Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Akihutubia Taifa(sina hakika kama ni sahihi kusema hivi) tokea Kanisa la KKKT Usharika wa Chato leo asubuhi, Rais Magufuli amelitangazia Taifa na ulimwengu kuwa mtoto wake ni miongoni mwa waliougua na kisha kupona Corona yumo mtoto wake hapo hajasema ni yupi.
Hii ni aina ya Kiki mbovu ambayo wanaompangia Rais (kama taasisi) kipi aseme na kipi asigusie wanaendelea kumpotosha. Anna Mgwira alipopata Corona alisema na kujitenga, amepona juzi akatutangazia na tumempa pole, lakini Leo ghafla mtu anajitokeza eti na kwangu kulikuwa na mgonjwa amepona Jana. Iwe kweli au uongo lakini kutuambia sasa hivi ni kutaka tuamini haogopi huu ugonjwa huku akiendelea kujificha kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app

Huyo Anna Mgwira alijitangaza ana Corona then juzi kasema kuna majani ameyatumia sasa akipimwa anaonekana ni Negative,hayo ndio maajabu tuliyobarikiwa.
 
“Kwa hali hii, kama wiki tunayoianza kesho itaendelea hivi nimepanga kufungua vyuo ili Wanafunzi wetu waendelee kusoma, lakini nimepanga pia kuruhusu michezo iendelee kwasababu michezo ni sehemu ya Burudani, maisha lazima yaendelee” -JPM


“Ugonjwa huu wa corona ni vita kama vita nyingine, wakati unaanza nilisema siwezi kuruhusu lockdown, imagine unafungiwa ndani hupati hata nafasi ya kuonana na Mkeo?, unafungiwa ndani eti usitembee usiku kana kwamba corona inatembea usiku tu, nikasema hapana” -JPM
#JPMChato

Source :Millard Ayo
 
Hovyooo!
tapatalk_1589390986199.jpeg


Au Modds mnasemaje?
 
Kama yapi?
Magufuli amepiga marufuku mwenge
Magufuli amepiga marufuku sherehe za muungano na pesa kapeleka visiwani zikapambane na corona
Magufuli amefuta mei mosi
Magufuli amefunga shule zote na vyuo
Magufuli amesimamisha michezo yote
Serikali ya magufuli ilitayarisha hosputali zake kwa ajili ya kupokea wagonjwa
Magufuli amesisitiza barakoa na kunawa mikono
Ulitaka Rais wetu afanye nini?mnyonge mnyongeni
Hiivi kikosi kazi cha Covid-19 mbona hatukisikii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli, katika Vita dhidi ya COVID-19, Niko na JPM. Kuna Mambo Kama nchi hatupaswi kuyapokea tuu bila kuangalia uhalisia wa kimazingira.
Halaf wadau, naomba kuuliza, Ni Nani aliyewaambia Wakenya na waganda kuwa Corona anaambukizwa usiku tuu mpka waweke lockdown ya usiku tuu? Na ikumbukwe usiku n nyakati ambazo mikusanyiko ya watu huwa midogo.
Au ndo kusema viongozi wao ni myopic mpaka wanashindwa kung'amua vitu common?
 
Nimemuelewa kama mtu aliye na matatizo ya akili na nitasimamia hilo. Nimeshasema hata nyie vimagufuli vidogo sipotezi tena muda na nyie na hii kwako ni reply yangu ya mwisho.
Nimekwambia hata darasani siyo wanafunzi wote huelewa kwa wakati mmoja, so hata wewe taratibu utamwelewa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1589712621914.png

Mungu ametusaidia na kwa taarifa za leo wagonjwa wamepungua sana Amana ilikuwa inalaza Watu 198, leo walikuwepo Watu 12 tu, Mlogonzila ilikuwa inalaza Watu 30 leo wamebaki 6, pale Kibaha Hospitali ilikuwa inalaza zaidi ya Watu 50 leo wamebaki Watu 22. Hata ktk Mikoa Arusha imebaki na wagonjwa 11, Mwanza 6, Dodoma 2, Mungu amejibu mombi yetu na ashukuriwe, kwa mwendo huu nataka kuwasisitiza kuchukua tahadhari, kama wiki hii tunayoianza kesho itaendelea hivi nimepanga kufungua vyuo - Rais Magufuli
 
"unafungiwa ndani eti usitembee usiku kana kwamba corona inatembea usiku tu, nikasema hapana” -JPM
Mzee wetu anavijembe kwelikweli
 
Kwa hiyo umeshindwa kujumlisha hapo ili tujue kuna wagonjwa wangapi?

Au Modds mnasemaje?
 
Back
Top Bottom