanatokea biashara inagoma kuleta faida so hiyo ndio kesi ya Kenya sasa.Lakini ni bora mara mia kubinafsisha huwa kuna tija kiasi kuliko kuyaacha mikononi mwa serikali risk ya kufa ni kubwa
 
Hii kitu ni "Stage Managed", Tra pesa yoote wanayokusanya inaenda hazina na hawafanyi biashara na mashirika mengi ni hivyo hivyo sasa hilo gawio linatoka wapi???

The whole exercise looks to be nothing but a hoax designed to uplift somebody's dwindling credibility and to console the disenchanted people in the aftermath of the bungled civic elections.

However, the strategy will only deceive the fools whose number is dramatically declining as the days go by.
 
Back
Top Bottom