Wakuu nawasalimu kwa jina la yeye aishiye milele. Mungu aendelea kuwapa faraja,upendo na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Back kwenye mada. Jana mkuu wa kaya kaibuka baada ya wengi kudai kaikimbia kaya. Kaibuka na ungangali wake ule ule wala hajabadilika. Kaibuka akitoa maelekezo ya kidaktari huku hoja hoja zake nyingi zikipingana na wataalamu wetu. Nikajiuliza maswali kadhaa je kabla ya hotuba:
1. alipata ushauri wa wataalamu husika kujua ABC ya hili janga?
2.Mbona hotuba yake inapishana pishana na maelekezo ya wataalamu ambao ushauri wao tayari tulisha uamini na kutuumia,je kauli zake si zitaleta mtafaruku zaidi kwenye kaya?
3. Nimeshangaa mkuu wa kaya kuamini "Hearsays" nyingi kuliko tafti rasmi za wataalamu. Je haoni kwamba hiyo ni kuwapoteza zaidi wanafamilia wake?
4.Kuna raia wema wengi walikua wameshika kasi kujitolea kusaidia kutoa vitakasa na viziba midomo. Leo kiongozi unatoka na kauli tata zilizojaa tashwishwi ambazo hazina utafti rasmi hapo si ni sawa na kuwavunja moyo wahisani?
Binafsi kwenye hutuba yake sikuona mkakati wowote wa kimantiki.Nilizani kwa ukimya wake angekuja na strategical plan ya kueleweka akiwa kashirikiana na wataalamu wake. Nilichokiona mengi aliyoongea jana kajishauri yeye mwenyewe tu,kwani aligeuka kuwa Daktari.
Halafu vitisho viiingi visivyo na sababu. Kwa ufupi amezidisha taharuki badala ya kupunguza ndio maana nasema ni bora angekaa kimya tu awache akina Bashite waendelee na maigizo yao angalau kuna wakati huwa wanapitia.
Sent using
Jamii Forums mobile app