Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

mkuu kwanini ? mbona viongozi wa serikali wanakufa ovyo ? nini tatizo ? aisee Malaria hii alosema bwana mkubwa ?


Sent from my iPhone using JamiiForums
.
Screenshot_20200427-213414.jpg
 

mkuu ni kweli wanakufa na corona sio siri na hii yote ni upuuz wa serikali, haya sio mashindano yan nlivyosema wanakufa umeleta kifo cha jamaa wa chadema ila mpaka sasa imedondoka mijitu ya CCM kama saba ivi sa nan mshind hapo kama ingekuwa mashindano? serikali waache mambo ya kipuuz watu tutakufa kama kuku wa kideli, na nakuhakikishia itafika wakati utakubali tu, kama upo dar umwa saiv alafu upelekwe hospital utaelewa nasema nini..


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
toughlendon_1, Sio nyinyi misukule kila kiongozi wa serikali/CCM akifa mnakuja haraka jf kukejeli na kuandika Corona hiyo kwa furaha? Nimekuwekea hii picha ujue tu hata chadema wanakufa ukisema kisayansi sijui Ni sayansi ipi hiyo unayosema maana wataalam/madaktari wetu wanakesha kuhudumia na kudhibiti hili janga unaona wao hawajui kazi na wanacheza tu wewe mwana chadema uko nyuma ya keyboard ndio mtaalam wewe dokta wewe unakosoa tu unaropoka tu Kama wewe unajua kuliko hão wenye taaluma yao nenda kawasaidie uonyeshe hiyo sayansi yako tuje tukusifie

Kumbuka kuchukua tahadhari kwa kujikinga na kufuata ushauri na miongozo ya wataalam wa afya
 
Sio nyinyi misukule kila kiongozi wa serikali/CCM akifa mnakuja haraka jf kukejeli na kuandika Corona hiyo kwa furaha? Nimekuwekea hii picha ujue tu hata chadema wanakufa ukisema kisayansi sijui Ni sayansi ipi hiyo unayosema maana wataalam/madaktari wetu wanakesha kuhudumia na kudhibiti hili janga unaona wao hawajui kazi na wanacheza tu wewe mwana chadema uko nyuma ya keyboard ndio mtaalam wewe dokta wewe unakosoa tu unaropoka tu Kama wewe unajua kuliko hão wenye taaluma yao nenda kawasaidie uonyeshe hiyo sayansi yako tuje tukusifie

Kumbuka kuchukua tahadhari kwa kujikinga na kufuata ushauri na miongozo ya wataalam wa afya

Nimekwambia leta hoja sio mashindano ya siasa yan ccm vs chadema me sinaga chama, leta facts hapa mkuu me sio mwanaiasa, jana saa tano mtu kafa Lumumba makao makuu kabisa ya ccm, mpaka leo saa nane mait haijatolewa unadhani hiyo sio impact ya namna serikali inaichukulia korona? mtu kadondoka kama kuku wa kideli, haya labda kafa na malaria mbona haji kutolewa ? Serikali(Ambayo ni serikali ya CCM), wanawaza nini ?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Swelana,
Hapo hakuna jibu mkuu.

Kwanza hao unaowaomba watafute mbinu, sijui mbinu hizo zitatoka wapi? Wewe hadi sasa huwaonei huruma kwa yote waliyokwishayapitia?
Ningekusoma/kusikiliza kama ungewaomba polisi, lakini unawaonea wapinzani kwa kuwaonea tu?

Kufunga Dar kwa sasa ili iweje?

Himiza (sijui nani atakusikiliza wewe) barakoa ziwe kama uniform ya primary, hakuna kuikosa hata kwa saa moja ukiwa nje. Polisi walisimamie hili.

Mikutano yote ya makundi, hata huko kwenye ibada marufuku kabisa.

Polisi wasimamie, hata kwenye usafiri, 'Social Distancingizingatiwe'bila ya kuchekeana.

Kiufupi, lililopo sasa ni kutafuta njia za kupunguza/kudhibiti maambukizi, sio tena kuzuia kusambaa kwa ugonjwa. Ugonjwa sasa upo kila sehemu ya nchi, na kote kunahitaji hatua hizi za pamoja, sio sehemu moja tu ya nchi.

Sina hakika kama Trump atapona, kama coronavirus na hali ya uchumi itamwacha salama; kwetu hili halitusumbui, kwa sababu polisi na silaha zote zipo.

Kwa hiyo hata huko kuwaza tu ni kukosa heshima kwa watawala.
 
mr chopa,
mzee kuna kitu hakipo sawa mzee inapofanya vizuri tunasifia wanapokosea tunakosoa tu kuna kitu hakipo sawa yan serikali ijifunze kutokana na haya matatizo wanatakiwa wainvest heavily kwenye Afya , Nchi ina maVX V8 mengi kuliko ventilators VX moja dola 120000, ventilator moja dola 60000, barabara kilo meta moja inajengwa kwa Almost 1B, hii 1 billion inanunua ventilator ngapi ? achen kutetea upuuz


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hata kama mods wataufuta huu Uzi kwa ubabe au kwa kukusikiliza lakn,ninawaambia ukweli dar wagonjwa ni wengi na vifo ni vingi, Mimi Niko sekta ya afya niaminini niyasemayo,dar wengi ni wagonjwa na hawajijui.

