Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Uhalisia uko wapi? Ni kwamba Wizara inapika takwimu? Rais naye ana source tofauti na Wizara ya afya inayompatia taarifa(sahihi)? Rais haridhishwi na taarifa za Wizara kuonyesha tatizo linaongezaka na kwamba anatoa maelekezo ili taarifa zichukue mwelekeo wa kuonyesha shida sio kubwa?

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kahamishwa leo, je ni uhamisho wa kawaida au katikati ya vita ya corona kulikua na utofauti wa utoaji taarifa kati yake na Waziri ambapo mmoja imebidi ahamishwe? Kumbuka Rais alishawahi kusema alikua akiwafatilia Waziri wa Afya na huyu KM aliyehamishwa wakati huo akiwa naibu KM TAMISEMI(Afya) na akajua kua wanaugomvi
 
Tatizo, kama hawapimi watu, hivyo hawawajumuishi katika idadi rasmi, watu wanaumwa, halafu wanapona wenyewe, watu hawa wakipona, hawawezi kujumuishwa kwenye idadi rasmi ya waliopona, kwa sababu hawakuwemo kwenye hesabu tangu awali.

Magufuli alitakiwa kuongoza, si kuwasakizia wenzake kazi, halafu kuwazodoa na kulalamika.

Ina maana mikakati yote inavyofanywa rais hajui?

Kashindwa kazi?
 

umesema sahihi, naomba kukuhakikishia kuwa hata huyu Victoire ameongea kama kasuku, kakuruouka, kaiga, kalimeza na ndio maana anaandika bila aibu 'only in Tanzania' ukimuuliza nchi zingine inakuwaje? hawezi kutoa taarifa akiwa mbeya, mwanza, arusha?

mbona JPM mwenye wala sio mtu wa viwanja, na kula bata mamtoni....................hata akienda chatto alaumiwe?? aisee

achana nao hao
 
Kwa joto la 100'c si Pua itafanana kama mchemsho wa mbuzi wa pale kwa Mangi?
Umeambiwa above. Inaelekea Rais wetu anasoma sana social media na anaangalia sana YouTube. Kasema hadi ya vitunguu. Nimecheka. Yani ana majibu rahisi kwenye maswali magumu.
 
Wapumbavu wakubwa zaidi ni wale wasiojua maana ya lockdown na kushindwa kujua kuwa itatokea automatically. Wenye akili wameshafunga biashara zao na hadi kuna dayosisi za makanisa wamesimamisha shughuli zao.
Hakuna biashara iliyofungwa zaidi ya baadhi ya makanisa na misikiti nani afunge apate hasara? Tunafanya biashara Kama kawaida sijui huko ulipo wewe unaposema biashara zimefungwa ni wapi

Sent from my Infinix X624 using Tapatalk
 

Ye amekazania waliopona tuu.
Mbona hawatangazi idadi ya watu wanaofanyiwa vipimo?
 
Ina maana Leo anawakana wenzie walioshirikiana naye "kuzipika" hizo data??

Kwa kuwa ninavyomfahamu Jiwe, kama hizo data wangekuwa wanajitamkia tu wenyewe, tungeshasikia keshawatumbua
 
Kawasafirisha kina IGP,CDF,Chief wa uhamiaji n.k. Asante China.
 
Nilijua itakua Live vile tamko limetoka. All in all, bora wamefanikiwa kuonyesha

Hii hotuba ya leo niko 50/50, kuna mahali nimeielewa na pengine sijaielewa.

Kitu muhimu tu cha kukumbushana na wapendwa wetu, tujichunge vitu tunavyoandika mitandaoni, na kwenye groups za WhatsApp.

Vita ya corona kwa namna moja ni kama inaelekezwa kwa watu wanaopinga au kukejeli hatua za serikali.
 
Mda si mrefu takwimu za waliopona itasahihishwa
♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Wanasahau USA Kuna camp David's maraisi wanakaa huko hata miezi na hotuba zinatoka huko Kama kawaida sema nini wamezoea kukariri Kama kasuku

Sent from my Infinix X624 using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…