Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Huko Geita hakuna ikulu ndogo? Au hujui kila mkoa una ikulu ndogo? Hizi cheap politics hazitufikishi popote.

Mkuu kweli ikulu ndogo ya Chato inaruhusiwa kuwaita viongozi wa usalama kwenda kufanyia kikao huko?
 
Kama ni ivo basi itangazwe tu hakuna corona nchini ili watanzania wasiwe na hofu
Kikubwa taarifa zitoke halisi ili tujue ukubwa wa tatizo kuwashinikiza wizara ya afya itoe takwimu sahihi ni kama kuwafundisha kazi wizara hio, au hao watu waliopo kitengo apo afya tu wanamuambia mzee kuwa taarifa si sahihi, sasa waziri adanganye kisa nini? Wakati wa tatizo kama hili takwimu sahihi hutoa picha nzuri na watu wakijua ukubwa wa tatizo basi huweka zaidi tahadhari, tukificha ficha mochwari zikianza kujaa ni hatari sana, ila pia namuunga mkono Rais kwa swala la Lockdown ni irrelevant kwetu na litaleta maafa zaidi ya corona kama likitekelezwa
 
Taarifa za waliopona ni za muhimu zaidi Ripoti ionyeshe jumla ya wanaoumwa waliopokelewa,waliopona na waliokufa na balance ya ambao bado wanapambana na hali yao na corona wakigalagala hospitali ambao hawajukikani kama watakufa au kupona

Raisi yuko sahihi
 
Rais John Magufuli ameitaka Wizara ya Afya itoe takwimu za kweli kuhusu maambukizi ya corona ikiwa ni pamoja na kutangaza takwimu sahihi za watu wanaopona ili kuondoa hofu kwa Watanzania.

Kwa mujibu wa Rais idadi ya watu waliopona ni ndogo kuliko hali halisi na kwamba, ana taarifa kuwa hadi wakati Waziri Mkuu alipotangaza idadi ya watu walioambukizwa, waliopoteza maisha na waliopona zaidi ya watu 100 walikuwa wamepona.
Firm Fiasco
 
Ngoja nitunze maneno yangu nisije nika mponza melo na mimi mwenyewe....maana order ishatoka.
 
Huyu ndyo zake. Wamepika data weee leo hii eti toeni data za ukweli. Hii ndyo sababu ya kufanyia mabadiliko wizara? Hii tabia yake ya kutengeneza tatizo alafu anasolve ili aonekane hero, hii leo itagonga mwamba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..Chato ni kijijini kwa Magufuli.

..JK hakuwa kuzungumza toka Msoga.

..Mkapa hakuzungumza toka Lupaso.

..Mwinyi hakuzungumza toka Zanzibar au Mkuranga.

..Mwalimu Nyerere hakuwahi kuzungumza toka Butiama.

..Raisi anapaswa kuendesha shughuli zake toka IKULU, na siyo toka ktk nyumba yake binafsi. Serikali siyo KAMPUNI binafsi ya Raisi.
Kila mkoa Kuna Ikulu. Iringa ikulu IPO gangilonga,Mwanza IPO capripointi. Musoma IPO kwa RC .
Zinaitwa ikulu ndogo.
Mzee mkapa Aliwahi kuhutubia Nchi akiwa uingereza( alienda kutibiwa mguu)
Sherehe za Kitaifa Kikwete alihutubia Mei mosi 2015 akiwa CCM kirumba.
Inawezekana fungua fikra.
 
Jiwe umejua kunifurahisha leo, kuna wapumbavu wanatamani fungafunga oh funga masoko funga maduka funga baa mara zuia kile nawaambia hawajui wanachokitamani wangejua adha na tabu za lockdown na fungafunga ni zaidi, afadhali mara elfu kumi ya corona wasingekaa wakathubutu kupayuka habari za lockdown na funga hiki fungia kile.

Wapumbavu wakubwa zaidi ni wale wasiojua maana ya lockdown na kushindwa kujua kuwa itatokea automatically. Wenye akili wameshafunga biashara zao na hadi kuna dayosisi za makanisa wamesimamisha shughuli zao.
 
Data za watu waliopona zilistack kwa muda mrefu... Inawezekana wizara haitaki kusema kwa kuhofia watu wataidhaurau corona na umakini utapungua... Nadhani
 
Back
Top Bottom