Rais Magufuli, hili la Kangi Lugola hujatenda haki. Sheria ya Uhujumu Uchumi inawahusu wananchi tu?

Hata Warioba alisema, vita dhidi ya ufisadi haipiganwi kwa viongozi na wanasiasa. Hao wamekuwa kama untouchables
 
Tujiulize? Ni mambo mangapi ýa kifedha yamefanyika pasipo kufuata sheria au bila idhini ya bunge? TUMUACHIE MUNGU

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Jamani naombeni sana Mh rais mumuache mambo mazuri mengi mno ametufanyia jamani mtamkumbuka sana Huyu rais mimi binafsi namkubali sana Pamoja Na maneno yenu Mabaya lakini magufuli anawawekea lami nyakanazi Mpaka Kigoma mkoloni mwenyewe aliishindwa hiyo barabara. Tunduma Mpaka sumbawanga pasuliwa Mpaka Katavi inaunga Mpaka Kigoma Tena.Zito uwe Na adabu na shukrani Mungu anakuona


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Maarifa yako madogo sana.!!

Hapa tunazungumzia hatua za ziada ambazo Mh Rais na vyombo vya Usalama vinanapaswa kuchukua na sio ujenzi wa barabara

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ahsante sana Mjomba kwa comment yako nzuri.

Chaajabu Kangi anasema Rais amempumzisha. That is very strange.

Unajua ni wakati sasa Magufuli tuwe serious , honestly.

Hii mambo ya tumbua tumbua bila kuwajibishwa ifike pahala utambue kwamba tumechoka na haya Maigizo.

Mimi nakupenda sana Magufuli na Mimi ni muumini wako naliweka bayana hilo ; kuna Uharo mwingi umejitahidi kuufumua katika nchi iliyokuwa imeoza. Bravo katika hilo


Ila Kangi na timu yake wanapaswa kuwa Jela badala yke anasema UMEMPUMZISHA, like serious.

Attachment, below
 
Kangi lugola na timu yake Ni wahujumu uchumi inatakiwa wachukuliwe hatua za kisheria. Wakiachwa hivyo Basi watanzania tutajua kuwa Kangi alikuwa anatekeleza ilani aliyokuwa anatembea nayo.

Kabisa. Huyu Mtu ni kwenda Jela ndiyo Hii Tumbua italeta mantiki
 

Safi sana Critical thinker. This is the thing.

Hii ishu kama Magufuli asipomfikisha huyu mahakamani ; basi something is wrong with the whole system.
 

Amesema AG alienda kuzika.

Waliokaimishwa majukumu ndiyo waliopitisha.

Ni dhahiri kuwa baada ya kurudi ndiyo akakuta hiyo Mikataba na akawatonya state kujisalimisha.

Mikataba inayoenda Kwa AG ( mwanasheria Mkuu ) ni Ile yenye Value ya Kuanzia Mil 500 kwenda juu.

Hii mingine inaweza kusainiwa Wizarani hapo hapo kwa kutumia wanasheria wa Wizara.
 

Wewe mbona huna akili .

Kama walisaini huko huko nje , Mkataba ulifikaje kwa Mwanasheria Mkuu.

Public Procurement Act 2011 na Régulation yake ni lazima kwanza kabda ya kusaini Mkataba kama huo ni lazima uende kwa AG, na walifanya hivyo .

Halafu usitupangie cha kujadili, be liberal, mbona sisi hatukupangii cha kuandika.

This is JamiiForums, the land of opportunity to learn and to be exactly who you were meant.
 

Matumizi ya budget 2019 ni 23 trillion, watu wainaingia mkataba wa trillion 1.6 bila idhini ya bunge hii inawezekanaje?
 

Kwahiyo kila mtu anae comment hoja za msingi ni Zitto ? Hivi mbona sisi wa TZ hatuna akili , haki vile.

Je ni wapi tumepinga juhudi za Rais ?

Tunachojadili hapa ni what is the culminating result ya hizi tumbua tumbua?

Je hawa watu sawa wametumbuliwa lakini je hatua za kisheria ni zipi ?

Grow up man usichague ujinga.
 
We mbona bwege sana...
mikataba inatakiwa kusainiwa hapa nchini tena ukiwa na wataalamu maana unaweza kuchezewa ujanja hko nje ata ukasaini ukiwa umelewa ukaingiza nchi matatizoni, pili hamna niliposema ofisi ya mwanasheria mkuu haikuuona! Jifunze kusoma kiwerevu,tatu sijampangia mtu ajadili nini Ila nimesema msijidai wachunguzi huku uhalisia hamuujui. Soma kwa kuelewa sio kwa mihemuko kijana,pole
 

Kusaini Mkataba Huko huko ughaibuni una maanisha nini ?
 
Kangi ni TISS yupo kazini ila utakuja kujua baada mission kukamilika tena Magu ndiyo atatoboa siri!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumemsikia wenyewe Rais wetu, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, alipokuwa akitengua uteuzi wa waziri wa mambo ya ndani, Kangi Lugola, akitoa sababu kuwa ni kutokana na waziri huyo kusaini mkataba nje ya nchi, wa kuingiza vifaa vya zimamoto, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi trillion moja

Kama madai ya Rais Magufuli ni ya kweli, ni kwanini Jeshi la Polisi nchini halijamkamata Mheshimiwa Lugola na kumfungulia mashitaka ya utakatishaji wa pesa nyingi kiasi hicho?

Tunajua kuwa yupo mwandishi wa habari, Eric Kabendera, anayeendelea kusota rumande, kwa zaidi ya miezi 6 sasa, kwa tuhuma za utakatishaji pesa wa shilingi milioni 170

Tunajua pia yule mfanyakazi wa kituo cha haki za binadamu, Tito Magoti, naye amefunguliwa mashitaka ya utakatishaji pesa wa shilingi milioni 17 pekee!

Inakuwaje kwa hawa akina Lugola, ambapo kwa Maelezo ya Rais wetu Magufuli, amewatuhumu kushiriki kusaini mkataba wa kununua vifaa vya thamani ya zaidi ya shilingi trillion moja, waeendelee kukaa uraiani, ambapo Rais mwenyewe ametuhakikishia kuwa wanahusika na utakatishaji pesa wa zaidi ya shilingi trillion moja?

Hivi ni kipi kikubwa ni trillion moja ya Kangi Lugola au shilingi milioni 17 za Tito Magoti?

Kama Kangi Lugola hajafunguliwa kesi ya utakatishaji pesa basi tutajua kuwa hili suala ni la kisiasa

Tusaidiane katika kulidadavua suala hili kwa maslahi mapana ya Taifa letu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…