Sent using Jamii Forums mobile app
'Swelana', ngoja nikupe ushauri.
Uwe unapima watu wa kujibishana nao. Mtu kama huyo uliyemjibu haisaidii chochote kumjibu. Hawa wapo hapa jamvini kwa kazi maalum, hawana lolote la maana wanaloweza kuongeza kwenye mada yako.

Asiyejua Dar sasa hivi ni kituo kikuu cha gonjwa hilo ni nani? Wenyewe serikalini wanalijua barabara.

Kwa mara ya kwanza kabisa tokea Dar liwe jiji, maiti inaonyeshwa mitaani na wapita njia wakipita pembeni.

Haya tulizoea kuyaona Afrika Magharibi, leo hii ni Dar yetu ndiyo yenye heshima hiyo.

Hakika tumepiga hatua kubwa. Toka Mbunge kucharazwa risasi mchana kweupe, hadi maiti zikiachwa mitaani!

Baada ya hapa, ni kipi kitakachofuata?
 
Ikulu ipo kila mkoa kaka kila wilaya, we unahis rais akienda wilayani analala guesthouse au
Hofu imeanza kutanda Dar es Salaam.
Nakubaliana na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kuwa hofu ni hatari kuliko ugonjwa wenyewe.
Katika nyakati kama hizi, ni muhimu Jenerali aonekane hadharani kuwatoa hofu wananchi wake.
Huu ni wakati muafaka wa Rais Magufuli kupita sehemu mbalimbali za Jiji la Dar kuthibitisha usemi wake wa kutokuwa na hofu.

Rais Magufuli, onyesha kuwa huna hofu. Toka mafichoni Chato watu wakuone mitaa ya Lumumba ili watu wasiikimbie maiti. Vijana wa IGP Simon Sirro, walioiva kwenye taaluma ya Jeshi la Polisi wamejawa na hofu kiasi cha kuikimbia maiti mtaa wa Lumumba.

Amiri Jeshi Mkuu,toka Chato uonekane katika mitaa ya Lumumba, Manzese, Mbagala na kwingineko ili uwape watu hamasa ya kupambana na hofu ya COVID-19.

Toka Chato utembee katika mitaa ya Dar es Salaam bila hivyo vi-barakoa vya mabeberu kuonyesha kuwa wewe ni Amiri Jeshi Mkuu usiyejaribiwa na yeyote, hata kama anaitwa Covid-19!
 
Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Magufuli anatarajiwa kuzungumza mubashara na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu ugonjwa wa Corona kutokea Chato saa 9:45 alasiri leo tarehe 22.4.2020

Je chakula, mimea na tiba asili yanaweza kuongeza kinda ya mwili dhidi ya ugonjwa wa Corona?
 
Tulitaka kupambana na ugonjwa huu wa COVID-19 tusahau kuwaza kwamba uchumi wetu utakuwa katika Hali gani endapo tukichukua hatua Fulani.

Kwa Hali ilivyo bado nashauri kuwa lockdown Ni mhimu ili kupunguza maambukizi yanayoenea kwa Kasi ili baadae tuweze kulejea katika Hali ya kawaida.

Bila kufanya hivi kwanza tutegemee uchumi wetu utaporomoka kwa Kasi kuliko hata wale waliojifungia ndani. Pia Kuna mambo yatakwama mwaka huu mzima mfano kufungua vyuo pamoja na shule za msingi Nan sekondari. Wakati huo huo tukumbuke kuwa hotel na baa haziingizi kitu kwa wakati huu.

Sasa huo uchumi sijui utakuaje. Tuchukue hatua, ingawa tumechelewa lakini bado tuna kitu Cha kuokoa hasa kwa baadhi ya maeneo ya nchi.
 
Sisi Watanzania hatutaki lockdown Wanaotaka lockdown ni wanasiasa matajiri wasio kuwa na njaa

Sisi wamachinga,mamalishe, wauza kahawa, mawakala wa mpesa, wauza maduka, madalali,wakulima, wawabangaizaji nk.

Hatujawahi na hatuitaki lockdown sisi tutakufa kishujaa tukitafuta mkate wa kila siku
Rais Magufuli wanaolilia lockdown ni wanasiasa matajiri wenye mishahara mikubwa, wasio kuwa na njaa na wala hawajawahi kuja kwetu kuuliza matatizo yetu

Wao matajiri wana hofu ya kufa, sisi Watanzania tuliowengi tuna hofu ya njaa

Tupo tayari kufa barabarani tukitafuta mkate wa watoto wetu na wazee wetu kuliko kufa ndani na njaa tukiwa tumejifungia ndani

Msiwasikilize wana Siasa tusikilizeni sisi Watanzania tuliowengi. Wanasiasa hawazidi hamsini Watanzania tupo milion hamisini.

RAIS Magufuli usitufungie Ndani baba yetu2 tutakufa njaa ,hao wanasiasa hawana njaa wanatafuta umaarufu wa kisiasa
 
... leo utaanzisha thread za kingese kweli kweli! Kama umepagawa vile!
 
Usiwe unasahau kuweka namba zako za simu kwenye mabandiko yako mkongwe.
Tuko pamoja!!!
 
Back
Top Bottom