Swelana,
Hapo hakuna jibu mkuu.
Kwanza hao unaowaomba watafute mbinu, sijui mbinu hizo zitatoka wapi? Wewe hadi sasa huwaonei huruma kwa yote waliyokwishayapitia?
Ningekusoma/kusikiliza kama ungewaomba polisi, lakini unawaonea wapinzani kwa kuwaonea tu?
Kufunga Dar kwa sasa ili iweje?
Himiza (sijui nani atakusikiliza wewe) barakoa ziwe kama uniform ya primary, hakuna kuikosa hata kwa saa moja ukiwa nje. Polisi walisimamie hili.
Mikutano yote ya makundi, hata huko kwenye ibada marufuku kabisa.
Polisi wasimamie, hata kwenye usafiri, 'Social Distancingizingatiwe'bila ya kuchekeana.
Kiufupi, lililopo sasa ni kutafuta njia za kupunguza/kudhibiti maambukizi, sio tena kuzuia kusambaa kwa ugonjwa. Ugonjwa sasa upo kila sehemu ya nchi, na kote kunahitaji hatua hizi za pamoja, sio sehemu moja tu ya nchi.
Sina hakika kama Trump atapona, kama coronavirus na hali ya uchumi itamwacha salama; kwetu hili halitusumbui, kwa sababu polisi na silaha zote zipo.
Kwa hiyo hata huko kuwaza tu ni kukosa heshima kwa watawala.