Magufuli amesema ni ujinga wa kupitiliza kwa nchi ambazo zimeizunguka Tanzania kujaribu kufunga mipaka yao na Tanzania kwasababu nchi hizo zinaitegemea sana Tanzania.
Ametolea mfano kwa nchi moja(Kenya) ambayo inaitegemea Tanzania kwa mahindi, mchele na hata mifugo(nyama), kutangaza kufunga mipaka wakati ikijua kwamba hawana chakula cha kutosha.
Magufuli anategemea kufungua shule na vyuo vya elimu na kuruhusu ndege kuanzia safari zake za kawaida ndani ya wiki mbili zijazo kutokana na hali ya ugonjwa wa Corona kutengemaa nchini.