Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Bora angekaa tu kinywa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hamnaga akili nyie..hata kinachoonekana mtaani hamuoni,mmejaa upumbavu tu,mbona hamjafa mko hapa jf,kazi ni kuponda tu utadhani ninyi mnaakili kuliko wengine kumbe ni upuuzi tu..siasa na chuki za ukabila sijui zitawafikisha wapi

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Najiuliza vikaratasi alivyokuwa anasoma aliviandika akiwa kanisani au ametokanavyo home aliweka mfukoni?

Sina hakika kama waafrika tunamjua Mungu tunaemwabudu.

Kama Mungu angekuwa anamuadhibu mtu hapo hapo anapofanya kosa basi kuna viongozi midomo ingekwenda pembeni wakati wakihutubia kwa kufanya mzaha na Mungu.
Mungu wa kweli hayupo Kama udhanivyo! Mungu Ni mwenye rehema na upendo mwingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunajua usanii alioufanya Prof. Mabula Mchembe, ametoa wagonjwa wote karantini na hospitalini. Wale waliobaki ambao Magufuli kawataja leo ni wagonjwa walio katika hali mbaya sana. Hao ndiyo Mchembe katumwa wizarani kuwaruhusu wabaki hosipitalini. Yani wanaosubiri kufa!

Kama nchi mkishakuwa na kiongozi ambaye hajali kabisa binadamu wake lazima mjiulize sana!
 
Mhe. Rais Magufuli anatarajiwa kutuma salaam kwa Taifa leo Mei 17, 2020.

Hotuba yake inaaminika itajaa mambo mazito.

Kaa standby kwenye media zote na mitandao ya kijamii muda si mrefu ujao.

Inatarajiwa kuanzia mida ya saa sita na nusu mchana (12:30PM) ndipo atakuwa mubashara.

======




View attachment 1452519

‪RAIS AMETOA SALAAM BAADA YA KUSHIRIKI KATIKA IBADA YA KANISA LA KKKT USHARIKA WA CHATO‬

Raisi Magufuli akiwa katika kanisa la KKKT Chato amepata nafasi ya kuzungumza mbapo ameongea mambo mbalimbali,

Katika hotuba hiyo Raisi ameanza kwa kumshukuru Mungu na viongozi wa dini wote nchini. Raisi magufuli amesema “Waimbaji wameimba hapa kwamba bila mungu huwezi kuongoza, bila kumtanguliza mungu huwezi ukafanya chochote. Kwahiyo napenda niwashukuru Watanzania wote, Viongozi wa dini mbalimbali ambao wameshiriki kuliombea taifa hili"

"Na ndio maana siku za nyuma wakati ugonjwa huu umeingia niliwaomba ndugu zangu watanzania angalau tutumie siku tatu za kuomba kwelikweli. Ninawashukuru sana kwa sababu wote tuliomba tulifunga na Mungu amejibu na Mungu ametusikia”

“Ndugu zangu mifano mingi imetolewa, hata katika mahubili yako leo Baba Mchungaji katika injili na katika matendo ya mitume umeeleza ni namna gani watu walivyoweza kumtegemea Mungu walivyoweza kufanikiwa”

“Yule kipofu alimlilia yesu, Mwana wa Daudi nirehemu, Yesu ambaye ni mtoto wa Mungu ambaye naye pia ni Mungu alimponya. Wakati wa dhoruba kula baharini wanafunzi walivyokuwa wamelala wakaona mtumbwi unataka kuzama walipiga kelele” Katika maandiko pia sehemu zingine Yesu aliwakemea kwanza mitume kwa kuwa na Imani ndogo na baadaye akaikemea pepo na mambo yakawa shwari kwahiyo sisi katika kipindi chochote kigumu cha aina yoyote tukimtanguliza Mungu tutafanikiwa”

“Kwahiyo ninawashukuru sana ndugu zangu, ninawashukuru sana Wachungaji, Masheikh, Mapadri, Maaskofu kila mmoja katika eneo lake ambao tulimtanguliza Mungu na Mungu ametusaidia sana”.

“Ndugu zangu katika mapambano ya aina yoyote ni vita. Ugonjwa huu wa Corona hauna tofauti na vita nyingine. Nilikwisha eleza na wataalamu pia wameahaeleza ni namna gani nzuri ya kuweza kupambana na ugonjwa huu hata Baba Mchungaji umezieleza mbinu zote”.

“Ni kweli sikutoa amri ya lockdown ya kuwafungia watu majumbani, ulikuwa ni utumwa wa ajabu. Imagine wewe Lyabange ufungiwe saa nyingine hata usionane na Mme wako Iseme au na watoto wako. Sisi hapa huwa tunaondoka asubuhi kwenda kuchukua chakula, ukachume viazi, maharage yako, uende ziwani ukavue hivyo vyote vingekuwa vimezuiliwa tungekuwa tuko wapi sisi Watanzania miliono 60?"

Huruhusiwi kwenda sokoni, na saa nyingine unaruhusiwa kutoka kidogo tu, halafu usiku usitoke kana kwamba Corona inatembea usiku tu. Hebu tujiulize sisi Watanzania tuna miradi mingi tumeweka katika nchi yetu, Hiyo miradi yote ingekuwa imesimama.

"Tunajenga reli kwa mabilioni ya fedha, Makandarasi kutoka Nje wale wote tungewazuia vijana wasipate kazi tungekuwa wapi?"

