Watanzania ni wabunifu na watundu sana.
Wanajua kuzoea shida haraka na kupunguza makali yake.
Mbinu za kujifukiza, kunywa juisi ya tangawizi, limau, vituunguu na pilipili kichaa imewafanya wengi wanapohisi kuwa na tatizo la mafua au homa, hutumia vitu hivi na kujifungia ndani na kujiweka karantini (isolation room) wakiendelea kupata huduma za madawa haya na lishe nzuri.
Wameambiwa corona haina tiba kwa hiyo kupelekwa hospitali ni kuepuka kuambukiza wengine na kupata huduma zingine za kitabibu kwa magonjwa mengine yanayojitokeza baada ya mtu kuugua corona. Mbinu zote mbili za kujiepusha kuwaambukiza wengine na kutibu magonjwa mengine tofautu na corona, zinatumika hata mtu akiwa nyumbani (isolation room) kwa mafanikio makubwa.
Mbinu hii pengine inaweza kuwa ngumu kidogo kwa watu wanaopanga nyumba moja na hawawezi kupata chumba cha kujiweka karantini( isolation room).
Pengine mbinu hii inaweza kuwa imepunguza idadi ya wagonjwa wanaotibiwa na Serikali na kwa ujumla inaweza kuwa salama na nafuu kwa mgonjwa kuliko kuchanganywa na wagonjwa wengi wa corona.
Tukumbuke vipimo vyetu vimethibitika kuwa si sasa asilimia mia moja kwa hiyo mgonjwa anaweza kupimwa na akaonekana ana maambulizi na kupelekwa kwenye isolation hospital na baadaye huko huko akaambukizwa corona ambayo alikuwa hana.
Hongera Watanzania, Hongera Mh. Rais Makufuli na mkuu wa mkoa wa Dar kwa ujasiri wa kupambana na ugonjwa wa corona kwa mbinu za kisaikolojia na kushawishi watu kutumia dawa mbadala badala ya kutegemea zile za wazungu tu.
Mzungu ni sawa na kuku wa kisasa, akiugua kila kitu atategemea daktari aje amuhudumie.
Mtanzania ni sawa na kuku wa kienyeji, chakula na dawa anajitafutia mwenyewe na ukufika muda wa kuingia ndani hurudi mwenyewe bila kushurutishwa na mtu.