Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

“Kwa hali hii, kama wiki tunayoianza kesho itaendelea hivi nimepanga kufungua vyuo ili Wanafunzi wetu waendelee kusoma, lakini nimepanga pia kuruhusu michezo iendelee kwasababu michezo ni sehemu ya Burudani, maisha lazima yaendelee” -JPM

“Ugonjwa huu wa corona ni vita kama vita nyingine, wakati unaanza nilisema siwezi kuruhusu lockdown, imagine unafungiwa ndani hupati hata nafasi ya kuonana na Mkeo?, unafungiwa ndani eti usitembee usiku kana kwamba corona inatembea usiku tu, nikasema hapana” -JPM
#JPMChato

Source:Millard Ayo
 
Magufuli sitokaa tena nijibu mambo yake anayozungumza wala sitokaa nimuanzishie thread humu. Nasema kweli kabisa! Leo nimejua kumbe hata nchi yoyote ile duniani inaweza kuongozwa na kiumbe wa ajabu kama wananchi wake na watu wa maamuzi hawatakuwa makini.

Tanzania nadhani tumeletewa Hutu mtu ili tuelewe kuwa tunatakiwa kuchukulia kila jambo kwa umuhimu wake. Tunaonywa kuacha kupuuza vitu.

Magufuli nilikuwa natumia nguvu kuwaza vitu vya hovyo anavyoamua nilikuwa nakosea sana! Nilipaswa kutumia muda wangu kumfahamu zaidi akili yake! Mungu nisamehe! Zaidi ninafanya mambo yangu bila kumsikiliza yeye kwenye jambo lolote lile maana uwezo huo ninao! Ninafanya mambo yangu kwa kuizingatia akili yangu. Magufuli sitokaa nifuate kitu anachonielekeza maana nimemjua!
Kumbe ulikuwa mpuuzi kiasi hicho. Tumia nguvu, akili na maarifa yako kubiresha maisha yako na wapendwa wako. Siasa ni hobi tuu Kama ilivyo hobi nyingine.
 
Acha ujinga wewe ebu angalia kuanzia april moja mpaka may 5 watu wangapi maarufu wamepukutika kwa korona? Wewe unadhani serikali yako ficha ficha jazz band itakwambia ukweli? 1 April alianza mtu maarufu Marini Hassan watu wakaenda kumzika bila kuchukua tahadhari akaondoka na wawili fasta huku kina Egbert Mkoko na wenzake wakipona(walitoa ushuhuda wa kupona korona),kigogo ndio aliyetoa taarifa marine kafa kwa korona na kaambukiza kina egbert lakini watu walipinga ila juzi nimeuona live egbert mkoko akitoa ushuhuda wa kupona korona!!

Baada ya Marini hassan vifo vikaanza kufululiza sana vya mawakili,wachungaji na viongozi wa serikali,hao ni wale tunaowajua,mie watu watatu kitaani wamedanja na korona,wengine wamepona,wengine walifanya contact tracing wakawekwa karantini lakini walitoka salama!!

Uliangalia BBC? Kikeke alikuwa anamuhoji Baruani Mshale mkazi wa Njiro uliona alivyosema? Kama wewe mkazi wa njiro nenda kaulize kule kila siku ni misiba watu wanaondoka na korona.

Acheni ujinga nyie kuwachuza watu as if hakuna ugonjwa huu wakati upo,hatuwezi kutatua matatizo kwa kujidanganya kwamba hayapo.
Nimekuuliza kitaa chenu...sijui mineno mingi ya nn
 
Mhe. Rais Magufuli anatarajiwa kutuma salaam kwa Taifa leo Mei 17, 2020.

Hotuba yake inaaminika itajaa mambo mazito.

Kaa standby kwenye media zote na mitandao ya kijamii muda si mrefu ujao.

Inatarajiwa kuanzia mida ya saa sita na nusu mchana (12:30PM) ndipo atakuwa mubashara.

