Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Aiseee sina la kusema ngoja nitafute muarobaini wangu kabla haijaisha

Hapa kweli kiongozi tunaye duh!

"Fumigation ni upuuzi " Kwa hiyo ile Ofisi ya Temeke iliyokuwa inahifadhi dawa za fumigation kumbe haikuwaka moto kwa bahati mbaya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikalili kijana,rais ni higher authority anaweza endesha shughuri zake akiwa popote pale,rais ndio Ikulu ,Ikulu sio jengo.
Hawajui wamezoea kuona DJ anavyoendesha Sacco's wanajua na uraisi ni Kama mwenyekiti wa Sacco's ya ufipa

Sent from my Infinix X624 using Tapatalk
 
Huyu mzee ni kiongozi mbovu, wa hovyo. Kwa alichoongea leo ni kwamba ana tatizo kubwa kuliko tunavyomdhania. Mungu tusaidie
Mkuu, unaonaje kama ukichukua form hii 2020 tukupe kura uingie ikulu.
 
Usikalili kijana,rais ni higher authority anaweza endesha shughuri zake akiwa popote pale,rais ndio Ikulu ,Ikulu sio jengo.
Unajua akili mbovu za watanzania kama wewe ndizo zinazofanya nchi ionekane ya wajinga. Hivi kama ingekuwa hivyo kungekuwa na haja ya kuwa na ofisi rasmi ya Rais? Hivi unaelewa maana ya ikulu?
 
Ushauri wa bure fuateni maelekezo ya madaktari na yale ya shirika la afya duniani (WHO).
Hawa wahuni wengine ni vyema mkawapuuza, wapuuzeni wao na kauli zao za kihuni.
People are dying out there, we're all ignorant to a tragedy until it happens to you.
Chukua hatua, you're on your own....ilinde familia yako na jilinde pia.
Korona inaua.
 

Huna hiyo sababu, ndio maana JPM ni rais na wewe upo hapa JF unaganga njaa.
 
"Lakini pia taarifa zetu ziendane na ukweli hasa katika watu wanaopona. Nina taarifa kwamba mpaka leo tulikuwa na wagonjwa 284, lakini naambiwa karibu 100 ya wagonjwa walishapona. Hizi takwimu za wagonjwa wanaopona nazo zitangazwe ili kuwaondolea hofu wananchi" - Rais John Magufuli.
 
Yaani kiongozi mkuu wa Nchi Kuja kwa raia kutoa ushuhuda was Jambo ambalo liko chini ya uwezo wake nikuonesha kiasi gani hana mawasiliano mazuri na wataalam wake. Chukulia mfano hizo kemikali zingekuwa na madharaa kwa binadam nani alipswa kuwajibika??, Ilihali haya yanafanyika chini ya kijana wake mpendwa. Tuache kusifu mambo yakipuuzi
Rais Magufuli yuko sahihi kwa 100%
 
Kwa taarifa yako tangu juzi wamarekani hawataki tena lockdown wanaandamana mitaani.
Acheni uongo wenu nyie watu! Eti Wamarekani wakati ni baadhi tu ya wafuasi wa Trump! Wafuasi ambao hawana tofauti na MATAGA wanaounga mkono chochote kutoka Magogoni!

Trump alituma tweets nadhani 3 au 4 akitaka baadhi ya majimbo yawe "LIBERATED" from lockdown kinyume na matakwa ya wengi including governors, ndipo Waafidhina wafuasi wa Trump siku ya pili wakaingia mtaani!!

Kuona hivyo, baadhi ay taasisi, including WSJ na NBC wakaitisha kura za maoni naikaja kugundulika majority ya Wamarekani, including Republicans, wanataka lockdown isiondolewe mapema, na ikagundulika waliokuwa wameandamana ni wafuasi wa Trump katika kumuunga mkono nia yake!
 
Kweli kabisa anastahili pongezi..ni rais wa wanyonge..anatupenda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…