Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Akiwa Chato:
Ndege za Utalii zimeshajaa hadi August
Tuko mbioni kuruhusu zianze kuingia nchini waje wajionee wenyewe
Vyuo vikuu navyo tutafungua karibuni
Tuna vyakula vingi tuko tayari kuwauzua majirani
Huu ugonjwa sio kama Ebola, tusiogope
Dereva kasafiri na gari zaidi ya 1000km unakuja unampima unasema anaCorona......kicheko




Wagonjwa wa korona wamepungua sana
Kwa mfano

Dar Es Salaam
Waliobakia Mahospitalini

Amana 12
Mloganzila 6
Kibaha 22
Aghakan 31
Hindumandal 7
Rabinsia 14

Arusha
Vituo viwili wagonjwa hakuna, Mushono 11

Mkoa w Mwanza
Vituo vya Buswelu kuna wagonjwa 2 na Misungwi pia 2 na Bugando kuna wagonjwa 2

Lakini vituo Ukerewe, Mogela, Mkuyuni, Sengerema, Kwimba kote hakuna wagonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JPM
"Hili ni taifa huru, ni taifa linalojiamini, lilishapambana na majanga mengi likadhinda.
Hakuna cha lockdown wala shangazi yake lockdown😀😀🙌
Akili za kuambiwa changanya na zako, unaambiwa kakae lockdown na ww unaenda jifungia chumbani huku hata chakula huna"
 
“Mimi Mtoto wangu wa kumzaa amepata corona akajifungia, akajifukiza akapiga malimao, sasa hivi ni mzima kabisa anapiga push-up, msije mkadhani mimi sijapata Mtu wa karibu mwenye corona, tuondoe hofu”-JPM

“Kuna mambo ya hovyo yanafanyika, kila Mtu akifariki wanakimbilia kumpima corona, Mtu amefariki unampima yanini?, nguvu za kumpima wanazo, za kumuhudumia akapona hawana, Mtu atakapofariki kwa ugonjwa wowote hata wa corona lazima azikwe kwa kawaida, corona sio Ebola” -JPM

“Kuna rafiki yangu mmoja Injinia alipata kiharusi akapelekwa Muhimbili, wakampima wakasema ana corona, amepelekwa Amana Watu wanamuogopa kisa ana corona, Ndugu zake wakamtoa wakampeleka Agha Khan, wamechukua vipimo wakakuta mzima hana corona, amepona yupo nyumbani” -JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila tukumbuke kua naomba nimnukuu waziri wa elimu wa Kenya "Kaburini HAKUNA masomo" mwisho wa kunukuu
Big up Mr President nasubir kitabu Chako MIAKA 15 au ishirini ijayo....
 
I see
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…