JF will cover it

======

View attachment 1452519

‪RAIS AMETOA SALAAM BAADA YA KUSHIRIKI KATIKA IBADA YA KANISA LA KKKT USHARIKA WA CHATO‬

Raisi Magufuli akiwa katika kanisa la KKKT Chato amepata nafasi ya kuzungumza mbapo ameongea mambo mbalimbali,

Katika hotuba hiyo Raisi ameanza kwa kumshukuru Mungu na viongozi wa dini wote nchini. Raisi magufuli amesema “Waimbaji wameimba hapa kwamba bila mungu huwezi kuongoza, bila kumtanguliza mungu huwezi ukafanya chochote. Kwahiyo napenda niwashukuru Watanzania wote, Viongozi wa dini mbalimbali ambao wameshiriki kuliombea taifa hili"

"Na ndio maana siku za nyuma wakati ugonjwa huu umeingia niliwaomba ndugu zangu watanzania angalau tutumie siku tatu za kuomba kwelikweli. Ninawashukuru sana kwa sababu wote tuliomba tulifunga na Mungu amejibu na Mungu ametusikia”

“Ndugu zangu mifano mingi imetolewa, hata katika mahubili yako leo Baba Mchungaji katika injili na katika matendo ya mitume umeeleza ni namna gani watu walivyoweza kumtegemea Mungu walivyoweza kufanikiwa”

“Yule kipofu alimlilia yesu, Mwana wa Daudi nirehemu, Yesu ambaye ni mtoto wa Mungu ambaye naye pia ni Mungu alimponya. Wakati wa dhoruba kula baharini wanafunzi walivyokuwa wamelala wakaona mtumbwi unataka kuzama walipiga kelele” Katika maandiko pia sehemu zingine Yesu aliwakemea kwanza mitume kwa kuwa na Imani ndogo na baadaye akaikemea pepo na mambo yakawa shwari kwahiyo sisi katika kipindi chochote kigumu cha aina yoyote tukimtanguliza Mungu tutafanikiwa”

“Kwahiyo ninawashukuru sana ndugu zangu, ninawashukuru sana Wachungaji, Masheikh, Mapadri, Maaskofu kila mmoja katika eneo lake ambao tulimtanguliza Mungu na Mungu ametusaidia sana”.

“Ndugu zangu katika mapambano ya aina yoyote ni vita. Ugonjwa huu wa Corona hauna tofauti na vita nyingine. Nilikwisha eleza na wataalamu pia wameahaeleza ni namna gani nzuri ya kuweza kupambana na ugonjwa huu hata Baba Mchungaji umezieleza mbinu zote”.

“Ni kweli sikutoa amri ya lockdown ya kuwafungia watu majumbani, ulikuwa ni utumwa wa ajabu. Imagine wewe Lyabange ufungiwe saa nyingine hata usionane na Mme wako Iseme au na watoto wako. Sisi hapa huwa tunaondoka asubuhi kwenda kuchukua chakula, ukachume viazi, maharage yako, uende ziwani ukavue hivyo vyote vingekuwa vimezuiliwa tungekuwa tuko wapi sisi Watanzania miliono 60?"

Huruhusiwi kwenda sokoni, na saa nyingine unaruhusiwa kutoka kidogo tu, halafu usiku usitoke kana kwamba Corona inatembea usiku tu. Hebu tujiulize sisi Watanzania tuna miradi mingi tumeweka katika nchi yetu, Hiyo miradi yote ingekuwa imesimama.

"Tunajenga reli kwa mabilioni ya fedha, Makandarasi kutoka Nje wale wote tungewazuia vijana wasipate kazi tungekuwa wapi?"

"Tunajenga Mradi wa umeme, thamani yake ni Zaidi ya Trilioni saba zimechukuliwa na Watanzania kwenda kuinvest pale kusudi tuwe na umeme, leo wale wote tungekuwa tumewasimamisha, vijana wale wote tungekuwa tumewasimamisha; tunajenga barabara zote zingekuwa zimesimama."

"Hapo tunajenga meli kwenye ziwa Viktoria na juzi mmeona Injini zimekuja kutoka Korea, zote zile zingekuwa tumesimamisha na injini zisingekuja."

.
Awaasa wahumini waendelee kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa huu lakini pia amesifia kuona waumini woote kanisani hakuna hata mmoja alivevaa barakoha...Aiseee...Ehh Mungu wangu
 
Acha ujinga wewe ebu angalia kuanzia april moja mpaka may 5 watu wangapi maarufu wamepukutika kwa korona? Wewe unadhani serikali yako ficha ficha jazz band itakwambia ukweli? 1 April alianza mtu maarufu Marini Hassan watu wakaenda kumzika bila kuchukua tahadhari akaondoka na wawili fasta huku kina Egbert Mkoko na wenzake wakipona(walitoa ushuhuda wa kupona korona),kigogo ndio aliyetoa taarifa marine kafa kwa korona na kaambukiza kina egbert lakini watu walipinga ila juzi nimeuona live egbert mkoko akitoa ushuhuda wa kupona korona!!