"Tunajenga Mradi wa umeme, thamani yake ni Zaidi ya Trilioni saba zimechukuliwa na Watanzania kwenda kuinvest pale kusudi tuwe na umeme, leo wale wote tungekuwa tumewasimamisha, vijana wale wote tungekuwa tumewasimamisha; tunajenga barabara zote zingekuwa zimesimama."

"Hapo tunajenga meli kwenye ziwa Viktoria na juzi mmeona Injini zimekuja kutoka Korea, zote zile zingekuwa tumesimamisha na injini zisingekuja."

“Kila mmoja afikirie katika maeneo yake tungekuwa wapi? Ndio maana nilimuomba sana Mungu na nawashukuru sana viongozi wa dini zote nikasema hapana, hakuna kujifungia ndani kwa sababu huu utakuwa ugonjwa mkubwa Zaidi kuliko Corona”

Lakini watu ukishawafungia ndani utawalisha chakula? Watafanyaje? Sitaki kueleza matatizo wanayoyapata katika maeneo mengine nyinyi wenyewe mnajua lakini sisi tumeamua kwenda hivi.

Tuliamua tumtangulize Mungu, tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu. Na katika hali halisi Mungu amesikia sala zenu kwa taarifa za leo nilizoletewa na naomba niwaeleze kidogo nilizoandika hapa.

Wagonjwa wamepungua san ahata katika hospitali zetu; Mfano Hospitali ya Amana ya Dar es Salaam ilikuwa inalaza watu 198, leo walikuwepo watu 12 tu.

- Hospitali ya Mloganzila ilikuwa inalaza watu 30 leo wamebaki 6

- Pale kibaha palikuwa pana kituo kinaitwa Rulanzi huwa wanalazwa pale Zaidi ya watu 50 leo walikuwa wamebaki 22 na hawa 22 sio kwamba wamezidiwa wako kama sisi ila tu ado wanaonesha positive.

- Kwenye hospitali ya Agha Khani nako wamepungua wamebaki watu 31,
- Hindu Mandal wamebaki 16,
- Ragent Hospital wamebaki 17,
- TMJ wamebaki 7,
- Labinisia kule Tegeta wamebaki watu 14

"kwahiyo, unaweza kuona trend ya majibu ya Bwana Mungu wetu yalivyofanya kazi".

"Lakini pia hata katika mikoa, Arusha wana vituo vitatu.
- Mshono kina wagonjwa 11,
- Longido jina la kituo linaitwa Nyorendeke hakuna mgonjwa hata mmoja.
- Karatu kuna kituo kinaitwa Dofu hakina mgonjwa.

"Mwanza hapa wana vituo jumla kumi, vinane ni kutoka Halmashauri zifuatazo;

- Busweru wana wagonjwa wawili
- Misungwi wana wagonjw wawili wote wana hali nzuri
- Ukerewe kuna kituo kinaitwa Nyakatunguru hakuna hata mgonjwa mmoja
- Nagu kuna kituo kinaitwa John Mongela hakuna mgonjwa
- Jiji la Mwanza kituo cha Mkuyuni hakuna mgonjwa
- Buchosa kituo cha Nyamunge hakuna mgonjwa
- Sengerema hakuna mgonjwa
- Kwimba hakuna Mgonjwa
- Hospitali mbili za Bugando na seketule Wagonjwa ni wawili hao wana uhitaji wa kuangaliwa kwa sababu pia wana magonjwa mengine.


.

Taarifa swafii! Tufungue shule, vyuo, shughuli za burudani na siasa, na shughuli zingine za biashara. Hii inatokana na idadi ya wagonjwa ni kidogo mno (129) compared to 60 million people. Tusiogope. Shule zifunguliwe haraka.
 
Nikikumbuka uongo wake kwenye sakata la korosho, siwezi kumuamini huyu jamaa, labda baada ya kuvuta bangi ya lumumba inayolimwa na chakubanga.
Yeye yuko vichakani, halafu anatuambia sisi tuchape kazi.
kama unataka kujifungia kajifunge mzee, hujalazimishwa
 
Unaweza kutuwekea vipimo vya daktari hapa ambavyo kigogo kakuonesha kwamba huyo uliyemtaja ana corona?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kama kusoma haujui picha tu unaona na ni kipimo tosha,kifo cha marine kiliondoka na co-workers wenzake wawili huku wenzao watatu wakipata matibabu mloganzira.

Proof ya pili ni aina ya mazishi yao yaani ni watu 10 tu huku ikisimamiwa na "WAJUBA" wa manispaa hapo ni kipimo tosha kwamba ni FUTA tu.
 
Hili Ni tatizo
IMG_20200517_141251.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama kusoma haujui picha tu unaona na ni kipimo tosha,kifo cha marine kiliondoka na co-workers wenzake wawili huku wenzao watatu wakipata matibabu mloganzira.

Proof ya pili ni aina ya mazishi yao yaani ni watu 10 tu huku ikisimamiwa na "WAJUBA" wa manispaa hapo ni kipimo tosha kwamba ni FUTA tu.
Basi wewe endelea kuomboleza hivyo vifo na huyo kigogo tuache sisi tuchape kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamnaga akili nyie..hata kinachoonekana mtaani hamuoni,mmejaa upumbavu tu,mbona hamjafa mko hapa jf,kazi ni kuponda tu utadhani ninyi mnaakili kuliko wengine kumbe ni upuuzi tu..siasa na chuki za ukabila sijui zitawafikisha wapi

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
Wajinga Sana hawa watu, dj na kundi lake walikimbia bunge wakiogopa Corona halafu wakarudi bungeni Tena!! Yaani akili za hawa watu zilishatekwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom