Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Haya majibu yalitokana na vipimo vya maabara ipi? ile ile iliyosema kuwa haitoi majibu sahihi? au kulikua na maabara nyingine tofauti na hii?
last time we was told maabara imesitisha kufanya vipimo kupisha uchunguzi..may be this are previous data
 
Haya majibu yalitokana na vipimo vya maabara ipi? ile ile iliyosema kuwa haitoi majibu sahihi? au kulikua na maabara nyingine tofauti na hii?
Hawa walipimwa maabara tofauti akiwemo mtoto aliyekuwa anakunywa tangawizi na malimao pamoja na kujifukiza na sasa tunapiga push-ups.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi mabeberu wamezingua tena nini?!.

Sent using Jamii Forums mobile app
C778BDD9-5B5E-4ED5-B1FB-840E02DB9056.jpeg
 
Hakuna kitu alishawahi kuongea ukakubali
Fatilia post zangu uone, nimekubaliana naye kama 50% na kumpinga kama 50%. Mimi sio sifiasifia kila kitu wala pondea kila kitu, vipo vitu vingi tu namuunga mkono, lockdown isiwepo naunga mkono, alivyopambana na wachina naunga mkono, kuzuia watoto waliopata mimba wasisome nimepinga, umeme stiglers gorge nimeunga mkono, anavyomkumbatia bashite nimepinga sina chuki na magufuli wala nini. Natumia akili sio matako
 
Duh . . .noma sana
Mkuu hatuongea kuchengemsha genge ni true story njiro ni misiba kila siku muulize hata Lema,nimumuuliza jamaa yangu wa njiro kaniambia njiro hatari haipiti siku anakatika mtu kwa korona na hadi Baruani Mshale(Ni Mkurugenzi wa Mikakati -Twaweza) aliconfirm BBC Swahili akihojiwa na Kikeke kuwa shangazi yake wa njiro alifariki kwa korona,
 
Kwa kifupi ni kwamba kama afya yako mgogoro, umri wako umeenda au unampendwa kwenye classification za hatari ni jukumu lako kujikinga na Corona as far as Magu is concerned anajua upo sana hila watu wanapona pia.

Tena leo kaingia kwenye mchanganyiko kama zuga mbona yeye aogopi umati be it at safe distance na si ajabu waumini wote waliwekwa karantini ya wiki mbili kwanza.
 
We worship God,

others like Chadema worship corona

Thank you Mr President
 
Mhe. Rais Magufuli anatarajiwa kutuma salaam kwa Taifa leo Mei 17, 2020.

Hotuba yake inaaminika itajaa mambo mazito.

Kaa standby kwenye media zote na mitandao ya kijamii muda si mrefu ujao.

Inatarajiwa kuanzia mida ya saa sita na nusu mchana (12:30PM) ndipo atakuwa mubashara.

======



‪RAIS AMETOA SALAAM BAADA YA KUSHIRIKI KATIKA IBADA YA KANISA LA KKKT USHARIKA WA CHATO‬

Raisi Magufuli akiwa katika kanisa la KKKT Chato amepata nafasi ya kuzungumza mbapo ameongea mambo mbalimbali,

Katika hotuba hiyo Raisi ameanza kwa kumshukuru Mungu na viongozi wa dini wote nchini. Raisi magufuli amesema “Waimbaji wameimba hapa kwamba bila mungu huwezi kuongoza, bila kumtanguliza mungu huwezi ukafanya chochote. Kwahiyo napenda niwashukuru Watanzania wote, Viongozi wa dini mbalimbali ambao wameshiriki kuliombea taifa hili"

"Na ndio maana siku za nyuma wakati ugonjwa huu umeingia niliwaomba ndugu zangu watanzania angalau tutumie siku tatu za kuomba kwelikweli. Ninawashukuru sana kwa sababu wote tuliomba tulifunga na Mungu amejibu na Mungu ametusikia”

“Ndugu zangu mifano mingi imetolewa, hata katika mahubili yako leo Baba Mchungaji katika injili na katika matendo ya mitume umeeleza ni namna gani watu walivyoweza kumtegemea Mungu walivyoweza kufanikiwa”

“Yule kipofu alimlilia yesu, Mwana wa Daudi nirehemu, Yesu ambaye ni mtoto wa Mungu ambaye naye pia ni Mungu alimponya. Wakati wa dhoruba kula baharini wanafunzi walivyokuwa wamelala wakaona mtumbwi unataka kuzama walipiga kelele” Katika maandiko pia sehemu zingine Yesu aliwakemea kwanza mitume kwa kuwa na Imani ndogo na baadaye akaikemea pepo na mambo yakawa shwari kwahiyo sisi katika kipindi chochote kigumu cha aina yoyote tukimtanguliza Mungu tutafanikiwa”

“Kwahiyo ninawashukuru sana ndugu zangu, ninawashukuru sana Wachungaji, Masheikh, Mapadri, Maaskofu kila mmoja katika eneo lake ambao tulimtanguliza Mungu na Mungu ametusaidia sana”.

“Ndugu zangu katika mapambano ya aina yoyote ni vita. Ugonjwa huu wa Corona hauna tofauti na vita nyingine. Nilikwisha eleza na wataalamu pia wameahaeleza ni namna gani nzuri ya kuweza kupambana na ugonjwa huu hata Baba Mchungaji umezieleza mbinu zote”.

“Ni kweli sikutoa amri ya lockdown ya kuwafungia watu majumbani, ulikuwa ni utumwa wa ajabu. Imagine wewe Lyabange ufungiwe saa nyingine hata usionane na Mme wako Iseme au na watoto wako. Sisi hapa huwa tunaondoka asubuhi kwenda kuchukua chakula, ukachume viazi, maharage yako, uende ziwani ukavue hivyo vyote vingekuwa vimezuiliwa tungekuwa tuko wapi sisi Watanzania miliono 60?"

Huruhusiwi kwenda sokoni, na saa nyingine unaruhusiwa kutoka kidogo tu, halafu usiku usitoke kana kwamba Corona inatembea usiku tu. Hebu tujiulize sisi Watanzania tuna miradi mingi tumeweka katika nchi yetu, Hiyo miradi yote ingekuwa imesimama.

"Tunajenga reli kwa mabilioni ya fedha, Makandarasi kutoka Nje wale wote tungewazuia vijana wasipate kazi tungekuwa wapi?"

"Tunajenga Mradi wa umeme, thamani yake ni Zaidi ya Trilioni saba zimechukuliwa na Watanzania kwenda kuinvest pale kusudi tuwe na umeme, leo wale wote tungekuwa tumewasimamisha, vijana wale wote tungekuwa tumewasimamisha; tunajenga barabara zote zingekuwa zimesimama."

"Hapo tunajenga meli kwenye ziwa Viktoria na juzi mmeona Injini zimekuja kutoka Korea, zote zile zingekuwa tumesimamisha na injini zisingekuja."

“Kila mmoja afikirie katika maeneo yake tungekuwa wapi? Ndio maana nilimuomba sana Mungu na nawashukuru sana viongozi wa dini zote nikasema hapana, hakuna kujifungia ndani kwa sababu huu utakuwa ugonjwa mkubwa Zaidi kuliko Corona”

Lakini watu ukishawafungia ndani utawalisha chakula? Watafanyaje? Sitaki kueleza matatizo wanayoyapata katika maeneo mengine nyinyi wenyewe mnajua lakini sisi tumeamua kwenda hivi.

Tuliamua tumtangulize Mungu, tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu. Na katika hali halisi Mungu amesikia sala zenu kwa taarifa za leo nilizoletewa na naomba niwaeleze kidogo nilizoandika hapa.

Wagonjwa wamepungua san ahata katika hospitali zetu; Mfano Hospitali ya Amana ya Dar es Salaam ilikuwa inalaza watu 198, leo walikuwepo watu 12 tu.

- Hospitali ya Mloganzila ilikuwa inalaza watu 30 leo wamebaki 6

- Pale kibaha palikuwa pana kituo kinaitwa Rulanzi huwa wanalazwa pale Zaidi ya watu 50 leo walikuwa wamebaki 22 na hawa 22 sio kwamba wamezidiwa wako kama sisi ila tu ado wanaonesha positive.

- Kwenye hospitali ya Agha Khani nako wamepungua wamebaki watu 31,
- Hindu Mandal wamebaki 16,
- Ragent Hospital wamebaki 17,
- TMJ wamebaki 7,
- Labinisia kule Tegeta wamebaki watu 14

"kwahiyo, unaweza kuona trend ya majibu ya Bwana Mungu wetu yalivyofanya kazi".

"Lakini pia hata katika mikoa, Arusha wana vituo vitatu.
- Mshono kina wagonjwa 11,
- Longido jina la kituo linaitwa Nyorendeke hakuna mgonjwa hata mmoja.
- Karatu kuna kituo kinaitwa Dofu hakina mgonjwa.

"Mwanza hapa wana vituo jumla kumi, vinane ni kutoka Halmashauri zifuatazo;

- Busweru wana wagonjwa wawili
- Misungwi wana wagonjw wawili wote wana hali nzuri
- Ukerewe kuna kituo kinaitwa Nyakatunguru hakuna hata mgonjwa mmoja
- Nagu kuna kituo kinaitwa John Mongela hakuna mgonjwa
- Jiji la Mwanza kituo cha Mkuyuni hakuna mgonjwa
- Buchosa kituo cha Nyamunge hakuna mgonjwa
- Sengerema hakuna mgonjwa
- Kwimba hakuna Mgonjwa
- Hospitali mbili za Bugando na seketule Wagonjwa ni wawili hao wana uhitaji wa kuangaliwa kwa sababu pia wana magonjwa mengine.

Lakini Dodoma kuna vituo vinne mjini viko viwili vina wagonjwa wawili kwa vyote wanahitaji uangalizi na karibu na pia wanamagonjwa mengine, wawili walikuwa wagonjwa Zaidi ya arobaini na kitu wengine wote wamerudi nyumbani.

- Kongwa hakuna mgonjwa
- Kondoa tuna kituo kinaitwa Baleko hakuna mgonjwa. Na kadhalika na kadhalika

Kwahiyo, Mungu amejibu maombi yenu, Mungu amejibu maombi yetu, na Mungu ashukuriwe sana kwa kutusikiliza. Kwa mwendo huu nataka niendelee kuwasisitiza muendelee kuchukua tahadhari, tuendelee kumuomba. Na tahadhari hizi ambazo tumeendelea luzichukua tuendelee nazo.

Na kwa trend hii ninavyoiona hapa, kama wiki hii tunayoianza kesho itaendelea hivi nimepanga kufungua Vyuo ili wanafunzi wetu waendelee kusoma. Lakini nimepanga pia sisi kama taifa kuruhusu michezo iendelee kwa sababu michezo ni sehemu moja ya burudani kwa Watanzania.

Lakini pia, mpaka ninavozungumza hapa kuna Mashirika ya ndege sitaki kuyataja hapa yameshabook watalii, wengine mpaka mwezi wa nane ndege zimejaa kwa ajili ya kuja Tanzania kuanza kutalii.

Wanakuja kwa sababu wanaujua ukweli, wanakuja kwa sababu Tanzania ni pazuri. Na mimi nimeshatoa maagizo kwa Waziri wa Maliasili pamoja na Waziri wa Uchukuzi waruhusu hizo ndege ziingie na wala hawatawawekea karantini. Akishafika hapa akapimwa Tmperatute akakutwa temperature iko kawaida hana dalili za Corona, aende akaangalie wanyama akakoronaizi huko akaende vizuri.

Hatuwezi sisi kama taifa huru tukakubali Corona itawale. Mungu wetu atatawala lakini Corona haitatawala.

Ttumekuwa na magonjwa mengi, magonjwa kama Ukimwi nayo ni Virus, Surua ni Virus na kadhalika, lakini hatujakubali yakatawala.

Uchumi wetu ni namba moja kwanza, tukiufanya uchumi wetu ukalala hata mishahara hatutalipa, hata sadaka tutakosa au uongo baba? Leo pasingekuwa na misa hapa sadaka ingepatikana? Hamna! Toleo la kumi kwa Bwana wetu Mungu tusingetoa. Kwa hiyo, maisha lazima yaende. Lakini nitoe wito kwa Watanzania, pamekuwa na maneno mengi ya kuongezwa ongezwa na kutiwa chumvi. Narudia hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko ugonjwa wa Corona.

Inawezekana watu wamepoteza maisha kwa sababu ya hofu au kudanganywa. Yuko rafiki yangu mmoja Injinia, na nataka niutoe mfano wa kweli alipata strock nyumbani, akabebwa akapelekwa Muhimbili pale Jakaya Kikwete akiwa amepata Strock, kuharusi

Amekaa pale baada ya siku mbili tatu akiendelea kutibiwa wakampima Corona wakasema ana Corona, Wakamtoa pale Muhimbili Jakaya Kikwete Centre kwamba huyu ana Corona anapelekwa Amana.

Amepelekwa pale Amana, akalazwa kwenye kitanda watu wanamuogopa ana Corona. Baadaye ndugu zake wakasemakuwa hapa kama bado amechelewa kushughulikiwa hivi tumchukue. Wakampeleka kwenye hospitali ya Agha Khan, na kule kwa sababu alikuwa ameshaambiwa ana Corona akatafutiwa chumba kimoja akaambiwa atoe advance kwanza miliono 6.

Wakachangishana wakatoa hizo miliono 6, wakachukua tena vipimo walivyoenda kumpima wakamkuta hana Corona, ndipo wakamuhamisha, wakamuhamishia kwenye wodi ya kawaida. Sasa hivi ameshapona yuko nyumbani anazungumza,

Kwahiyo unaweza ukaona ni kwa namna gani wengine wamepoteza kwa sababu ya kufikia Corona, Corona Corona. Wapo Wauguzi na Madaktari walikuwa wanafanya Muhimbili na kadhalika kwenye siku za mwanzo walikutana na wagonjwa kuwahudumia. Wakaenda wakafungiwa kwamba lazima wakae siku 14 walikuwa Madaktari 60 pamoja na Manesi.

Sasa ukishakuwa Daktari ni kwa namna gani utaacha kukutana na mgonjwa was Corona?

Nilipokutana na hizi habari nikasema wafungulie kwa sababu kukuitana na Wagonjwa wa Corona ndio wajibu wao. Wanaendelea na kutoa huduma. Kwa hiyo katika mipango hii ya kupambana na Corona kuna mambo mengi yameingizwa ya hovyo humu ndani.

Wapo watu wamekuwa wakifariki kwa ugonjwa mwingine, kwanza wanang’ang’ania kumpima. Huyo ameshafariki unampima umfanye nini? Nguvu za kupima wanazo lakini za kumhudumia mpaka afariki hawana. Na akipima kila kitu kinaandikwa Corona. Na wanamzuia asiende kuzikwa na ndugu zake. Sasa kama umempima unaogopaje kuwaruhusu ndugu zake wakamzike mahali walipo. N mbinu za ajabu, za hovyo.

Kwa hiyo nitoe wito kwa Madaktari kwa sababu najua watanisikia na Wizara ya Afya mtu atakapofariki kw ugonjwa wowote hata kama ni kwa Corona afikishwe na aheshimiwe kwa maziko ya kawaida kutokana na heshima ya uanadamu Corona sio Ebola!! Mbona wa Ukimwi hatuwatengi? Nao tuwatupe hukohuko. Mnona wa TB hatufanyi hivyo? Mbona wa Surua hatufanyi hivyo nao ni virus?

Ni muelekeo tu wa hovyo ambapo saa nyingine watu wetu tumekuwa tukidanganywa. Mimi napozungumza hapa nina Mtoto wangu alipata Corona, Mtoto wa kuzaa mimi!! Amejifungia kwenye chumba akaanza kujitibu akajifukizia, akanywa malimao na tangawizi, amepona yuko mzima sasa anapiga push up.

Huu ndio ukweli siwezi nikasema uongo mbele ya madhabahu hapa kwa sababu ninamuheshimu Mungu wangu, Na nampenda Mungu wangu nampenda Yesu wangu siku zote. Kwa sababu wanaweza kufikiri labda mimi hili halijanipata, mtoto wangu wa kuzaa.



.
Duh[emoji856][emoji856][emoji856]

Its not over until its over...[emoji769]
 
Hiyo sana toa. Wanaopona ni wengi kuliko wagonjwa wapya na mwisho wa siku wataisha. Ninawashangaa watu kuikomalia Tanzania wakati si miongoni mwa nchi zenye maabukizi. Hata majirani zetu wa kaskazini mashariki wana maambukizi mengi zaidi. Afrika maambukizi mengi yako Afrika ya kusini, Afrika ya kaskazini na Aftika Magharibi. Sisi Afrika mashariki ikiwemo nchi yetu maambukizi ni kidogo sana. Lakini dunia nzima inapigia makelele nchi yetu utafikiri wana hasira fulani na sisi vile! Huwezi kuwasikia wakizungumzia nchi zenye maambukizi kwa maelfu!! Watukome!

Sent using Jamii Forums mobile app
Apo umezungumza kama mlevi wa gongo kilabuni.COVID-19 ni janga la kidunia.Kuna faida nyingi za kupima na kutoa takwimu katika kudhibiti ugonjwa.Ni kama upimaji na utoaji wa takwimu ulivyosaidia katika ukimwi.
Bila ya kuwa na mkakati watanzania wengi watafariki kimya kimywa.Kumbuka 1% ya wanaopata ugonjwa huu hufariki.Tupo 55 milioni.Je 1% ya watu milioni 55 ni watu wangapi?
 
Mkuu hatuongea kuchengemsha genge ni true story njiro ni misiba kila siku muulize hata Lema,nimumuuliza jamaa yangu wa njiro kaniambia njiro hatari haipiti siku anakatika mtu kwa korona na hadi Baruani Mshale(Ni Mkurugenzi wa Mikakati -Twaweza) aliconfirm BBC Swahili akihojiwa na Kikeke kuwa shangazi yake wa njiro alifariki kwa korona,

[emoji205][emoji205][emoji205][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi ninyi mnaodai lockdown si mjifungie wenyewe ndani na wake zenu mtuache sisi tutembee.Hapa mtaani kwetu kuna wazungu a.k.a mabeberu wapo nje kiguu na njia tena hata hawavai barakoa.Kama kufungiwa ndani ni vizuri hawa wazungu si wangebaki ndani kutii maagizo ya balozi zao?
 
Back
Top Bottom