Baada ya Marini hassan vifo vikaanza kufululiza sana vya mawakili,wachungaji na viongozi wa serikali,hao ni wale tunaowajua,mie watu watatu kitaani wamedanja na korona,wengine wamepona,wengine walifanya contact tracing wakawekwa karantini lakini walitoka salama!!

Uliangalia BBC? Kikeke alikuwa anamuhoji Baruani Mshale mkazi wa Njiro uliona alivyosema? Kama wewe mkazi wa njiro nenda kaulize kule kila siku ni misiba watu wanaondoka na korona.

Acheni ujinga nyie kuwachuza watu as if hakuna ugonjwa huu wakati upo,hatuwezi kutatua matatizo kwa kujidanganya kwamba hayapo.
Wenye akili tunaendelea kuchapa kazi huku tukichukua tahadhali.
Wajinga endeleeni kuomboleza vifo vya corona vinavyotokea kwenye page ya kigogo 2014

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je amezungumzia hali ya ugonjwa nchini??

Amekumbushia kuhusu kuchukua tahdhari?
 
Wenye akili tunaendelea kuchapa kazi huku tukichukua tahadhali.
Wajinga endeleeni kuomboleza vifo vya corona vinavyotokea kwenye page ya kigogo 2014

Sent using Jamii Forums mobile app
Taja mtu ambaye kigogo amesema amefariki kwa korona halafu sio kweli kuwa alidanganya,nitajie hata mmoja!! Kigogo alisema nyaga ana korona mkabisha ila sasa anaumwa yupo TMJ,Marine mlibisha,Lwakatare mlibisha,Mitiming milibisha etc ila sasa Mzee Baba kasema watu wa korona wazikwe kikawaida tu ndio maana unaona watu wanakabidhiwa miili wakazike wao!!
 
Mkuu usishawishike hata siku moja kumuamini huyu mzee,hana ukweli hata mmoja.

Anatupeleka sipo kabisa mkuu,yaani kauli zake tu ni utata mtu alafu sijui hana kumbukumbu ya kile alichokinena hapo awali.

Tumeangamia kama taifa,dereva wenyewe ndo huyu basi tupo hatarini kutumbukia mto wami.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kabisa unaamini Rais amekusudia kuangamiza roho za watanzania? Ni mtu mbaya na katili kiasi hicho! Ndicho unachotaka tukiamini?

Anyway tusipomuamini Rais unataka kutushauri tumwamini nani? Maana umeishia kusema tusimwamini Rais ila hujatoa huyo mwingine ambaye ww unaona anastahili aaminiwe!

Mm binafsi nachagua kumwamini na kuyaamini maamuzi na miongozo yake, maana siku zote namwomba Mungu ampe hekima ili aliongoze taifa letu vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli sitokaa tena nijibu mambo yake anayozungumza wala sitokaa nimuanzishie thread humu. Nasema kweli kabisa! Leo nimejua kumbe hata nchi yoyote ile duniani inaweza kuongozwa na kiumbe wa ajabu kama wananchi wake na watu wa maamuzi hawatakuwa makini.

Tanzania nadhani tumeletewa Huyu mtu ili tuelewe kuwa tunatakiwa kuchukulia kila jambo kwa umuhimu wake. Tunaonywa kuacha kupuuza vitu.

Magufuli nilikuwa natumia nguvu kuwaza vitu vya hovyo anavyoamua nilikuwa nakosea sana! Nilipaswa kutumia muda wangu kumfahamu zaidi akili yake! Mungu nisamehe! Zaidi ninafanya mambo yangu bila kumsikiliza yeye kwenye jambo lolote lile maana uwezo huo ninao! Ninafanya mambo yangu kwa kuizingatia akili yangu. Magufuli sitokaa nifuate kitu anachonielekeza maana nimemjua!

Huku tutakaa tukimbishania hata mtu ambaye hapaswi kubishaniwa huku zaidi ya kutibiwa. Hivyo sitokaa tena kubishana kuhusu mambo ya Magufuli. Mambo yenu na Magufuli wenu shauri yenu as far as hayanidhuru mimi na jamii yangu zaidi ya kuwaelimisha watu ambao kumbe na wao ni kina Magufuli wadogo!
Najua hii hotuba imekuuma sana,!
Taratibu utaelewa tu, hata darasanai kuna wanafunzi huwa inachukua muda kuelewa.

Viva JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom